Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Mhe.James Mbatia amesema atakwenda Mahakamani kuzuia mchakato wa kumpata Spika mpya wa Bunge kwa sababu Mhe.Job Ndugai hakufuata taratibu za kisheria na kikatiba kujiuzulu nafasi ya Spika wa Bunge.
Huo utaratibu wa kikatiba unaoutaka ambao hauko kwenye katiba ni upi? Tupatie vifungu vya katiba.
Mimi katiba niliyo nayo haina kujizulu na hivyo hakuna utaratibu wa kujiuzulu. Soma kifungu cha 84
(7) Spika atakoma kuwa Spika na ataacha kiti cha Spika
litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo -
(a) iwapo mtu huyo alichaguliwa kutoka miongoni mwa
Wabunge, basi ikiwa atakoma kuwa Mbunge kwa
sababu yoyote ambayo haihusiki na kuvunjwa Bunge;
au
(b) ikiwa kutatokea jambo lolote ambalo, kama
asingekuwa Spika, lingemfanya mtu huyo asiwe na
sifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguzi wa
Spika; au
(c) Bunge litakapokutana kwa mara ya kwanza baada ya
Uchaguzi Mkuu uliofanywa baada ya Bunge kuvunjwa,
lakini masharti ya aya hii yatatumika bila ya kuathiri
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
masharti ya ibara ndogo ya (4) ya ibara ya 90 ya
Katiba hii; au
(d) ikiwa mtu huyo ataondolewa kwenye madaraka ya
Spika kwa azimio la Bunge lililoungwa mkono na
Wabunge amabo idadi yao haipungui theluthi mbili ya
Wabunge wote; au
(e) ikiwa mtu huyo atashindwa kuwasilisha kwa Rais
tamko rasmi kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo
(5) ya ibara hii; au
(f) ikiwa mtu huyo atapatikana na hatia kwa kosa la kutoa
habari za uongo, kwa kiapo kinyume cha sheria ya
Kanuni ya jinai, kuhusu tamko rasmi lolote lililotolewa
kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (3) ya ibara
hii; au
(g) ikiwa mtu huyo atashindwa kuwasilisha kwa Rais
taarifa ya mali kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo
ya (5) ya ibara hii kabla ya kumalizika muda uliowekwa
kwa ajili hiyo kwa mujibu wa sheria iliotungwa na
Bunge;
(h) ikiwa itathibitika kuwa mtu huyo amevunja masharti ya
Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;