Jambo TV: Wakazi wa Dar wamshukuru Rais kwa huduma ua umeme kurejea!

Wabongo wamefanywa mazombi hatari, kwani hitilafu na ubovu wa MIUNDOmbinu, ulisabsbishwa na Rwanda au Kenya! ?
Uchawa kila sehemu,unamshukuru house girl kwa kuhakikisha nguo zimetakata! Kwani cha ajabu nini! Analipwa mshahara ili atakatishe nguo! Nguo zikitakata, ndio kazi, yake,na stahili yake ni salary tu,
Ingetokea jambo LA kipekee, kama vile nyumba imeshika moto kwa hitilafu ya umeme! House girl yupo peke yake na watoto,kwanza akatoa watoto nje, pili akafanikiwa kuingia chumba cha boss wake, akaokoa nyaraka nyeti za kampuni, na pesa,tatu, akaweza kukata umeme, na kupanda dalini na kuzima moto, nyumba ikapona, hasara ikawa ndogo! Hapo lazima umshukuru!
Sasa samia kafanya nini cha upekee!! Kuteua majambazi!?
So patheitic
 
Nchi ina watu wa hovyo sana hii zaidi ya neno hovyo
Nchi imejaa
Chawa
Viriboto
Kunguni
Viwavi
 
Kwanza napenda kutoa shukrani zangu za dhati kumshukuru Mh rais kwa kuturejeshea umeme.
 
Hili ajuza ni jitu la ovyo toka kupata uhuru.

Pumbavu wamekata tena sasa hivi.
 
Kabla hajakua Raisi Umeme ulikuwepo na ulikuwa haukatiki sasa hizi pongezi ziwe tunamshukuru Raisi kwa kuturejeshea Umeme aliokuwa ameukata.

Hii itaeleweka vizuri.
 
😆😆😆😆😆
 
sure wameshukuru sana...

maana hawakua hewani mda mrefu sana leo dah....
 
Mkikosa cha kuandika, jaribuni kuwatafuta raia watawapa habari za kuandika.
Huko mitaani kuna kero lukuki.
Watawapa habari za kuandika tena za maana kuliko hizo habari zenu.
 
Tunaendelea kumshukuru hata kama wameuchukua tena, tuzidi kumshukuru mheshimiwa

Ameen.

Kwa kuukata tena anatupa mitihani kupima imani zetu, kwa maana yeye anajua shida zetu za umeme na mahitaji ya mioyo yetu.

Samia ametoa umeme.... Samia ametwaa umeme.... Tumshukuru kwa Yote.... Jina lake lihimidiwe
.
 
Mimi nimshukuru Rais kwa huu utulivu unaoendelea muda huu hata kuwezesha umeme huo kurudi bila wananchi kuleta dingombingo hasa ukiangalia leo ni mapumziko wa wakristu wengi wapo majumbani. Ingekuwa ngumu sana kumaliza siku bila umeme
 
Tunaendelea kumshukuru hata kama wameuchukua tena, tuzidi kumshukuru mheshimiwa

Ameen.


Kwa kuukata tena anatupa mitihani kupima imani zetu, kwa maana yeye anajua shida zetu za umeme na mahitaji ya mioyo yetu.

Samia ametoa umeme.... Samia ametwaa umeme.... Tushukuru kwa Yote.... Jina lake lihimidiwe
.
 
Hii ni dharau wakuu...sidhani hata kama mwenyewe anafurahia mambo haya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…