Pre GE2025 Jambo TV yasema itarusha Live mkutano wa CHADEMA licha ya kupewa vitisho

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Still bado kuna nafuu mkuu.
 
Naogopa wasije wakawazingira!
 
Nadhani Mh. Rais alikuwa ana danganya watu na 4R zake.
Haya tunayo yaona siku hizi za karibuni ni ishara tosha kwamba kuna ulaghai ulio kithiri kwenye kauli ya 4R. Pia tume ya haki jinai ilikuwa ni Issue ya matumizi mabaya ya kodi zetu. Hakukuwa na sababu za msingi kuanzisha ile thme na kuwapa facility zote kwa gharama za Watanzania halafu vyombo vya dola vina fanya mambo ya utawala wa Magufuli.
Na Rais amekaa kimya kama msemo wake wa chura.
Kama alikuwa ame maanisha na 4R zake tulitegemea kuona IGP, kamishna wa Mafunzo na operesheni na Waziri mwenye dhamana ya Wizara ya mambo ya ndani wakiwa wamesha tuachia ofisi zetu
Tuna laani yanayo fanyika hivi sana kwa vyama vya upinzani na Rais amekaa kimya.
Hii ina tuaminisha kuwa ni kweli Chadema wali gundua ulaghai wa hali ya juu kwenye vikao vya maridhiano ambavyo havikuwa na tija.
 
Ukiona yanayofanyika sasa hivi unajua maji yameshazidi unga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…