Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kutokana na upatikanaji wa hewa safi katika fukwe zote za bahari.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakazi hao wamesema toka ameingia madarakani kiasi cha hewa ya oksijeni kimeongezeka mara dufu ukilinganisha na awamu zilizopita.
“Watu wengi sana ikiwamo mimi walishuhudia upungufu mkubwa wa hewa ya oksjeni katika "atmosphere*, ambayo kwa kiasi kikubwa ilichangiwa na vyama vya upinzani hasa CHADEMA, lakini kutokana jitahada za rais kupitia falsafa yake ya 4Rs kila kitu kimekuwa sawa” Amezungumza Lucas Mwashamba mkazi wa Mbozi.