James Mbatia amtaka Majaliwa ajiuzulu Uwaziri Mkuu

James Mbatia amtaka Majaliwa ajiuzulu Uwaziri Mkuu

Ajiuzulu kwa sababu zipi hasa? kwani Rais ameshavunja baraza la mawaziri?
Sababu za kujiuzulu ameweka mleta uzi....Huwa waziri mkuu anapojiuzulu basi automatically baraza la mawaziri linavunjika hapo hapo
 
Hapana tusimuonee Majaliwa. Kama katiba yetu haisemi wazi nini kinatakiwa kufanyika makamu rais akirithi urais,inabidi tuwalaaum ccm kwa kukataa katiba mpya ambayo ingeweka Kila kitu wazi na kwa utashi wa wananchi wenyewe. Kwa Sasa tumuachie Mama Suluhu atafute suruhu kwa busara zake. Ila Minyani itakayokataa katiba mpya ndiyo tuikome.
Kuweka sawa tu hapa.
Katiba imesema wazi, rais akifariki, mtu mwingine anakuwa rais. Na mtu huyo ni makamu wa urais. Urais wa Tz sio jambo la kurithishana bali ni jambo la kikatiba.

Mama Samia kwa sasa ni rais wa Tanzania mwenye mamlaka yote sawa sawa na marais wengine wote waliopita. Anapaswa kuunda serikali yake kwa kuteua baraza lake la mawaziri kama marais wengine waliopita.
 
Madam President ana karoho ka kumuenzi Hayati JPM hivyo msitarajie mapya sana toka kwake zaidi ya kuendeleza yaliyopo.
 
Mbona mnamlazimisha sana wazee, mnataka mama abaki pekeake ili mumpelekeshe jinsi mnavyojiskia 😁😁😁!!?

Sasa kwa taarifa yenu atajiuzulu kisha atateuliwa upya acheni utoto!
Watu wanamuogopa sana waziri mkuu wetu Majaliwa kwasabababu ni mchapakazi hodari, sasa wanataka mama Samia hasiwe na nguvu ili wampelekeshe wapendavyo, mimi namwomba huyu mama hawe mkali na mwenye msimamo.
 
Kuweka sawa tu hapa.
Katiba imesema wazi, rais akifariki, mtu mwingine anakuwa rais. Na mtu huyo ni makamu wa urais. Urais wa Tz sio jambo la kurithishana bali ni jambo la kikatiba.

Mama Samia kwa sasa ni rais wa Tanzania mwenye mamlaka yote sawa sawa na marais wengine wote waliopita. Anapaswa kuunda serikali yake kwa kuteua baraza lake la mawaziri kama marais wengine waliopita.
Mambo marahisi unayafanya kuwa magumu- ukirithi kampuni hubadilishi hati ya usajili.
 
Majaliwa anatakiwa aonyeshe njia, anapaswa kujiuzuru ili kumpa nafasi mama Samia kuunda baraza lake la mawaziri.

Kitendo cha Majaliwa kung'ang'ania madaraka ni kitendo cha aibu kwa taifa..
Majaliwa hana kosa wala hana sababu za kukosa usingizi. Kama madame president hana guts za kumtumbua na kuvunja baraza, who is to blame? It is certainly not Majaliwa’s business

Ndio maana Bashiru na Majaliwa wanasema madame has no clue. Yeye anachojua ni kususasusa tuu na kufunga mitandio tu😊. Probably akasusa na kuresign before 2025
 
Kwani mwigulu Ni mwana sheria nguli tangu lini .Mwigulu Ni mchumi sio mwanasheria kabisa sijuagi Hawa mawaziri huteuliwa kwa kigezo gani kweli hebu wajuzi wa sheria nielewesheni please
 
Bwana Mbatia mimi ni kijana mdogo tu tena mtanzania mwenzako.
Mimi ninacho kielewa hao mawazili wote walioteuliwa kipindi cha awamu ya Magufuli, uteuzi ulifanyika na mama akiwemo. Sasa unataka ateue wengine wepi tena mkuu Mbatia. Ninachoelewa Makamu wa Rais huwa huwa anashauriana na Rais wakati wa kuteua.
 
Mama Samia S.H huyo Majaliwa baki nae atakufaa mbeleni, hao waliobaki ni uamuzi wako ila wafikirie kidogo hawa japo wana mapungufu ila wana Unafuu.

1.Jumaa Aweso - Waziri wa Maji

2.Suleiman Jafo - Tamisemi



The rest kula vichwa kadri utakavyoweza
 
Ni udhaifu mkubwa na aibu kufanya kazi na watu waliokula kiapo cha utii kwa serkali ya marehemu.
 
Sio vichwa vigumu bali ni wajuaji. Ndio maana ili utawale vyema ni muhimu kuwaziba midomo wapuuzi maana watakuyumbisha katika mission yako! Hiki ndio alikifanya Magufuli akaonekana katili ila dhamira ilikua njema kabisa.

Yani kuongoza Tanzania ni sawa na kufundisha darasa la wanafunzi 200 ukitarajia kutakuwa na hali ya utulivu na ustaarabu katika kuuliza maswali na majibu ila badala yake kila mtu ananong'ona na kuropoka ovyo bila utaratibu halafu kuadhibiwa hawataki.

Wana expect wafanyiwe ustaarabu ambao wao hawana, hao ndio watanzania bana.😁
Idiot
 
Katiba iko wazi kabisa, ni kwa wale wasioisoma au wale wanaoisoma kwa kupindishapindisha tu kwa ajili ya ajenda zao tu. Angalia, katiba yetu inasema hivi:
View attachment 1736040
View attachment 1736041
View attachment 1736043View attachment 1736044
View attachment 1736045

Angalia kifungu kidogo hicho cha (10) nilichowekea rangi, kuwa mtu atakayechukua madaraka ya urais ama kwa kurithi kutokana na kifungu kidogo cha (3) (yaani rais kuondolewa madarakani na baraza la mawaziri) hadi kifungu kidogo cha (5) (yaani rais akifariki), hana madaraka ya kuvunja Bunge au Baraza la mawaziri au kutengua teuzi za rais aliyekuwapo.
Hicho kifungu kinahusu kaimu Rais hataweza kufanya mabadiliko kwakuwa Rais bado yupo isipokuwa madaraka yake yanatekelezwa na mtu mwingine kwa muda.
 
Back
Top Bottom