James Mbatia amtaka Majaliwa ajiuzulu Uwaziri Mkuu

Majaliwa pia ni mtu muongo anasema uongo akiwa msikitini ilo nalo linamtosha kujiuzuru tu
 
Hapana tusimuonee Majaliwa. Kama katiba yetu haisemi wazi nini kinatakiwa kufanyika makamu rais akirithi urais,inabidi tuwalaaum ccm kwa kukataa katiba mpya ambayo ingeweka Kila kitu wazi na kwa utashi wa wananchi wenyewe. Kwa Sasa tumuachie Mama Suluhu atafute suruhu kwa busara zake. Ila Minyani itakayokataa katiba mpya ndiyo tuikome.
 
Ni kweli Rais huwa harithi watu..hawa wote waliapa kiapo cha utii mbele ya Rais ambaye ni Marehemu,

Sasa wanatakiwa kuapa kiapo cha utii mbele ya Mama Samia.

Huwezi kufanya kazi na mtu mwenye kiapo kingine protocol inagoma hapo!!

Cha msingi ni ajiuźulu ama asipojiongeza basi mama avunje balaza lote aanze na Mwanasheria Mkuu!!

Tatizo CCM hawataafiki hoja hii...wazoefu wa kuvunja katiba na Protocol.
 
Hivi hapa duniani kuna nchi haina hayo mambo uliyoyasema.
 
Yes ofcourse, kwa nature ya watanzania wanatakiwa kuongozwa kama mifugo sababu ustaarabu ni kipengele kwao. Awe na elimu asiwe nayo wana asili ya ujuaji sana ndugu zetu hawa.
Tutamkumbuka sana yule mzee hata kama sio HADHARANI basi NAFSI zetu zitatusuta I SWEAR

Hivi kaka unaweza kuniambia watanzania wanataka nini ? SIJAJUA nini kimelikumba Taifa hili Mimi sijui kwa kweli
Naona tuna ambaa ambaa tuu
 
PM kama Rais wafuate matakwa ya sheria. Ni bahati mbaya sana kama Mbatia ni mouth piece ya Rais wa JMT. Hakuna mtu aliye mnyanganya Rais madaraka yake ya kuvunja baraza la mawaziri na kuweka anao wataka. Hata kubadilisha serikali yote bado viko mikononi mwake.

Kwa maneno mengine kujenga ama kubomoa ni maamuzi yake. Jana kahakikishiwa utii na vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi autumie atakavyo na impendezavyo.
 
Ajiuzulu kwa sababu zipi hasa? kwani Rais ameshavunja baraza la mawaziri?
 
Huo ni uchochezi sasa

Mwanasheria nguli Dr Mwigullu Nchemba alishatoa ufafanuzi!
Si ili asikose kitumbua chake ndiyo sababu akasema halazimiki? Ningeshangaa kama angeshauri baraza livunjwe hasa baada ya kuonja raha ya kuukosa uwaziri.
 
Rais ana uwezo wa kulivunja baraza la mawaziri, hata kama PM asipojiuzulu.
 
Nilikua nafikiri mbatia ni mtu wa maana, kumbe ovyo kabisa. Mh. Rais dhibiti hii kitu mapema.
Hapa ndipo pengo la Magufuli litaonekana mapema mno. Wanasiasa wapuuzi aina ya Mbatia...

Raisi angekuwa anafanya jambo lenye madhara kwa raia he would have been right.

Ni sawa na mtu uendeshe gari halafu abiria walioko nyuma wanakuambia mataa hayo mbele usimame sasa! Ilihali una utashi wako na unajua la kufanya.

Tuta hilo ukanyage breki sasa mzee usije ukalitupa gari.

Zebra hio simamisha upishe watu wapite dereva.

Katika mazingira ya aina hii dereva lazima mtaishia kumuona mbaya tu.
 
Moja ya kauli inayo onyesha udhalilishaji kwa kuonyesha Rais hawezi kuvunja baraza la mawaziri kwakua anamuogopa/ anamuonea aibu waziri mkuu. Nimawazo ambayo sikutegemea kama yatatolewa na Mbatia.
 
Mama samia inatakiwa awe na msimamo, akisikiliza hawa watu atapotea...
Leo hili kesho lile, wasuniri rais wao aingie madarakani aunde serikali alafu wamwbie waziri mkuu wao ajiuzulu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…