Ulimbo
JF-Expert Member
- Aug 14, 2009
- 3,768
- 4,038
Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Mh James Mbatia amefika Mkoani Mbeya kwa ziara ya kichama na Kupokelewa na RC wa Mkoa huo huku akiahidiwa ulinzi.
Katika ziara yake hiyo ya kichama atafika Busokelo ambako atapokea wanachama wapya wa chama hicho kutoka Chadema.
Ziara hii imekuja baada ya jana kufika ikulu kuteta na Mh. Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM.
Ina maana hiyo ziara ni matokeo ya kukutana na Rais? Je hao wanachama walikuwa tayari wameshaandaliwa na alienda Ikulu kuomba kibali cha kuwapokea? au ina maana katumwa na mwenyekiti mwenzake wa chama kingine walipokutana ikulu ili wakisha ingia nccr then wapitilize moja kwa moja hadi kijani?