Jamani ukerewe daaaah !

Jamani ukerewe daaaah !

Bora ungepangiwa hata Tandahimba au Nkasi ukalime mashamba but Ukerewe labda uvue samaki. Huko kuna kamji kanaitwa Nansio ndio makao makuu ya wilaya. Miaka na miaka imepita hata hakaendelei. Watu ni wivu wa mafanikio ya wenzao na uchawi tu.
 
Bora ungepangiwa hata
Tandahimba au Nkasi ukalime mashamba but Ukerewe labda uvue samaki. Huko
kuna kamji kanaitwa Nansio ndio makao makuu ya wilaya. Miaka na miaka
imepita hata hakaendelei. Watu ni wivu wa mafanikio ya wenzao na uchawi
tu.

kamanda kazi mbona unanitisha mkuu !
 
MIMI NIMEPANGWA SIMIYU KAMA.YUPO ANAYETAKA ANIPELEKE MBEYa au Rukwa
 
Tatizo Ukerewe wanga wengi huwezi kuendelea kama wenye mji wenyewe wameukimbia mwenyeji utauweza.
 
Kuna machungwaa mengi na samaki furahi banaa na mke utapata mkereweee
 
ndg,ucjali,kule mi ndo hme,kisiwa cha wasomi ktk tanzania.yale mambo ya ushirikina hakuna.cha mhmu,fika mapema,au 2taftane ntakpa dtails kamili,na ukikosa pakfkia,utafkia hata kwe2
We mtie moyo tu mara akifika huko anavuka tena anapelekwa Ukala maana k-star amesema amepangwa Ukerewe hajasema kama ni Nansio au Ukala maana anaweza vuka maji akajua ndio amefika mara anaambiwa kuna kisiwa kingine kinaitwa Ukala anavuka kwenda Bwisya. By the way Ukerewe si pabaya sana kama atajituma anaweza akawa na link nzuri tu na Mwanza na Musoma kwa shughuli za kijasiamari, akivuka ferry ya Kisorya anaingia Bunda thena anaamua kwenda Mwanza au musoma kama vipi anakatiza majini mpaka mwanza
 
Last edited by a moderator:
Maisha ni popote ndug xo huna budi kumshukuru mungu kwa kukupa ajira then after kaangalie mazngira ya eneo la kaz huwez jua may be ni mahali panapokufaa... piga kaz aisee...!
 
We mtie moyo tu
mara akifika huko anavuka tena anapelekwa Ukala maana
k-star amesema amepangwa Ukerewe hajasema kama
ni Nansio au Ukala maana anaweza vuka maji akajua ndio amefika mara
anaambiwa kuna kisiwa kingine kinaitwa Ukala anavuka kwenda Bwisya. By
the way Ukerewe si pabaya sana kama atajituma anaweza akawa na link
nzuri tu na Mwanza na Musoma kwa shughuli za kijasiamari, akivuka ferry
ya Kisorya anaingia Bunda thena anaamua kwenda Mwanza au musoma kama
vipi anakatiza majini mpaka mwanza

mkuu nielekeze hatua kwa hatua mpaka kufika hapo ukerewe. maana nasikia kuna kupitia BUNDA na kuna kupitia MWANZA kwenda moja kwa moja !
 
Last edited by a moderator:
Karibu Nansio, kumbuka kuja na nyavu za kuvulia samaki (mbogora).
 
Mkuu kama ni ukerewe basi anza mapema mazoezi ya kupiga mbizi kwenye madimbwi kabla hujafoka huko, utaweza kweli kupanda mitumbwi daily kwenda kazini? Pia kama huna Yesu jiandae kubebwa msukule ukafundishe makaburini usiku maana ukerewe ni hatari kwa ushirikina, Jiandae kuharibika lafudhi yako, mamba wanakuhusu pia.
 
mkuu nielekeze hatua kwa hatua mpaka kufika hapo ukerewe. maana nasikia kuna kupitia BUNDA na kuna kupitia MWANZA kwenda moja kwa moja !
Kufika ukerewe unaweza pita kwa meli kutokea mwanza kama 3 to 4 hours unafika, au kwenda mpaka Bunda then Kisoria halafu utavuka kwa pantoni kama 15 minutes
 
Kufika ukerewe unaweza pita kwa meli kutokea mwanza kama 3 to 4 hours unafika, au kwenda mpaka Bunda then Kisoria halafu utavuka kwa pantoni kama 15 minutes

shukrani sana Mpushi kwa maelezo yako mazuri !
 
Maisha ni popote ndug xo huna budi kumshukuru mungu kwa kukupa ajira then after kaangalie mazngira ya eneo la kaz huwez jua may be ni mahali panapokufaa... piga kaz aisee...!

asante kwa ushauri mzuri mkuu.
 
Jamaa hiyo safari inakutaka uambatane na jeshi la mbinguni. Unapanda zaidi ya usafiri aina tano? Ahsante Mungu wamenipeleka Musoma. Nikipitia hapa NAIROBI mda kidogn natokelezea mzigoni. Ila usife moyo. BWANA MUNGU ALIYE MWONGOZA ELIA JANGWANI ATAKUPIGANIA. Fanya kazi yako kwa moyo. Elekeza panapokutaka. Omba bila kikomo. Halafu nimeona ukipata mke KULE UKEREWE.
 
mkuu nielekeze hatua kwa hatua mpaka kufika hapo ukerewe. maana nasikia kuna kupitia BUNDA na kuna kupitia MWANZA kwenda moja kwa moja !
Mkuu ni kweli kwamba kuna njia mbili kwenda Ukerewe yaani njia ya Bunda na kupitia Mwanza ila inategemea unatokea wapi, njia ya Bunda ni nzuri kwa wale wanaotokea Musoma, Tarime njia inayotokea Kenya kupitia Sirari na wilaya zote za mkoa wa Mara pamoja na wale wanaotokea Arusha kupitia Karatu, Ngorongoro, Serengeti. Kwani ukifika Bunda inakuchukua kama saa moja mpaka kufika Kisorya then unapanda ferry kwa dakika kama 20 to 30 hivi unaingia Ukerewe (umbali umezidi kidogo pale kigamboni ferry)

Mwanza ni kwa wale wanaotoka mikoa hii mingine yaani inayoingia Mwanza kwa kuunganisha barabara itokayo Dar to Mwanza pia kwa wale wanaotoka Kigoma na Bukoba kwa kuwa lazima wapiti Mwanza kwanza hivyo wakifika Mwanza wanapanda meli kwa masaa 4 then wanafika Ukerewe japokuwa wengine hasa wenye private transport na waogopa kusafiri kwenye maji hupenda kupitia Bunda kasha wanavuka dakika chache kwa ferry. Ukerewe inaundwa na visiwa viwili cha Ukala na Nansio (ambacho ndio unaingia kwa pande zote na ndicho kinabeba jina la Ukerewe na ni makao makuu ya wilaya). Ukifika Nansio then unapanda kivuko kingine kwenda Ukala unasafiri kama dakika 45 majini. Kwa kifupi ukiambiwa Ukerewe ujue kuna Nansio na Ukala na visiwa vingine vidogo vidogo kama ilivyo Unguja na Pemba kwa Zanzibar. Kwahiyo peleleza ujue umepangiwa Ukala au Nansio ili upate picha halisi wakati unakwenda.

Kwa ujumla wewe nenda ukapaone mwenyewe kwani maisha popote kikubwa wewe unatakiwa uwe na malengo in the next 10 years unataka uwe wapi na katika level ipi ya mafanikio kwani hata hawa wazee wetu tunaoona wamejenga Kapripoint-Mwanza, Shanty town – Moshi, Uzunguni au Area C na D kwa Dodoma, Upanga au Masaki au msasani au kule Wilolesi na Gangilonga kwa Iringa sio walianzia hapo kwani ukiwauliza wanaweza wakakuambia walianza maisha sehemu kama Chamchuzi au kijumbura huko Karagwe au Mapanda kule Mufindi lakini mwisho wa siku wanakula bata. Ni vizuri kwenda na kuona hali halisi kwani watz wengi tunaijua nchi kwa kuangalia ramani hivyo kuna maeneo mengine unaweza ukayaona ya ovyo kumbe kama umekwenda kimkakati unaweza piga hela na kuamua kujenga popote na kuanzisha maisha. Lakini hizi kazi wakati mwingine inaweza ikawa imepatikana katika ambalo hulipendi lakini kwa kwenda kwako huko inakukutanisha na marafiki wapya na mwisho wa siku unaongeza wigo mpana wa kuangalia fursa zingine au unaweza ukakutana na fursa nyingine pia

Kuhusu wanga mkuu hiyo inategemea na wewe kwani kama una tabia za kiwanga wanga hata kama upo Dar bado wanga watakuathiri, kiujumla nimependa ushauri wa Iselamagazi amesema wanga wapo ila wanarogana wao kwa wao hivyo kama na wewe ni mwanga itakua ngumu lakini kama sio mwanga basi utafanya kazi bila wao kukuathiri
 
Back
Top Bottom