Anaweza kufanya hivyo kama rais, lakini siyo kuwa kwa yeye kuapa tu, basi baraza lote lililokuwapo limekosa uhalali. Yeye ameingia hapo kuendeleza serikali iliyokuwapo madarakani baada ya kiongozi wake kufariki. Kwa mamlaka ya urais aliyo nayo sasa anaweza kubadilisha baraza lile kama ambavyo Rais aliyemrithi angefanya.
Tofauti ni kuwa kuna wengi wanaodai kuwa kifo cha Magufuli ni kifo cha serikali, na kuwa Samia lazima aanze na serikali mpya; hawatambui kuwa Samia karithi serikali ya Magufuli. Ni Yeye tu anayeweza kuibadili lakini siyo kuwa serikali hiyo imekufa. kama hamtaki majaliwa, basi anaweza kabisa kuvunja baraza la mawaziri na kuunda jipya kama ambavyo Magufuli angeweza kufanya wakati wa uhai wake.