Jameni walokole, hivi haya maneno mnayatumia vile yanavyopaswa ama mnatulisha matangopori?

Mkuu nikianza kukupiga maswali ya kidini unaweza kunijibu vizuri?
 
Ushindwe kwa jina la yesu , wewe una roho ya mpinga Kristo
Hapana sishindwi, na mimi ni mktisto pia, niko hapa kutetea na kubaki kwenye misingi ya dini..kuwatoa nje ya msitari wapuuzi wachache wanaotaka kuaribu kabisa mantiki ya ukristo.
Hakuna ukristo mambo leo.
Mmeingiza matakataka mengi kwenye ukristo.
Saiz tunaona zinabarikiwa ndoa za jinsia moja(havimiliki)
Tunaona wanawake wanakuwa wachungaji na inachukuliwa ni kawaida.
Watu wanasali kwa kupiga mayowe.
Watu wanaongea lugha za ajabu kwamba wanawasiliana na Mungu kwa lugha maalum.
Kanisani kumekuwa na michango lukuki kupitiliza na imekua ni kawaida.
Makanisa yamekuwa na mamisalaba na mapicha ya Yesu(haikubaliki) na wacha nichambue hii

Waebrania11:1
“Imani ni bayana ya mambo yatarajiwayo, ni hakika mambo yasiyoonekana”
Imani ni bayana ya mambo ya kiroho mambo yasiyo-onekana. Yatupasa kuamini bila ya kuona.
Picha ya Yesu na nan ana uwakika kweli yule ni yesu? Kuna matoleo mangapi za picha za yesu?
MSALABA
Nan ana uwakika yesu alipigiliwa kwenye jumlisha ama x ama fito iliyosimama?
Biblia ilipotaka tuamini pasipo kuona, Mungu alishajua kuna…. Inatosha

Watu wangu wanapotea kwa kukosa maarifa
 
Wewe ni dhehebu gani mkuu.
 
Okoka mpendwa yesu anakupenda , bila kubatizwa kwa maji marefu na kumpokea yesu awe bwana na mwokozi wa maisha yngu ni kazi bure
 
Kwahiyo watu wasipokee roho mtakatifu wakanena kwa lugha mpyaa🫥🫣

Mchungaji inabidi asukume range ili utukufu wa Mungu uonekane kwa mtumishi wake
 
Yesu hakuacha dini.
Mimi ni mkristo. Maana yake mfuasi wa kristo.
Wakusanyikapo wawili watatu kwa ajili yake, teyari ni kanisa.
Hajasema dhehebu.
Ukifata madhehebu utapotea
Saafi tupange siku tukusanyike mimi na wewe kuna maswali unijibu😂🙏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…