Mkuu ni kweli kwamba kuna njia mbili kwenda Ukerewe yaani njia ya Bunda na kupitia Mwanza ila inategemea unatokea wapi, njia ya Bunda ni nzuri kwa wale wanaotokea Musoma, Tarime njia inayotokea Kenya kupitia Sirari na wilaya zote za mkoa wa Mara pamoja na wale wanaotokea Arusha kupitia Karatu, Ngorongoro, Serengeti. Kwani ukifika Bunda inakuchukua kama saa moja mpaka kufika Kisorya then unapanda ferry kwa dakika kama 20 to 30 hivi unaingia Ukerewe (umbali umezidi kidogo pale kigamboni ferry)
Mwanza ni kwa wale wanaotoka mikoa hii mingine yaani inayoingia Mwanza kwa kuunganisha barabara itokayo Dar to Mwanza pia kwa wale wanaotoka Kigoma na Bukoba kwa kuwa lazima wapiti Mwanza kwanza hivyo wakifika Mwanza wanapanda meli kwa masaa 4 then wanafika Ukerewe japokuwa wengine hasa wenye private transport na waogopa kusafiri kwenye maji hupenda kupitia Bunda kasha wanavuka dakika chache kwa ferry. Ukerewe inaundwa na visiwa viwili cha Ukala na Nansio (ambacho ndio unaingia kwa pande zote na ndicho kinabeba jina la Ukerewe na ni makao makuu ya wilaya). Ukifika Nansio then unapanda kivuko kingine kwenda Ukala unasafiri kama dakika 45 majini. Kwa kifupi ukiambiwa Ukerewe ujue kuna Nansio na Ukala na visiwa vingine vidogo vidogo kama ilivyo Unguja na Pemba kwa Zanzibar. Kwahiyo peleleza ujue umepangiwa Ukala au Nansio ili upate picha halisi wakati unakwenda.
Kwa ujumla wewe nenda ukapaone mwenyewe kwani maisha popote kikubwa wewe unatakiwa uwe na malengo in the next 10 years unataka uwe wapi na katika level ipi ya mafanikio kwani hata hawa wazee wetu tunaoona wamejenga Kapripoint-Mwanza, Shanty town Moshi, Uzunguni au Area C na D kwa Dodoma, Upanga au Masaki au msasani au kule Wilolesi na Gangilonga kwa Iringa sio walianzia hapo kwani ukiwauliza wanaweza wakakuambia walianza maisha sehemu kama Chamchuzi au kijumbura huko Karagwe au Mapanda kule Mufindi lakini mwisho wa siku wanakula bata. Ni vizuri kwenda na kuona hali halisi kwani watz wengi tunaijua nchi kwa kuangalia ramani hivyo kuna maeneo mengine unaweza ukayaona ya ovyo kumbe kama umekwenda kimkakati unaweza piga hela na kuamua kujenga popote na kuanzisha maisha. Lakini hizi kazi wakati mwingine inaweza ikawa imepatikana katika ambalo hulipendi lakini kwa kwenda kwako huko inakukutanisha na marafiki wapya na mwisho wa siku unaongeza wigo mpana wa kuangalia fursa zingine au unaweza ukakutana na fursa nyingine pia
Kuhusu wanga mkuu hiyo inategemea na wewe kwani kama una tabia za kiwanga wanga hata kama upo Dar bado wanga watakuathiri, kiujumla nimependa ushauri wa
Iselamagazi amesema wanga wapo ila wanarogana wao kwa wao hivyo kama na wewe ni mwanga itakua ngumu lakini kama sio mwanga basi utafanya kazi bila wao kukuathiri