James Mbatia amkingia kifua Spika Ndugai, kwenda mahakamani kuzuia mchakato wa kutafuta Spika mpya

James Mbatia amkingia kifua Spika Ndugai, kwenda mahakamani kuzuia mchakato wa kutafuta Spika mpya

imetoa funzo kuwa waafrika huwa tunatumika tu kama tambala na kutupwa huko, swala la spika kujihuzuru kisa ametoa maoni yake ni udikteta wa hali ya juu sana.
Cha kushangaza si bbc, Dot welle ya ujerumani ,chadema, Act wazalendo wala Ulimwengu waliokemea udikteta huu!.
Kama ingekuwa ni kipindi cha Magufuli ungeona ambavyo mishipa imewatoka kukemea udikteta kisa tu alikuwa anawabananga kwelikweli kwenye ulaji wao, leo kwa kuwa rais Samia amewaachia wale jinsi wanavyotaka basi wako kimyaaa wanakenua meno kana kwamba hawaoni kuwa kama kiongozi wa mhimili kama bunge anaweza kufukuzwa kwa kutoa maoni je wewe kikaragosi wa Maswa ndani ndani itakuwaje?
Kipindi cha Magufuli hata kufukuza watumishi hewa waliita ni udikteta.
Dada andamana tukutengue kiuno ! Wapuuz nyie,mlikuwa mnamchukulia poa Samia
 
huu ni umaarufu wa kijinga ,,yani lijitu limejiuzulu mwenyewe nyie mnamtetea,,muacheni aondoke kabisa na wale covid-19

Ahaha ww ni mwanaume uwezi kwenda, zile ni nafasi za wanawake
 
Kumekucha! Unaweza kukuta shughuli ndio kwanza imeanza [emoji2960]
 
Ndugayi sasa ndio anaona jinsi alovyowakataa wapinzani
Kumbe wangekuwa msaada wake
Lakini amechelewa ishi na watu vizuri jaman
Alichaguliwa kuwa spika wa bunge Novemba 17, 2015 baada ya kupata kura 254 kati ya 365, na mpinzani wake Goodluck Ole Medeye kutoka CHADEMA akipata kura 109, huku kura mbili zikiharibika.

Kwenye bunge lililokuwa na mchanganyiko huu, Ndugai asingejiuzulu kwani ili afukuzwe na bunge zinahitajika kura theluthi mbili ambazo ni 244 zimkatae. Lakini kwa upande mwingine angekuwa amewashika CHADEMA vizuri, angeweza kupata kura zote za CDM 109 na kushawishi kura 3 tu kutoka CCM jumla 122 ili kuzuia asifukuzwe!

Sasa ndipo tunazidi kuona madhira ya uchaguzi wa 2020.
 
Kama hiyo barua imekosewa maana yake tuna watu wengi ambao hawaisomi katiba, Katiba Mkuu CCM haisomi, Katibu wa bunge haisomi, na wengi wananchi wa kawaida hawaisomi.

Lakini pia inawezekanaje Ndugai kwa experience yake serikalini akosee mtu wa kumu-address? hapa madai ya kulazimishwa kujiuzulu yanapata nafasi kubwa, inawezekana kuna wajinga wameandika barua wakamlazimisha aitume huko kwa KM wa CCM.
 
Hivi kuna mwana ccm hata mmoja aliejitokeza na kuwa upande wake,?
labda awe hataki tena kuwa mbunge na amejichoka. Waulize Lowasa na Sumaye mziki wa CCM. Ni mziki mnene hadi mwenyewe unarudi
 
Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Mhe.James Mbatia amesema atakwenda Mahakamani kuzuia mchakato wa kumpata Spika mpya wa Bunge kwa sababu Mhe.Job Ndugai hakufuata taratibu za kisheria na kikatiba kujiuzulu nafasi ya Spika wa Bunge.
Huo utaratibu wa kikatiba unaoutaka ambao hauko kwenye katiba ni upi? Tupatie vifungu vya katiba.
Mimi katiba niliyo nayo haina kujizulu na hivyo hakuna utaratibu wa kujiuzulu. Soma kifungu cha 84

(7) Spika atakoma kuwa Spika na ataacha kiti cha Spika

litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo -

(a) iwapo mtu huyo alichaguliwa kutoka miongoni mwa

Wabunge, basi ikiwa atakoma kuwa Mbunge kwa

sababu yoyote ambayo haihusiki na kuvunjwa Bunge;

au

(b) ikiwa kutatokea jambo lolote ambalo, kama

asingekuwa Spika, lingemfanya mtu huyo asiwe na

sifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguzi wa

Spika; au

(c) Bunge litakapokutana kwa mara ya kwanza baada ya

Uchaguzi Mkuu uliofanywa baada ya Bunge kuvunjwa,

lakini masharti ya aya hii yatatumika bila ya kuathiri

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

masharti ya ibara ndogo ya (4) ya ibara ya 90 ya

Katiba hii; au

(d) ikiwa mtu huyo ataondolewa kwenye madaraka ya

Spika kwa azimio la Bunge lililoungwa mkono na

Wabunge amabo idadi yao haipungui theluthi mbili ya

Wabunge wote; au

(e) ikiwa mtu huyo atashindwa kuwasilisha kwa Rais

tamko rasmi kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo

(5) ya ibara hii; au

(f) ikiwa mtu huyo atapatikana na hatia kwa kosa la kutoa

habari za uongo, kwa kiapo kinyume cha sheria ya

Kanuni ya jinai, kuhusu tamko rasmi lolote lililotolewa

kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (3) ya ibara

hii; au

(g) ikiwa mtu huyo atashindwa kuwasilisha kwa Rais

taarifa ya mali kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo

ya (5) ya ibara hii kabla ya kumalizika muda uliowekwa

kwa ajili hiyo kwa mujibu wa sheria iliotungwa na

Bunge;

(h) ikiwa itathibitika kuwa mtu huyo amevunja masharti ya

Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
 
View attachment 2071935
Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Mhe.James Mbatia amesema atakwenda Mahakamani kuzuia mchakato wa kumpata Spika mpya wa Bunge kwa sababu Mhe.Job Ndugai hakufuata taratibu za kisheria na kikatiba kujiuzulu nafasi ya Spika wa Bunge.
Huyu "Mama Tanzania"😂 ameibukia tena huku?
 
View attachment 2071935
Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Mhe.James Mbatia amesema atakwenda Mahakamani kuzuia mchakato wa kumpata Spika mpya wa Bunge kwa sababu Mhe.Job Ndugai hakufuata taratibu za kisheria na kikatiba kujiuzulu nafasi ya Spika wa Bunge.
Nia yake naiona ni njema, lakini anamtafutia matatizo mengine Jaji Mkuu, Afrika sio Bara nyepesi, ni Bara gumu mno kuliko Mabara yote Duniani.

Mhimili mmoja ndio unaamua kuhusu mihimili migine. Na hakuna yeyote anaweza fanya kitu.
 
😂Huyo "SUPIKA📣" asiyejua utaratibu wa "kikatiba" wa kuandika barua ya kujiuzuru aliwezaje kusimamia utungaji wa sheria?.."ONLY IN TANZANIA"

👇👇👇👇
Kwa mujibu wa www.parliament.go.tz
Nafasi yake iko wazi na vikao vya kamati vimesitishwa,taratibu za uchaguzi zinaendelea.

KAZI IENDELEE 💪🇹🇿👍
 
Mwammbieni ampe kadi ya chama chake.
Akawe spika wa bunge wa chama chake.
Mnaomtetea ndugai HAMJIELEWI.
 
View attachment 2071935
Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Mhe.James Mbatia amesema atakwenda Mahakamani kuzuia mchakato wa kumpata Spika mpya wa Bunge kwa sababu Mhe.Job Ndugai hakufuata taratibu za kisheria na kikatiba kujiuzulu nafasi ya Spika wa Bunge.
Nadhani anapoteza muda. Ila wana siasa waache tu!!!
 
Back
Top Bottom