Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 593
- 1,376
Yaani kuzungumza na watu wawili ndio imekuwa "Wakazi wa Dar"? Jambo mmeanza kuzingua.
=====
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kutokana na huduma ya umeme kurejea baada ya kuwapo kwa hitilafu katika gridi ya Taifa iliyodumu kwa saa kadhaa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakazi hao wamesema walikuwa na hofu ya bidhaa walizoziacha kwenye jokofu kuharibika kwa joto kali lakini hatua ya kurejea kwa umeme imeleta ahueni kwao
“Watu wengi sana ikiwamo mimi bado wapo kwenye sikukuu na walitumaini kwamba bidhaa zao zingekuwa salama kutokana na kutokukatika kwa umeme kwa siku nyingi, sasa usiku umeme umekatika ghafla sijui ingelikuaje kama usingerejea mapema” Amezungumza Amina Rajab mkazi wa Magomeni Kota.
Naye, Ramadhani Mubaarak ambaye amejiajiri kupitia mtandaoni amesema yeye amefika kazini akiwa hajui kama umeme utarudi ama la lakini kabla ya kupata athari zaidi katika kazi yake, umeme ulirejea.