Jamani tusemeni tu ukweli, Mange Kimambi is a Tanzanian hero

Jamani tusemeni tu ukweli, Mange Kimambi is a Tanzanian hero

Info nyingi anazopewa huwa haziko sawa ila kwa kua ameshaaminika basi watu wanaamini kua ni za kweli lakini nyingi wanamuingiza chaka!! Na kwa mwenye akili nzuri na timamu sio wa kumsapoti Mange maana amekua akitukana hata wenye kumzidi umri tena matusi ya nguoni kabisa.Ningemsapoti sana kama angelikua anatumia lugha nzuri kuwasilisha hoja zake lakini kwa lugha anazotumia ninaamini sio mtu wa kujiheshimu na ana chuki binafsi.Na atabaki tu kupost kwenye mitandao na hakuna kitu kitakachofanyika na watu mtamaliza MB zenu bure jamani.Haya ni maoni yangu na ndo ninachoamini.
 
Hivi aliyewataja hadharani mapapa wauza unga sio shujaa na jasiri??? Hii ipo tz tu![emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ao mapapa wauza unga waliotajwa wapo wapi sasa hivi? Je wamefungwa? Wameacha kuuza unga?
 
Tz haiwezi ikawa na hero mtukanaji kama yule
Hivi wewe unataka kusema mtukanaji ni Mange peke yake mpaka unalifanya kuwa jina lake? Wangapi humu wanatukana? Hivi kuwaambia watu wafyatue watoto siyo matusi? Sikubaliani na matusi lakini asilaumiwe mmoja wakati watu wengi licha ya kusema matusi kama mange lakini wanayaonyesha matusi na kuyafanya matusi kila uchao!
 
Seriously??????
Leo kasema dada zari anamtoto kesho kasema diamond na zari inabidi waachane, matusi kibao yaan ndo lugha yake af unasema hero
Huyu ni mtu wa kiki na matukio, followers zake wakimwambia ki2 ye anawasirisha iwe uongo au ukweli

Mtu nikimsikia2 ananambia data katoa kwa mange namzarau
 
Hivi wale wanaojua ngeli neno hero linatumika kwa ke?
 
mange tyako tuuu yule hana lolote

unadhani kuwa watu hawana habari wanazo sana ndo wanao mpa uyo mange wako

tatizo ni sheria mbovu wee iseme tuu kama uwendi kunyia debe
Sasa kwa nini hizo habari wasikupe wewe? Jibu ni rahisi tu kuwa huna ubavu wa kuzianika! Kwa hiyo anapelekewa shujaa anayeimudu kazi!
Wala usiseme ni kwa kuwa yuko nje ya nchi kwani aliye nje ya nchi ni Mange peke yake?
 
Hotel yaoTriz inapigwa mnada na Lukuvi..ati wanadaiwa kodi ya ardhi....wenyewe wanasema wamelipa...visasiii
 
hebu nikuulize imekuwaje tangu jana mange kafuta clip zote za makonda kafunga nahiyo account? kama ulijifanya kiherehere za kukoment mambo ya kijinga your gone myfriend! anza kabisa kuandaa watu wa kukudhamini.
Kwani wewe hufutagi SMS kwenye Simu yako? Ujumbe ukitimiza majukumu yake hakuna sababu ya kuubakisha!
 
Hahahah, watu wameweka kambi kwenye akaunti yake si mchezo wanasubiri ubuyu wa moto
 
Hahahah, watu wameweka kambi kwenye akaunti yake si mchezo wanasubiri ubuyu wa moto
dfa6271a1587d0cca591d30f4a85df6f.jpg


1k unred messages in a matter of hours when she just took a nap. Alafu asiwe hero
 
Hivi wale wanaojua ngeli neno hero linatumika kwa ke?
Mkuu sio kila mtu anajua ngeli humu. Ili wengi waweze kuelewa ndyo maana tuneacha ivyo. Ucdhani ni wewe mwenyewe ndye wajua.
 
Leo nilkuwa sehem nakunywa khwa. Bwana mmoja alisema neno limenifikirisha sana. Huyo bwana aliropoka kuwa "kuliko kufa Mange kimambi ni bora wafe wanaume wa dar milion moja" Tuliangua vicheko vya kutosha ila baadye niliwaza sana hya maneno.

770267396df5dc6a2e855babd967a128.jpg


Yani kufa Mange Kimambi ni bora wafe watu million moja. Hii imenipa tafsiri kuwa mange kimambi kwa sasa anaplay part kubwa sana kama wistle blower hapa Tanzania.

Mange kimambe amekuwa kama chanzo kikubwa sana ya kuvujisha mambo ambayo yanatokea nyuma ya pazia ya serkali yetu.

Ujasiri wa huyu dada sio wa kawaida. MANGE KIMAMBI ANAUJASIRI WA KISHUJAA.

Sasa Amekuwa si mtu wa kupuuzwa kama ilivyokuwa apo zamani. Ametusaidia watanzania wengi (Tunaojielewa) kuconnect dots. Wengi tumefunguka macho na masikio yetu. Tumegundua kuwa serkali ilikuwa unatusikilizisha na kutuonesha matango pori.

Nakupa big up Dada Mange. Tupo kwenye hya mapambano pamoja. Keep it up. You are the Hero.

Wapo ambao hamta nielewa ila ipo siku mtaelewa.

Clauds walimchamba sana Mange, ila leo wanaona umuhimu wake.
Akianza kumtukana Manywele muendelee kumsifia hivohivo
 
Jamani ku deal na serikali sio kitu rahisi kumbuka serikali wana uwezo wa kukuzimisha hata huko ulipo
Yani huyo dada ni kama kajitoa kafala maana serikali yoyte ulimwenguni ikiamua kuku ua haishindwi
Sasa kuua watu ni sifa? Ni Nani ambaye hatakufa?
Sitetei matusi lakini natetea ujasiri wa kuanika nuruni mambo yaliyofanyika gizani!
Mambo kama aliyofanya Bashite pale clouds kuna watu hata hayo wanasema "ni siri ya sirikali" kisa eti kwa kuwa mhusika ni mteule kipenzi!
Mambo kama ya Bashite kutumia cheti fake hata hayo pia ni "siri ya sirikali" wahusika wooooooootttttttttttteeeeeee kimyaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!! Wanaoyaanika wanaonekana wabaya pamoja na kutoa ushahidi lakini kimyaaaaaa!
Ni mazingira hayo yanayowafanya watu wamwone Mange ni shujaa!.
Kwa mfano, kubandika namba ya Gari nyingine kwenye Gari nyingine ni kosa! Wahusika wapo pamoja na kupewa ushahidi lakini kimyaaaa! Hata kukanusha tu wameshindwa! Kisa, MTOTO wa mfalme haguswi!!!!!!!!!!
Tungeujua ukweli huu bila matusi ni nzuri zaidi, lakini ni Mara milioni tukaujua ukweli kwa lugha mbovu kuliko ukweli ukafichwa kwa lugha ya "staha" eti "ni mpambanaji wa madawa ya kulevya" wakati upambanaji kumbe ni kichaka cha kujifichia wakati "akifanya yake"! Mtashangaa tu michuma ya nguvu inapaki kwa mteule!
Mungu anaona!!!!!!!!! Mwaweza kuwanyamazisha wote lakini dhamiri zenu hamna ubavu wa kuzinyamazisha!!!!!!!!!! Kubwa kuliko yote hamwezi kumnyamazishaMungu!!!!!!!! Sema kikombe bado hakijajaa!!!!!! ndiyo maana inaonekana kama vile Mungu haoni!!!!!! Juweni kuwa subira ya Mungu inawavuta kwenye toba!!. Siku kikombe cha uovu kikijaa!!! ndipo mtakapojua kuwa kumbe Mungu alikuwa anaona!!!!!
 
Back
Top Bottom