James Mbatia amtaka Majaliwa ajiuzulu Uwaziri Mkuu

James Mbatia amtaka Majaliwa ajiuzulu Uwaziri Mkuu

Wewe Mpaka piko jiuzulu mzee mpe space mama samia achague timu yake

Raisi.jpg
 
Mbona mnamlazimisha sana wazee, mnataka mama abaki pekeake ili mumpelekeshe jinsi mnavyojiskia 😁😁😁!!?

Sasa kwa taarifa yenu atajiuzulu kisha atateuliwa upya acheni utoto!
Tumpelekeshe mama Samia kivipi?
Kwani Mama Samia hajitambui?
Unataka kusema Mama Samia anamuhitaji Majaliwa ili asipelekeshwe?
Huko ni kumdhalilisha wazi wazi Rais wetu, Mama Samia Suluhu.

Mama Samia kwa sasa ndio rais wa Tanzania wa awamu ya Sita. Lazima apewe nafasi ya kuunda serikali yake na kufanya kazi zake kwa uhuru na haki.

Majaliwa aliteuliwa kuwa waziri mkuu chini ya utawala wa awamu ya tano ulioongozwa na Magufuli. Magufuli hayupo tena madarakani, Majaliwa anawajibika kwa rais yupi?

Majaliwa anapaswa kujiuzuru ili kulinda heshima yake, kuilinda katiba na kulinda heshima ya taifa la Tanzania.

Majaliwa jiuzuru sasa.
 
Sio vichwa vigumu bali ni wajuaji. Ndio maana ili utawale vyema ni muhimu kuwaziba midomo wapuuzi maana watakuyumbisha katika mission yako! Hiki ndio alikifanya Magufuli akaonekana katili ila dhamira ilikua njema kabisa.

Yani kuongoza Tanzania ni sawa na kufundisha darasa la wanafunzi 200 ukitarajia kutakuwa na hali ya utulivu na ustaarabu katika kuuliza maswali na majibu ila badala yake kila mtu ananong'ona na kuropoka ovyo bila utaratibu halafu kuadhibiwa hawataki.

Wana expect wafanyiwe ustaarabu ambao wao hawana, hao ndio watanzania bana.😁
Dikteta hajawahi kua na dhamira njema
 
Chezea ugali utaribu ni ule ule kama walivompa urais bana piga chini baraza maisha yaanze moja
 
Hahahahah

Baki na Mavi yako Nyumbani

Ntamiss sana Mtani wetu JPM
Hata Mimi mtani wangu namkubali saana. Ile roho, ujasiri, na uthubutu haumithiliki kirahisi.

Au nasema uongo ndugu zangu!

Mara Baki na Mavi yako. [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Huo ni uchochezi sasa

Mwanasheria nguli Dr Mwigullu Nchemba alishatoa ufafanuzi!
Siku hizi siyo mchumi first class! hata kama PM atagoma kujiuzulu bado rais anayo mamlaka ya kuvunja baraza la mawaziri, kufanya reshuffle na hata ku-suspend bunge na kurudi kwenye uchaguzi...
 
Wanasiasa wana maneno sana. Hawa wapinzani ni wepesi sana kuongea, ila wao huwa KAMWE hawatoi mifano au kutenda yale wanayoyahubiri. Mfano, ni uwajibikaji wa kidemokrasia, pale chama kinaposhindwa uchaguzi, basi kiongozi wa juu wa chama hicho kujiuzuru. Last year Jeremy corbyn alijiuzuru baada ya kubwagwa na boris. Huyu mbatia mbona yeye hajiuzuru kwa chama chake kuangushwa?
 
Mbona Marais wa nchi nyingine wanaongoza huku wakikosolewa na nchi za zinapata maendeleo kuliko TZ
Ina maana viongozi wetu ni vichwa panzi sana kiasi kuwa sauti kidogo tu za maoni tofauti zinawachanganya Hadi wanashindwa kazi?
Jiwe alikuwa kichwa panzi kiasi hicho au ni kiburi?😂
Baadhi ya Mitz ni mijitu mijinga sn..... Kwao rais ni mungu wao yani
 
Hapana tusimuonee Majaliwa. Kama katiba yetu haisemi wazi nini kinatakiwa kufanyika makamu rais akirithi urais,inabidi tuwalaaum ccm kwa kukataa katiba mpya ambayo ingeweka Kila kitu wazi na kwa utashi wa wananchi wenyewe. Kwa Sasa tumuachie Mama Suluhu atafute suruhu kwa busara zake. Ila Minyani itakayokataa katiba mpya ndiyo tuikome.
Katiba iko wazi kabisa, ni kwa wale wasioisoma au wale wanaoisoma kwa kupindishapindisha tu kwa ajili ya ajenda zao tu. Angalia, katiba yetu inasema hivi:
1616866030184.png

1616866092167.png

1616866154621.png
1616866206509.png

1616866344647.png


Angalia kifungu kidogo hicho cha (10) nilichowekea rangi, kuwa mtu atakayechukua madaraka ya urais ama kwa kurithi kutokana na kifungu kidogo cha (3) (yaani rais kuondolewa madarakani na baraza la mawaziri) hadi kifungu kidogo cha (5) (yaani rais akifariki), hana madaraka ya kuvunja Bunge au Baraza la mawaziri au kutengua teuzi za rais aliyekuwapo.
 
Back
Top Bottom