Jamani kitaa ni kigumu sana, ukikutana na watu wa namna hii usiache kutoa msaada

Jamani kitaa ni kigumu sana, ukikutana na watu wa namna hii usiache kutoa msaada

VIONGOZI WA KISIASA NA SERIKALI wanaweza kuja na mipango mikakati ya kusaidia ajira zisizo rasmi.
Kama aliyekuja na wazo la kuruhusu 1.BODA BODA NA BAJAJI alisaidia kutengeneza ajira zisizo rasmi kwa vijana ,wengi wanaendesha maisha yao kupitia boda boda na bajaji.

2.Aliyejenga chuo kikuu cha UDOM alikuja na wazo zuri ,mana hawa vijana bila vyuo vingi vya kati na vikuu kuongezwa watasoma wapi na idadi ya wasomi inazidi kuongezeka,japo bado kinahitajika MASOMO YA UJUZI ,VYUO VINGI VYA UFUNDI NA UJUZI wanafunzi wakimaliza shule ya msingi na sekondari wahitumu wakiwa na UJUZI WA UFUNDI utakaowawezesha kujiajiri hata wasipoendelea na VYUO VIKUU .Mfano elimu ya sekondari si form four ni ya lazima ,mtu akimaliza FORM FOUR katika MTAALA WA MASOMO YA FORM FOUR OLEVEL ajifunza na masomo ya ufundi ujuzi ,amalize akiwa na ujuzi fulani au ufundi fulani.

3)SERIKALI IFUFUE VIWANDA na ijenge viwanda kila wilaya au kadiri ya malighafi zinazopatikana katika hiyo wilaya.Kuwe na mashamba makubwa ya serikali kila wilaya,miradi ya uvuvi,madini,viwanda vya simenti,ufugaji,n.k ya serikali kila wilaya na vijana waajiriwe katika viwanda vya serikali vitakavyojengwa kila wilaya.Bidhaa zitakazozalishwa na viwanda vya serikali ziuzwe nje ya nchi au nchini kwa bei sawa na bidhaa za viwanda vya watu binafsi.KILA WIZARA IJE NA WAZO la kubuni miradi mkubwa utakaotoa ajira kwa vijana na kuipa faida wizara serikali.ITATATUA CHANGAMOTO ya ajira kwa vijana na kukuza uchumi wa taifa.
 
Asante sana ubalikiwe

Lakini sasa mtumish Kuna sadaka za aina mbili

Yaan aina za sadaka ni mbili

1. Kwa makuhani, yaan kanisani
2. Kwa wahitaji, yaan masikin, hospital wagonjwa wafungwa na omba omba

Kwahiyo jitaid utoe kote kote mtumish

Yote kwa yote nakusapot sana

MUNGU MWENYEZI AKUBARIKI SANA
Namba 2 ndio sadaka bora ya muda wote
 
Mkuu mi nimeshakuwa kiongozi kanisani kwa awamu tofauti tofauti hivyo hadi nafikia kuacha na kukataa uongozi najua ninacho kifanya 100%.

Waumini wanaweza toa hela kwa umoja na upendo lakini itakayo nunuliwa vitu vya kupeleka kwa hitaji ni robo tu nyingine inapigwa juu kwa juu.

Yaani kama mmechanga 2000 basi wahitaji itawafikia 500 tu. Nimeshaambiwa mimi ni muasi na wameshasubri nipate tatizo wasilete huduma kwangu. Najua nachofanya na kila ninapo toa kwa wahusika huwa wanafurahi mno mbele yangu.

Huu hapa mfano mmoja tu

Niliwahi mpelekea maam mjane mmoja vitu kadhaa wa kadhaa pamoja na nguo nadhani wanaita JAVA kama sio wax Zilikuwa pair 3 kama sijasahau na nilinunua 35k kila pea

Baada ya kumpa yule mama alilia machozi mbele yangu akaniambia nichukue jogoo la kuku nikakataa sasa kipindi nampa alipiga yowee mama jirani akaja ndo akaniambia chukua huyo kuku.......nikachukua.

Kesho yake yule mama alienda kuwashukuru wazazi wangu ukumbuke ni wakijij jirani wala wazazi hawakujua nilichokifanya ndo wakaniambia nilijisikia furaha mno nilipopata taarifa kutoka kwa wazazi.

Yule mama wakati wa mavuno huwa anapeleka nyumbani karanga,mahindi au mpunga halafu wazazi wanani taarifu nafuata. Huwa ansema huyu ni mwanangu kabisa hata akipata wageni waheshima ataenda home kumfuata baba akale kuku pale.
Hii comment imejaa pride hatari, itoshe kusema kwamba unakiburi na unapenda kujiinua.
 
Ukikutana na watu wa namna hii basi fanya kununua kitu
View attachment 3218915

Hata ukiwa hauna njaa fanya kuwa sehemu ya furaha kwao. Kitaa ni kigumu sana wanandugu.
View attachment 3218916
Miezi ya mwisho wa mwaka nilikuwa sehemu semina
Kuna mother anauza vitafunwa/vitumbua
Mama mtu mzima umri wa mama yangu.
Day one 2,3 nikapita namsalimia. Day 4 roho ikanituma nitoe chochote kununua.
Nikatoa buku nikamwambia nitapita kuchukua baadaye.. kiukweli si mpenzi wa vitumbua.
Nilinunua kumsapoti tu, isitoshe nilikokuwa naenda kulikuwa na chakula kuanzia asbh hadi muda tunaondoka tumeshiba ndiii.

Nafsi ikawa inanisuta kwamba mbona umempa kidogo?
Umepewa Bure toa Bure...
Kiukweli I did nothing ni neema ya Bwana kupata zile pesa.

Kesho yake nilipita tena nikatoa hela yote niliyopata jana yake, nikampa yule mama. .haikuwa kubwa sana ila ndipo uwezo wangu ulipoishia.
Mama akiweka kila kitu chini akanyoosha mikono kunikumbatia.
Nikachuchumaa kumkumbatia pia kama dakika 2 amenikumbatia yule mama.

Alitamka maneno ya Dua za Baraka
Sikuyaelewa maana sijui kiarabu ila nadhani ni Aya za kwenye Quran.

Nikamwambia ukweli kwamba sitaweza kuchukua vitumbua maana tunakokwenda wanatuandalia chakula kuanzia muda tunaingia hadi tunatoka.

Alinibariki
Niliondoka nikiwa na amani na furaha sana.

.........
Jiwekeeni hazina Mbinguni ambapo hakuna wezi Wala kutu.
 
Huwa nafanya hivyo kuna siku nilikutana na mawakala wanaotembea kwa mguu wanasijiri laini wamechoka na wana njaa hallafu hawana hela.

Nilikuwa na pikipiki wakaniomba lift wakasema hawana wana buku yaani wamesajiri laini moja toka asbuhi hadi saa9 nikawaambia bila buku2 sibebi wakasema haya .... Yote ilikuwa zuga tu kuona kama kweli hawana hela nikawasha niende mara yule wa kike akasema ni mbebe yeye kwa buku1 maana hata nguvu hana amechoka sana nikaichukua ile buku nikamuita na jamaa nikawabeba.

Niliwauliza maswali kadhaa wa kadhaa then tukafika kwa mama ntilie nikawashusha nikawaambie waagize msosi wa nguvu wale washibe walitumia kama buku6 wote nikawaacha wanakula nikawapa na buku10 wagawane 5-5 na ile buku yao.
Faza mi pia nasajiri laini..
Show yake kali yaani hawa voda hawa jamni acha tuu
 
Nilishawahi kulinganisha Kati ya sadaka ya kanisani na sadaka ya kuwapa wahitaji ni sadaka ipi inayoleta majibu ya haraka na hata unapata amani moyoni mwangu!.
Aisee majibu niliyoyapata ni kuwa sadaka ya kutoa Kwa kuhitaji Ina nguvu zaidi.
Huo ni ukweli mimi mwenyewe sipingi mtumish

Lakin na wa kanisan wakumbuke
 
Miezi ya mwisho wa mwaka nilikuwa sehemu semina
Kuna mother anauza vitafunwa/vitumbua
Mama mtu mzima umri wa mama yangu.
Day one 2,3 nikapita namsalimia. Day 4 roho ikanituma nitoe chochote kununua.
Nikatoa buku nikamwambia nitapita kuchukua baadaye.. kiukweli si mpenzi wa vitumbua.
Nilinunua kumsapoti tu, isitoshe nilikokuwa naenda kulikuwa na chakula kuanzia asbh hadi muda tunaondoka tumeshiba ndiii.

Nafsi ikawa inanisuta kwamba mbona umempa kidogo?
Umepewa Bure toa Bure...
Kiukweli I did nothing ni neema ya bwana kupata zile pesa.

Kesho yake nilipita tena nikatoa hela yote niliyopata jana yake, nikampa yule mama. .haikuwa kubwa sana ila ndipo uwezo wangu ulipoishia.
Mama akiweka kila kitu chini akanyoosha mikono kunikumbatia.
Nikachuchumaa kumkumbatia pia kama dakika 2 amenikumbatia yule mama.

Alitamka maneno ya Dua za Baraka
Sikuyaelewa maana sijui kiarabu ila nadhani ni Aya za kwenye Quran.

Nikamwambia ukweli kwamba sitaweza kuchukua vitumbua maana tunakokwenda wanatuandalia chakula kuanzia muda tunaingia hadi tunatoka.

Alinibariki
Niliondoka nikiwa na amani na furaha sana.

.........
Jiwekeeni hazina Mbinguni ambapo hakuna wezi Wala kutu.
Ubalikiwe sana mtumish sadaka kwa masikin

1 , hutakasa dhambi

2, hufungua vifungo
 
VIONGOZI WA KISIASA NA SERIKALI wanaweza kuja na mipango mikakati ya kusaidia ajira zisizo rasmi.
Kama aliyekuja na wazo la kuruhusu 1.BODA BODA NA BAJAJI alisaidia kutengeneza ajira zisizo rasmi kwa vijana ,wengi wanaendesha maisha yao kupitia boda boda na bajaji.

2.Aliyejenga chuo kikuu cha UDOM alikuja na wazo zuri ,mana hawa vijana bila vyuo vingi vya kati na vikuu kuongezwa watasoma wapi na idadi ya wasomi inazidi kuongezeka,japo bado kinahitajika MASOMO YA UJUZI ,VYUO VINGI VYA UFUNDI NA UJUZI wanafunzi wakimaliza shule ya msingi na sekondari wahitumu wakiwa na UJUZI WA UFUNDI utakaowawezesha kujiajiri hata wasipoendelea na VYUO VIKUU .Mfano elimu ya sekondari si form four ni ya lazima ,mtu akimaliza FORM FOUR katika MTAALA WA MASOMO YA FORM FOUR OLEVEL ajifunza na masomo ya ufundi ujuzi ,amalize akiwa na ujuzi fulani au ufundi fulani.

3)SERIKALI IFUFUE VIWANDA na ijenge viwanda kila wilaya au kadiri ya malighafi zinazopatikana katika hiyo wilaya.Kuwe na mashamba makubwa ya serikali kila wilaya,miradi ya uvuvi,madini,viwanda vya simenti,ufugaji,n.k ya serikali kila wilaya na vijana waajiriwe katika viwanda vya serikali vitakavyojengwa kila wilaya.Bidhaa zitakazozalishwa na viwanda vya serikali ziuzwe nje ya nchi au nchini kwa bei sawa na bidhaa za viwanda vya watu binafsi.KILA WIZARA IJE NA WAZO la kubuni miradi mkubwa utakaotoa ajira kwa vijana na kuipa faida wizara serikali.ITATATUA CHANGAMOTO ya ajira kwa vijana na kukuza uchumi wa taifa.
Unapoteza mda wako tu kuishauri serikali ya mama Samia iliyojaa mafisadi na wala rushwa

Mkuu mwenyewe wa nchi haoni aibu kuuza nchi yake mwenyewe
 
Back
Top Bottom