Jamani huyu msichana mie simuelewi. Naombeni ushauri

Habari za saa hizi wana jukwaa.

Kwanza nikiri kabisa, nimekuwa single kwa mda mrefu na hii ni kutokana na kukataliwa na waschana wengi niliokuwa nikiwatongoza. Baada ya hapo nikaamua kupotezea mchongo wa mahusiano so sikutaka kujihusisha kimahusiano na msichana yeyote.

Sasa juzi hapa kazini kwetu alikuja msichana fulani kufanya field ambapo wakati anaanza field mie nilikuwa likizo hivyo nilikuja kurudi kazini nikakuta kashakuwa mwenyeji na kashazoeana na watu hapa kazini.

Mara ya kwanza hatukuzoeana sana nae, hivyo zaidi ya salamu tulikuwa hatuzungumzi kitu ila ni mtu fulani muongeaji sana (yaani sana) kwahiyo alikuwa ananiongelesha mambo madogo madogo kama 'Joel mida ya kuondoka imefika, vipi bado upo?' sasa katika kuzungumza mambo madogo kama hayo akawa ameanza kunizoea hivyo akaanza kuniletea utani wa hapa na pale.

Sasa kuna kipindi pale kazini kulikuwa na tukio maalumu kwahiyo wafanyakazi walikuwa wanakuja wachache tena vijana tu, wale wengine walikuwa wanaenda huko kwenye hilo tukio. Kwa nafasi hiyo ya watu kuwa wachache akawa ananiletea utani flani hivi ambao ulianza kunistua na kuamsha hisia zangu.

Alikuwa ananiita na kuanza 'Joel, daah nimekumiss sana' akinambia hivo namchunia mara 'Joel, kwani mi huwezi kunioa? Nna kasoro gani?' au wakati mwingine anasema: 'Joel, I love you' au anaweza sema 'Joel, nakosa usingizi kwa ajili yako', sasa mie nilikuwa nachukulia utani ila nikaanza kuhisi labda anamaanisha ila anashindwa kusema siliasi.

Kingine kuna rafiki yake pale kazini aliwahi kumtuma aje aniambie kuwa ananitaka ila huyo rafiki ake utani mwingi so alinambia kiutani utani. Sasa sijui alikuwa siliasi kumtuma huyo rafiki yake au la?

Basi nikaanza mchakato wa kumfukuzia ili nimpate, shida ikaanzia hapo, nikimwita niongee nae faragha anakataa anasema 'njoo wewe' wakati anajua kuwa anapokaa yeye pale kazini wanakaa kibao so siwezi kuongea nae faragha. Nikimwita wakati wa kutoka anasema nna haraka nataka niondoke. Nikaona isiwe tabu ngoja nimuombe namba ili weekend niombe appointment sasa ikawa kila nikiomba appointment anakataa mara 'oooh nna kazi nyingi' basi jumamosi flani nikaamua nimpigie simu nimtongoze, nikamtongoza anakanambia namtania then simu akakata simu. Kesho jumapili nikampigia simu hakupokea nikamtumia sms hakujibu nikampigia tena mara kibao hakupokea. Nikaamua nimpotezee, Jumatatu anafika, akaanza tena shobo zake 'Joeeel, nimekumisi' nikamlia bati(nikamchunia).

Nilipoona anashobo sana na nimekula bati nikahisi labda anataka ila hataki kutongozwa kwenye simu, nikaaza kumwita tena faragha akawa anazingua. Akazingua hivyovyo mpaka umefika mda wa field kuisha akaondoka.

Sasa baada ya kuondoka nilimpigia simu akapokea mara moja tu ila akanambia hatuwezi kuongea yuko bize nikamwambia ntakupigia kesho. Kesho imefika hapokei simu wala hajibu sms mpaka leo hii.

Kiukweli ni mzuri sana tu, halafu mweupeee, chotara flani hivi la kiarabu, hiyo shepu ndo usiseme kwahiyo na mi nampenda. Ila sasa mpaka sa hivi hapokei simu wala hajibu text sasa wakuu hebu nishaurini nifanye nini ili apokee simu yangu maana mie nshaoza kwake Dah!

Natamani apokee simu niongee nae nimuombe date ila ndo hivyo hapokei, text ndo hajibu kabisaaa nimetuma karibia kumi. Sasa mie sitaki kumwacha naombeni mnishauri cha kufanya ili nimpate.

Ananiumiza sana kichwa aiseee, leo kutwa nzima namuwaza yeye.

Mnisamehe kama nimewakwaza kwa kuandika maneno mengi.

Nashkuru kwa ambao mtanishauri vizuri bila kunitukana au kunidhihaki.
Wewe ulishasema una pepo la kukataliwa, mkuu rudi kwenye mode yako ya kukaa bila wasichana utapata amani, sasa mtu hajibu wala kupokea simu zako bado unamuwaza na kumuulizia, in short unamkwaza na hakutaki kbsa
 
Ulishindwa kumpata upo nae hapo, sahivi huko mbali hapokei simu wala msg utampata vipi, lazimisha moyo umsahau...futa namba, futa msg zake na kila kumbukumbu yake japo hautamsahau haraka ila utamsahau tu...
Ila Jo ulishindwa hata kumtoa out?
Niliwahi kumuomba tutoke akakataa.

Ila ntajitahidi nimsahau asee!
 
atakuwa anapenda drama za mapenzi ya kukimbizana kama wahindi, kwahiyo kama huwezi drama jiandae kuumia zaidi ila kama na wewe ni mzuri kwenye drama basi waweza endelea.
Mwanamke mwenye drama anazingua sana yaani. Sababu unakuta uko serious yeye anaruka ruka. Hao huwa wabafanya mtu kuchoka au kukinai penzi haraka
 
Ningekuwa me ndio wewe kwenye hizo ningekuwa kauzu hatari yani ningemu ignore akiwa curious enough, ningeita sehemu nile bila kutongoza.
 
Sijaona mahali Joel katoa hata ofa ya lunch mzee baba mkono mtupu haulambwi😀😀

Ila pia possible Joel ana tuvitu flani tunakata stimu, may be hana maneno ya kuvutia, may be hajui kutumia chance make hapo ofisini alivoambiwa I miss you alitakiwa aoneshe uwepo wake sasa ye anaanza kusubiri weekend broo zege hailali ikilala inakua sakafu.

Lastly ampotezee huyo nae hayupo tayari kutmbw asimfanye Joel jogoo anataka kukimbiiiizwa!!!
Madam umeua😂😂...mi pamoja na ubahili wangu bado sijamfikia joel😂😂😂😂😂😂...jamaa kashindwa kutoa hata ofa ya lunch kipindi chote mtoto amekuja field ofisini
 
Hakupendi huyo achana naye.. wako yupo atakuja tu ondoa shaka.. piga kazi ndugu....
NB: sumu ya mwanamke ni pesa ndo maana nakushaur piga kaxi watakuja wenyeweee bila kuwatongoza..
Nawakilisha kungwi mtoto.
 
Ungemwambia Face to Face nakupitia Tutoke out wewe ulikuwa unakosea kumtongoza kupitia Simuu...na alijua unamuogopa ndo maana yeye akawaa Ana confidence ya kukutania face to face Ila wewe unampotezea then kwenye simu unaanza kumlilia shida zakoo...!! Ungejiongezaa direct mkuu hata kwa kumletea vizawadi kumtoa Lunch hivi.... Ilaa hapoo kashasepaa ukijichanganya Utapigwaaa Vizingaa tuu
 
Wewe bado hujajua kutongoza,Mwanamke akikushobokea usinyeshe uoga wala kiherehere unambadilishia staili halafu mbele za watu.Yaani unamkwida kikweli kweli.

Sasa kwanza usimtongoze kwenye simu mwanamke ambaye anakushobokea mbele za watu.Unachokifanya unamwambia straight ila kimya kimya kwamba 'Dada najua unapenda mzaha na mimi ila ukinifanyia hivi mbili za watu unanikosesha amani kabisa"
 
Habari za saa hizi wana jukwaa.

Kwanza nikiri kabisa, nimekuwa single kwa mda mrefu na hii ni kutokana na kukataliwa na waschana wengi niliokuwa nikiwatongoza. Baada ya hapo nikaamua kupotezea mchongo wa mahusiano so sikutaka kujihusisha kimahusiano na msichana yeyote.

Sasa juzi hapa kazini kwetu alikuja msichana fulani kufanya field ambapo wakati anaanza field mie nilikuwa likizo hivyo nilikuja kurudi kazini nikakuta kashakuwa mwenyeji na kashazoeana na watu hapa kazini.

Mara ya kwanza hatukuzoeana sana nae, hivyo zaidi ya salamu tulikuwa hatuzungumzi kitu ila ni mtu fulani muongeaji sana (yaani sana) kwahiyo alikuwa ananiongelesha mambo madogo madogo kama 'Joel mida ya kuondoka imefika, vipi bado upo?' sasa katika kuzungumza mambo madogo kama hayo akawa ameanza kunizoea hivyo akaanza kuniletea utani wa hapa na pale.

Sasa kuna kipindi pale kazini kulikuwa na tukio maalumu kwahiyo wafanyakazi walikuwa wanakuja wachache tena vijana tu, wale wengine walikuwa wanaenda huko kwenye hilo tukio. Kwa nafasi hiyo ya watu kuwa wachache akawa ananiletea utani flani hivi ambao ulianza kunistua na kuamsha hisia zangu.

Alikuwa ananiita na kuanza 'Joel, daah nimekumiss sana' akinambia hivo namchunia mara 'Joel, kwani mi huwezi kunioa? Nna kasoro gani?' au wakati mwingine anasema: 'Joel, I love you' au anaweza sema 'Joel, nakosa usingizi kwa ajili yako', sasa mie nilikuwa nachukulia utani ila nikaanza kuhisi labda anamaanisha ila anashindwa kusema siliasi.

Kingine kuna rafiki yake pale kazini aliwahi kumtuma aje aniambie kuwa ananitaka ila huyo rafiki ake utani mwingi so alinambia kiutani utani. Sasa sijui alikuwa siliasi kumtuma huyo rafiki yake au la?

Basi nikaanza mchakato wa kumfukuzia ili nimpate, shida ikaanzia hapo, nikimwita niongee nae faragha anakataa anasema 'njoo wewe' wakati anajua kuwa anapokaa yeye pale kazini wanakaa kibao so siwezi kuongea nae faragha. Nikimwita wakati wa kutoka anasema nna haraka nataka niondoke. Nikaona isiwe tabu ngoja nimuombe namba ili weekend niombe appointment sasa ikawa kila nikiomba appointment anakataa mara 'oooh nna kazi nyingi' basi jumamosi flani nikaamua nimpigie simu nimtongoze, nikamtongoza anakanambia namtania then simu akakata simu. Kesho jumapili nikampigia simu hakupokea nikamtumia sms hakujibu nikampigia tena mara kibao hakupokea. Nikaamua nimpotezee, Jumatatu anafika, akaanza tena shobo zake 'Joeeel, nimekumisi' nikamlia bati(nikamchunia).

Nilipoona anashobo sana na nimekula bati nikahisi labda anataka ila hataki kutongozwa kwenye simu, nikaaza kumwita tena faragha akawa anazingua. Akazingua hivyovyo mpaka umefika mda wa field kuisha akaondoka.

Sasa baada ya kuondoka nilimpigia simu akapokea mara moja tu ila akanambia hatuwezi kuongea yuko bize nikamwambia ntakupigia kesho. Kesho imefika hapokei simu wala hajibu sms mpaka leo hii.

Kiukweli ni mzuri sana tu, halafu mweupeee, chotara flani hivi la kiarabu, hiyo shepu ndo usiseme kwahiyo na mi nampenda. Ila sasa mpaka sa hivi hapokei simu wala hajibu text sasa wakuu hebu nishaurini nifanye nini ili apokee simu yangu maana mie nshaoza kwake Dah!

Natamani apokee simu niongee nae nimuombe date ila ndo hivyo hapokei, text ndo hajibu kabisaaa nimetuma karibia kumi. Sasa mie sitaki kumwacha naombeni mnishauri cha kufanya ili nimpate.

Ananiumiza sana kichwa aiseee, leo kutwa nzima namuwaza yeye.

Mnisamehe kama nimewakwaza kwa kuandika maneno mengi.

Nashkuru kwa ambao mtanishauri vizuri bila kunitukana au kunidhihaki.
Achana naye, fanya mambo mengine.
a)[Parallel Running] Inawezekana alikuwa anakutaka ila as a second choice baada ya kupata shida kumnasa first choice. Ss na wewe ulipochelewa, ikatokea sasa first choice kakaa sawa....(You know where I am going with this)

b)[Winner Wannabe] Labda wakati huingiliki alikuchukulia as a challenge. Labda hapo kazini wanaume wote wameshamsumbua. We Joel ni nani labda? Iweje toka ufike kazini hujaenda kureport kwake? Basi akapambana akapata title yake kwa wewe hatimaye kushoboka then akawa satisfied.

c)[Not that Hot after all] Labda ulivyokua cool ulimvutia. Alivyokusumbua mkazoeana akaona huko vile alivyotegemea

I can go on and on with a bunch of other theories but, u get my point. Walk away! Kapambane na wanawake walio serious. Mbona wako wengi? Huyo hata akikukubalia kutakuwa na drama sana kwenye uhusiano. Mapema hiyo hajali feelings zako ndo atakuja kujali bdae? Achana na vitoto nenda tafuta matured woman. Wako wengi tena unawachelewesha!
 
Wewe ungekula bati tu kujishobokesha kumekunyima point
 
Japo huyo dem nae alikua anarukaruka ila Jo kuna makosa ya kiufundi kafanya
Jamaa inaonekana sio janja kabisa,huyo mtoto inaonekana kashindwa kumkula kwa uzembe wake...kama kamshindwa huyo aliyekuwa anamwambia anakosa usingizi sababu yake sjui ataweza mkulanani mwingine😂
 
Back
Top Bottom