Miezi ya mwisho wa mwaka nilikuwa sehemu semina
Kuna mother anauza vitafunwa/vitumbua
Mama mtu mzima umri wa mama yangu.
Day one 2,3 nikapita namsalimia. Day 4 roho ikanituma nitoe chochote kununua.
Nikatoa buku nikamwambia nitapita kuchukua baadaye.. kiukweli si mpenzi wa vitumbua.
Nilinunua kumsapoti tu, isitoshe nilikokuwa naenda kulikuwa na chakula kuanzia asbh hadi muda tunaondoka tumeshiba ndiii.
Nafsi ikawa inanisuta kwamba mbona umempa kidogo?
Umepewa Bure toa Bure...
Kiukweli I did nothing ni neema ya Bwana kupata zile pesa.
Kesho yake nilipita tena nikatoa hela yote niliyopata jana yake, nikampa yule mama. .haikuwa kubwa sana ila ndipo uwezo wangu ulipoishia.
Mama akiweka kila kitu chini akanyoosha mikono kunikumbatia.
Nikachuchumaa kumkumbatia pia kama dakika 2 amenikumbatia yule mama.
Alitamka maneno ya Dua za Baraka
Sikuyaelewa maana sijui kiarabu ila nadhani ni Aya za kwenye Quran.
Nikamwambia ukweli kwamba sitaweza kuchukua vitumbua maana tunakokwenda wanatuandalia chakula kuanzia muda tunaingia hadi tunatoka.
Alinibariki
Niliondoka nikiwa na amani na furaha sana.
.........
Jiwekeeni hazina Mbinguni ambapo hakuna wezi Wala kutu.