James Mbatia amkingia kifua Spika Ndugai, kwenda mahakamani kuzuia mchakato wa kutafuta Spika mpya

James Mbatia amkingia kifua Spika Ndugai, kwenda mahakamani kuzuia mchakato wa kutafuta Spika mpya

imetoa funzo kuwa waafrika huwa tunatumika tu kama tambala na kutupwa huko, swala la spika kujihuzuru kisa ametoa maoni yake ni udikteta wa hali ya juu sana.
Cha kushangaza si bbc, Dot welle ya ujerumani ,chadema, Act wazalendo wala Ulimwengu waliokemea udikteta huu!.
Kama ingekuwa ni kipindi cha Magufuli ungeona ambavyo mishipa imewatoka kukemea udikteta kisa tu alikuwa anawabananga kwelikweli kwenye ulaji wao, leo kwa kuwa rais Samia amewaachia wale jinsi wanavyotaka basi wako kimyaaa wanakenua meno kana kwamba hawaoni kuwa kama kiongozi wa mhimili kama bunge anaweza kufukuzwa kwa kutoa maoni je wewe kikaragosi wa Maswa ndani ndani itakuwaje?
Kipindi cha Magufuli hata kufukuza watumishi hewa waliita ni udikteta.
Tulia weweee...la sivyo utaanza kuhudhuria clinic ya moyo...si kwa hiz hasira ulizokuwa nazo..kpnd cha magu mlikuwa mnanyonga tu kamkujifunza kuchinjaa....sasa yamewafika mnaanza kupiga mikelele....muache ****** avune alichopanda
 
Hata kwenye talaka kuna wengine huwa ni ving’ang’anizi unasema nimekupa talaka anakuambia twende mahakamani
Naona inakaribiana na hii kidogo
 
Haijalishi ameondoka lwa usahihi ama isivyo ila aende zake huyo shem wa Yesu.

Kwani yeye aliwaingiza wale covid 19 wakina mzee kwa kufuata katiba?


Hawa watu wa ajabu wakina Mbatia wanatokea wapi? Wapumzike huko jamani aaaarrrrghhhr
 
"Utaratibu uliofanyika jana wa Job Ndugai kujiuzulu Uspika wake kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara 149 haikufatwa, kwahiyo ndugu Ndugai mpaka sasa hivi bado ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitakiwa kwenda kujiuzulu mbele ya Kikao cha Kamati ya Bunge”

Asema James Mbatia, Mwenyekiti NCCR Mageuzi.
 
Si yupo Naibu Spika yeye ndio atawahabarisha wabunge kilichojiri kisha mchakato wa uchaguzi wa Spika utaendelea.
 
Mzee Mbatia anakurupuka sana, sijui ana matatizo gani.
huenda ana matatizo ya kisaikolojia yanamsibu.
 
Kweli what goes around comes around. Huyu si ndio aliwang'ang'ania wale wanawake 19 pamoja na kuvuliwa uanachama na chama chao? Na pia alikataa kumtoa ubunge yule jamaa wa Mtwara pamoja na kua jamaa alijiuzulu mwenyewe!!!

Sasa naona wachambuzi wanasema eti na yule aliyekua anakataa barua za vyama kuwakana wabunge wao anaambiwa barua yake haitambuliki

Nchi ngumu hii!!!
 
Basi mwambieni agome kutoka kwny nyumba ya spika na kurudisha lile joho.
 
Mimi ni mjumbe tu...[emoji2297]
IMG-20220107-WA0001.jpg
 
Kama hiyo barua imekosewa maana yake tuna watu wengi ambao hawaisomi katiba, Katiba Mkuu CCM haisomi, Katibu wa bunge haisomi, na wengi wananchi wa kawaida hawaisomi.

Lakini pia inawezekanaje Ndugai kwa experience yake serikalini akosee mtu wa kumu-address? hapa madai ya kulazimishwa kujiuzulu yanapata nafasi kubwa, inawezekana kuna wajinga wameandika barua wakamlazimisha aitume huko kwa KM wa CCM.

Si ajabu na hata kwenye kuituma pia. Kwani Ayubu mwenyewe hata hadharani kaonekana?
 
Kumekucha! Unaweza kukuta shughuli ndio kwanza imeanza [emoji2960]
We jamaa utakuwa umekatiwa mrija , comment zako nyingi zinatia huruma sikuhizi. Kipindi cha mwendazake ulikuwa unapiga sana makofi, mwacheni SSH ajenge nchi ndio kwanza ana miezi 9.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom