Zangu zipi jadili hoja usiwe na mihemko tulia soma ibara hiyo yote utaelewa maudhui yake imeelezea watakao kaimu nafasi Rais na namna ya makamu kuwa Rais kwa tafsiri yako maana yake mh Rais Samia hawezi tengua uteuzi wa waziri yoyote mpaka amalize 2025 ? Inaingia akilini?
Hujasoma ibara hiyo; ina vifungu vidogo 11; umevisoma vyote? Nitajiaraibu kukufafanulia kama ifuatavyo.
Ibara ya 37 inahusu utejkelezaji wa kazi na shughuli za Rais aliyeko madarakani
Kifungu kidogo cha (1) kinasema rais halazaimishwi kufuata maoni ya washauri; hiyo ikiwa ni pampoja na baraza la mawaziri.
Kifungu kidogo cha (2) kinasema rais anaweza kuondolewa madarakani na baraza la mawaziri.
Kifungu kidogo cha (3) kinaweka utaratibu wa kumpata rais mwingine iwapo baraza la mawaziri litaamua kumuondoa madarakani rais aliyepo
Kifungu kidogo cha (4) kinaweka utaratibu wa kumpata rais mwingine iwapo baraza la mawaziri litaamua kumuondoa madarakani rais aliyepo ambaye hakidhi matakwa ya kifungu kidogo cha tatu.
Kifungu kidogo cha (5) kinaweka utaratibu wa kumpata rais mwingine iwapo kiti hicho kitakuwa wazi kutokana na rais aliyekuwapo kufariki, kupoteza sifa za uraisi na sababu nyinginezo.
Kifungu kidogo cha (6) kinazuia kumuondoa madarakani prematurely rais aliyepo madarakani
Kifungu kidogo cha (7) kinazuia kinaweka utaratibu wa rais kumteua mtu mwingine kukaimu nafasi ya urasi wakati rais mwenyewe hawezi kuyatekeleza
Kifungu kidogo cha (8) kinazuia kinaweka utaratibu wa rais kudelegate sehemu ya madaraka yake kwa waziri yoyote na jinsi ya utekelezaji wa madaraka hayo
Kifungu kidogo cha (8) kinazuia kinaweka utaratibu wa rais kudelegate sehemu ya madaraka yake kwa waziri yoyote na jinsi ya utekelezaji wa madaraka hayo
Kifungu kidogo cha (9)
-hiki ni redundant- kinahalalisha maamuzi ya baraza la mawaziri kwenye kifungu kidogo cha (2) na vile vile kinasistiza kuwa kuwa kifungu kidogo cha (7) hakimwondoi madarakani rais aliyepo.
Kifungu kidogo cha (10) kinaweka ukomo wa mamlaka ya rais yeyote aliyepatikana kwa kupitia vifungu hivyo hapo juu kuhusu Bunge wateule walioachwa na rais aliyekuwapo.
Hiki ndicho kina matatizo sana, kwani kimeandikwa kuonyesha kuwa kuwa rais akishafariki, basi hata Bunge halitavunjwa tena ambavyo ni kupingana na sehemu nyingine za katiba!! Lakini kwa sasa ndivyo katiba yetu ilivyo!
Kifungu kidogo cha (11) kinasema kuwa iwapo mbunge wa kuchaguliwa akipata madaraka ya urais kupitia aya hii ya 37 (yaani kifungu kidogo chochote kuanzia cha (1) hadi (10)) hatapoteza sifa za ubunge.
Hivyo ndivyo katiba yetu ilivyo. Sasa wewe nionyeshe ni kifungu gani kinachoweka ukomo wa matumizi ya hicho kifungu kidogo cha (10) cha katiba!