James Mbatia amtaka Majaliwa ajiuzulu Uwaziri Mkuu

James Mbatia amtaka Majaliwa ajiuzulu Uwaziri Mkuu

acha kukwepesha kwani huyo mbatia katoa ni amri au ushauri
Katoa amri, kama mama suluhu tu anaomba watendaji wa taasisi na mamlaka wazingatie kanuni na sheria katika uwajibikaji yeye Mbatia anatoa amri kama nani?
 
Huo ni uchochezi sasa

Mwanasheria nguli Dr Mwigullu Nchemba alishatoa ufafanuzi!
😅😅😅😅! Wakati mwanasheria huyo nguli akifafanua hayo kikatiba, mwenzie Tabibu nguli Dr. Selemani Jafo alikuwa akitoa ratiba ya nyungu season 3 nchi nzima. Hii nchi ilichezewa sana awamu ya 5 au namsema uwongo ndugu zangu?!
 
Unatumia akiri gani wewe kasome vizuri acha upotoshaji.Uyu hakukaimu urais ni Rais full anatakiwa kupanga watu wa kufanya nao kazi.Rudia tena na tena uone kifungu icho kinamzungumzia nani?
Iwapo hujui kusoma post za JF ukazielewa kabla ya kuzikibu unaweza kusoma katiba ukaielewa kweli?
 
Kabisa ili mama aongoze nchi bila kufunikwa na kivuli cha Magufuli, inabidi avunje hilo baraza haraka. Ma hata hao mawaziri hilo wanalijua, lakini wanalazimisha kuwepo ili kumtisha huyo mama asiwaguse. Na kwenye kuunda baraza lake ahakishe Majaliwa, Kabudi, Mwigulu na Jafo wasiwepo. Wale wate waliokuwa wanajipendekeza wazi wazi kwa Magufuli awapige chini haraka maana ndio watamkwamisha. Hao waliokuwa mawaziri wa wizara nyingine, awageuze kuwa manaibu mawaziri.

mnawaogopa hao wakali , manataka mumpelekeshe mama
 
Mzee wa "mama Tanzania" anazeeka vibaya! Atuoneshe mfano yeye ajiuzulu uenyekiti Nccr mana Hanna afanyalo enzi za mtaala alitishia kujiuzulu lkn wapi
 
Mhe:Rais Mama yetu Samia Suluhu Hassan chondechonde vunja baraza lote la mawaziri. Teua wachapa kazi na Waape kiapo cha utii mbele yako. Pia nakupongeza kwa uteuzi wa Dr. Philip Isdory Mpango kuwa Makamu wa Rais. Pia nakupongeza kwa kuanza vizuri na ATCL, TPA na BOT/HAZINA.

Tembea zaidi TAMISEMI, TRA, LOAN BOARD (HESLB), Mpe msimamo Speaker wa Bunge Job Ndugai wito wa kuwaondoa Wabunge hewa19, Fanya Special Auditing ya Miradi mikubwa ya JPM hata Ubungo Interchange, Busisi Bridge, Nyerere Hydro Power Project, na mwisho toa Ajira mpya.

Mungu akulinde na akuongoze Mama. Kila la Kheri.
 
Hatutaki mitano tena system wala maendeleo hayana chama system.

Sisi tunajua maendeleo ni magumu sana kuyafikia ila tunahitaji WAJIBU, HAKI, USAWA NA SHERIA iwe ndiyo dira yetu.

Vunja baraza lote na fyekelea mbali wapuliza zumari wote akina maderu...magamba.....gwajigirl...usimsahau na mla fia na njoge Kakuru.
 
Yes ofcourse, kwa nature ya watanzania wanatakiwa kuongozwa kama mifugo sababu ustaarabu ni kipengele kwao. Awe na elimu asiwe nayo wana asili ya ujuaji sana ndugu zetu hawa.
Punda Hawendi ila kwa Magongo ndio waleee. Nataka mama Samia ukimpa adhabu mtu usimwangalie machoni mpe kama humjui vile hawa watu ni vichwa ngumu sana so wape adhabu ya kijapani SAMURAI mwambie kisu hicho hapo jiue mwenyewe.
 
Baada ya Mh. Rais Samia kumteua Bw. Mpango aliyekuwa waziri wa fedha katika serikali ya Magufuli ni vema ukaonyesha mfano kwa wewe na Baraza zima la mawaziri mkajiuzulu ili kumpa Rais Samia wigo mpana zaidi wa kuunda serikali yake. Sasa hivi mnamlazimisha Mh. Rais kuziba kiraka cha Mpango katika wizara ya fedha tu na ninyi kubaki katika nafasi zenu.

Kujiuzulu kwako haina maana hawezi kukuteua tena bali ni kulinda heshima yako na ukiteuliwa tena itakupa wewe uhalali wa kufanya kazi zako kwa uhuru zaidi. Kuendelea kung'ang'ania hiyo nafasi kunaweza kusababisha ukaondolewa kwa fedheha.
 
Back
Top Bottom