Jamani natafuta kazi ya UPISHI Nimechoka kukaa nyumbani

Jamani natafuta kazi ya UPISHI Nimechoka kukaa nyumbani

Jamani hali ngumu,

Mwenye uhitaji wa Mpishi wa kupika vyakula mbalimbali hebu tupeane connection.

Nimesoma Hotel Management pale DDC Kariakoo na kufanya kazi sehemu mbalimbali.

Nyumbani kunachosha sana. Mnataka tufe na njaa au?

Niko Dodoma mjini.

Hata kama wataka kupikiwa nyumbani kwako niko tayari.

Karibuni PM

Mnaosema kuhusu zile Milioni 50, Nilikuwa namuombea ushauri mtu wala hazikuwa pesa zangu zile.
Maana naona mnaanza🤭
Wewe ungesema unatafuta wakumpikia jumla hapo ningekwelewa bado inahangaika na kazi tafuta wa ukweli wa kukuweka ndani hutachoka kabisaaaa
 
Nyumbani kunachosha sana
Kweli mkuu nyumbani panachosha hasa pale unapokuwa ni jobless unanyanyaswa, kwa nini ufadhaike,

mimi kama mwanachama wa majobless na msajili wa chama napenda kukwambia sisi tutakuwa familia yako mpya , sisi tutakuwa nyumba kwako.
Kama hutojali Naomba nikukaribishe kwenye chama cha majobless pro max
kikiongozwa na Mh. Rais wa majobless pro max Intelligent businessman na makamu wake Bolotoba katibu ni min -me
waziri wa mambo ya ndani ni Thecoder msajili wa chama ni dosho12 wakiki ni Selikavu mratibu wa mipango ni Edo kissy

na bila kumsahau semaji la cham makutupora , hadhi yako, haki yako, heshima yako italindwa,

pia tutakupa muongozo wa kutumia hela vizuri haiwezekani mil 50 ndani ya wiki imeisha😅😅😅.

Kidumu chama cha majobless pro max
 
Naweza nikafungua mama ntilie usimamie ama utanikimbia Mana nakufungulia wewe baadaye itakuwa unanilipa wewe , yaani Kila kitu nakupa labda nakuambia uwe unanipa let say 10k per day, unajua kupika Yale mapishi ya kitanga, naweza nitakufungulia baadaye ukanikimbia huku bado hela ya gu haijarudi. Inatakiwa uje uwe unawapikia wasukuma mpaka wanajilamba kidole kwa utamu. Sijajua Kama uko committed kiasi gani, Mana binadamu anabadilika fasta mno, yaani tokea nijue ubongo wa binadamu namuogopa kiumbe binadamu Ila pia ni mzuri,
Mie sintokuwa nakusimamia ujisimamie mwenyewe, yaani nalipia fremu,vyombo na chakula nanunua baadaye Sasa ndio unakuja utundu wako wa kuwavutia wateja wako, sijajua Kama unalo umbo na sura ambayo mteja anakula chakula anafurahi ama akikuona tu chakula kinashuka na anafurahi
 
Sawa, naweza kujisimamia mwenyewe pia kwa maana nilishawahi kuwa na ka-mgahawa ila Manispaa ikaja kuuvunja hivyo nikakosa sehemu ingine.
Amini nakwambia mimi ni mpishi hodari na wala hutojutia ukinipa hiyo nafasi
 
Unaweza ukafanya kazi miaka mingapi ndio ukaniacha Mana bana binadamu anabadilika mno ndio mana anahitaji katiba, zile amri za Mungu , yaani unaweza ukapata dili la kulipwa milioni hotel ya kitalii ukaniacha hapa na sijarudisha hela yangu.
Mie napanga fremu kabisa
 
Back
Top Bottom