Jamani kitaa ni kigumu sana, ukikutana na watu wa namna hii usiache kutoa msaada

VIONGOZI WA KISIASA NA SERIKALI wanaweza kuja na mipango mikakati ya kusaidia ajira zisizo rasmi.
Kama aliyekuja na wazo la kuruhusu 1.BODA BODA NA BAJAJI alisaidia kutengeneza ajira zisizo rasmi kwa vijana ,wengi wanaendesha maisha yao kupitia boda boda na bajaji.

2.Aliyejenga chuo kikuu cha UDOM alikuja na wazo zuri ,mana hawa vijana bila vyuo vingi vya kati na vikuu kuongezwa watasoma wapi na idadi ya wasomi inazidi kuongezeka,japo bado kinahitajika MASOMO YA UJUZI ,VYUO VINGI VYA UFUNDI NA UJUZI wanafunzi wakimaliza shule ya msingi na sekondari wahitumu wakiwa na UJUZI WA UFUNDI utakaowawezesha kujiajiri hata wasipoendelea na VYUO VIKUU .Mfano elimu ya sekondari si form four ni ya lazima ,mtu akimaliza FORM FOUR katika MTAALA WA MASOMO YA FORM FOUR OLEVEL ajifunza na masomo ya ufundi ujuzi ,amalize akiwa na ujuzi fulani au ufundi fulani.

3)SERIKALI IFUFUE VIWANDA na ijenge viwanda kila wilaya au kadiri ya malighafi zinazopatikana katika hiyo wilaya.Kuwe na mashamba makubwa ya serikali kila wilaya,miradi ya uvuvi,madini,viwanda vya simenti,ufugaji,n.k ya serikali kila wilaya na vijana waajiriwe katika viwanda vya serikali vitakavyojengwa kila wilaya.Bidhaa zitakazozalishwa na viwanda vya serikali ziuzwe nje ya nchi au nchini kwa bei sawa na bidhaa za viwanda vya watu binafsi.KILA WIZARA IJE NA WAZO la kubuni miradi mkubwa utakaotoa ajira kwa vijana na kuipa faida wizara serikali.ITATATUA CHANGAMOTO ya ajira kwa vijana na kukuza uchumi wa taifa.
 
Namba 2 ndio sadaka bora ya muda wote
 
Hii comment imejaa pride hatari, itoshe kusema kwamba unakiburi na unapenda kujiinua.
 
Ukikutana na watu wa namna hii basi fanya kununua kitu
View attachment 3218915

Hata ukiwa hauna njaa fanya kuwa sehemu ya furaha kwao. Kitaa ni kigumu sana wanandugu.
View attachment 3218916
Miezi ya mwisho wa mwaka nilikuwa sehemu semina
Kuna mother anauza vitafunwa/vitumbua
Mama mtu mzima umri wa mama yangu.
Day one 2,3 nikapita namsalimia. Day 4 roho ikanituma nitoe chochote kununua.
Nikatoa buku nikamwambia nitapita kuchukua baadaye.. kiukweli si mpenzi wa vitumbua.
Nilinunua kumsapoti tu, isitoshe nilikokuwa naenda kulikuwa na chakula kuanzia asbh hadi muda tunaondoka tumeshiba ndiii.

Nafsi ikawa inanisuta kwamba mbona umempa kidogo?
Umepewa Bure toa Bure...
Kiukweli I did nothing ni neema ya Bwana kupata zile pesa.

Kesho yake nilipita tena nikatoa hela yote niliyopata jana yake, nikampa yule mama. .haikuwa kubwa sana ila ndipo uwezo wangu ulipoishia.
Mama akiweka kila kitu chini akanyoosha mikono kunikumbatia.
Nikachuchumaa kumkumbatia pia kama dakika 2 amenikumbatia yule mama.

Alitamka maneno ya Dua za Baraka
Sikuyaelewa maana sijui kiarabu ila nadhani ni Aya za kwenye Quran.

Nikamwambia ukweli kwamba sitaweza kuchukua vitumbua maana tunakokwenda wanatuandalia chakula kuanzia muda tunaingia hadi tunatoka.

Alinibariki
Niliondoka nikiwa na amani na furaha sana.

.........
Jiwekeeni hazina Mbinguni ambapo hakuna wezi Wala kutu.
 
Faza mi pia nasajiri laini..
Show yake kali yaani hawa voda hawa jamni acha tuu
 
Nilishawahi kulinganisha Kati ya sadaka ya kanisani na sadaka ya kuwapa wahitaji ni sadaka ipi inayoleta majibu ya haraka na hata unapata amani moyoni mwangu!.
Aisee majibu niliyoyapata ni kuwa sadaka ya kutoa Kwa kuhitaji Ina nguvu zaidi.
Huo ni ukweli mimi mwenyewe sipingi mtumish

Lakin na wa kanisan wakumbuke
 
Ubalikiwe sana mtumish sadaka kwa masikin

1 , hutakasa dhambi

2, hufungua vifungo
 
Unapoteza mda wako tu kuishauri serikali ya mama Samia iliyojaa mafisadi na wala rushwa

Mkuu mwenyewe wa nchi haoni aibu kuuza nchi yake mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…