Tofautisha kupinga na ujuaji, ondoa fundo la ujinga huo. Baba yako anapoweka utaratibu wa kuendesha nyumba yake ikasimama ni mfano halisi wa uongozi thabiti. Asingekuwa imara pengine ungepewa mimba ukiwa form 2 ukaishia kuteseka kimaisha tu.
Ni sababu ya ukali wake na msimamo ambao mlikuwa mnauita ukoloni ndio uliopelekea nidhamu yako kuwa kubwa katika maisha. Ndio maana leo umefikia mafanikio uliyo nayo na una uwezo wa kuja JF ata kuchapisha bandiko. Ni wazi kuwa unampenda sana baba yako au mama sababu ya guidance aliokupa tangu awali.
Heshima ni kitu cha bure tu na unapswa kujiheshimu ili uheshimiwe. Sasa majority ya wabongo wasio na nidhamu hili linawapa shida.