James Mbatia amtaka Majaliwa ajiuzulu Uwaziri Mkuu

James Mbatia amtaka Majaliwa ajiuzulu Uwaziri Mkuu

ha ha haa

Mbona president anayo mamlaka ya kuvunja Baraza?

Hapa Mbatia anataka tuone Rais na Waziri mkuu Wana mgogoro. Kwamba Rais anashindwa kuunda Baraza jipya kwa vile Waziri Mkuu Majaliwa hajajiuzuru.

Wapi Kikwete, za kuambiwa tuchanganye na zetu.
Ameshauri Majaliwa atumie busara kujiuzulu

Sent from my MRD-LX1F using JamiiForums mobile app
 
Hakuna sababu ya kujiuzulu. Wala kuvunja Baraza maana Wakishiriki kuliunda.
 
Wacha watibuane wanajuana vizuri mradi waachie masalia ili maisha yasogee.
 
Katiba na sheria vinasemaje? Nilitegemea Mbatia angeshuka na kifungu cha sheria sio blablaa.
 
Kama hataki rais avunje baraza la mawaziri ili ateue wake na katiba Katiba iongezewe kifungu kinacho mtaka rais akiapishwa aunde upya baraza la mawaziri,kuondoa Utara uliojitokeza WA kulinda ugali wao Kama alivyofanya Madelu.
 
Katiba iko wazi kabisa, ni kwa wale wasioisoma au wale wanaoisoma kwa kupindishapindisha tu kwa ajili ya ajenda zao tu. Angalia, katiba yetu inasema hivi:
View attachment 1736040
View attachment 1736041
View attachment 1736043View attachment 1736044
View attachment 1736045

Angalia kifungu kidogo hicho cha (10) nilichowekea rangi, kuwa mtu atakayechukua madaraka ya urais ama kwa kurithi kutokana na kifungu kidogo cha (3) (yaani rais kuondolewa madarakani na baraza la mawaziri) hadi kifungu kidogo cha (5) (yaani rais akifariki), hana madaraka ya kuvunja Bunge au Baraza la mawaziri au kutengua teuzi za rais aliyekuwapo.
Unatumia akiri gani wewe kasome vizuri acha upotoshaji.Uyu hakukaimu urais ni Rais full anatakiwa kupanga watu wa kufanya nao kazi.Rudia tena na tena uone kifungu icho kinamzungumzia nani?
 
Watu wanamuogopa sana waziri mkuu wetu Majaliwa kwasabababu ni mchapakazi hodari, sasa wanataka mama Samia hasiwe na nguvu ili wampelekeshe wapendavyo, mimi namwomba huyu mama hawe mkali na mwenye msimamo.
Sema ni mpigaji anachapa kazi ipi? Anafanya chini ya kiboko bila kiboko hawezi.
 
Naona umetumwa rasmi kuja kumtetea huyo bosi wako. Ila sidhani kama itasaidia! Hata kama ataachwa kwenye hiyo nafasi, ukweli utabakia palepale!

Ameshapoteza mvuto kwa jamii ya wapenda haki na ukweli kutokana na vitendo vyake vya kupenda kusema uongo na kuwadanganya watu wazima kama watoto.
Wewe ni mtu mzima kumbe?
 
Huko Mimi sikutaka kujadili nilisimamia hapo kwamba hawezi fanya mabadiliko kwakuwa amezuiwa na vifungu sasa tupo pamoja shida ulihamaki hapa ni kupeana elimu na ufahamu

Tusaidiene majibu Rais mteule ni yupi? Na je mara Rais alipofariki katiba ilimteua makamu kuwa Rais lakini hakuweza kushika mpaka kiapo je hapo katika masaa anasubiri kuapishwa sio Rais mteule kidhana ? Nawaza tu
Anakuwa mteule kwasababu ya Katiba ila kuna mafumbo mengi Nyerere aliyaweka KATIBA MPYA NI LAZIMA.
 
Unatumia akiri gani wewe kasome vizuri acha upotoshaji.Uyu hakukaimu urais ni Rais full anatakiwa kupanga watu wa kufanya nao kazi.Rudia tena na tena uone kifungu icho kinamzungumzia nani?
Onyesha kifungu cha katiba kama alivyoonesha mwenzako hapo juu.
 
Na kwa mihemko hii ndio maana mnaigawa nchi, kwanza hakuna hicho ulichokiita "mission yako" katika nchi. Ni kukosa utashi wa kiuongozi pale unapotegemea kati ya waTz 61M kusema ndio kwa kila utakachokisema bila kuwepo wa kukupinga kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

Kama mnajijua hamna utashi huo wa kiuongozi basi bakini makwenu muongoze familia zenu hakuna atakayekuja kuwahoji, msije huku halafu mkipingwa mnaanza kulia lia na kunyamazisha watu kwa mabavu, tuko karne ya 21.

Watu kama nyie mngekuwepo kupindi cha biashara ya utumwa na ukoloni mpaka leo tungekuwa hatujapata uhuru. Kupingwa kupo tangu enzi za mitume, mje kwenye uongozi mkiwa mmejiandaa na hilo, kinyume na hapo bakini huko hakuna mtu anayeombwa kuja kugombea, ni mambo yenu binafsi tu ndio yanayowasukuma kutafuta uongozi kwa damu na machozi.
Mkuu umeongea kwa hisia kali lakini ndio ukweli wenyewe.
 
Waziri Mkuu kaa pembeni.. Mama aanze upya.
CCM ni ileile aisee..
 
Watu kwa kuharibu ugali wa wenzio hawajambo...

Binadamu tuna chuki + wivu balaa
 
Ndio maana ili utawale vyema ni muhimu kuwaziba midomo wapuuzi maana watakuyumbisha katika mission yako! Hiki ndio alikifanya Magufuli akaonekana katili ila dhamira ilikua njema kabisa.

Yani kuongoza Tanzania ni sawa na kufundisha darasa la wanafunzi 200 ukitarajia kutakuwa na hali ya utulivu na ustaarabu katika kuuliza maswali na majibu ila badala yake kila mtu ananong'ona na kuropoka ovyo bila utaratibu halafu kuadhibiwa hawataki.

Wana expect wafanyiwe ustaarabu ambao wao hawana, hao ndio watanzania bana.[emoji16]

Hahahahha..hakika Mkuu,ukifuatilia maneno ya watu hutoboi
 
Sio vichwa vigumu bali ni wajuaji. Ndio maana ili utawale vyema ni muhimu kuwaziba midomo wapuuzi maana watakuyumbisha katika mission yako! Hiki ndio alikifanya Magufuli akaonekana katili ila dhamira ilikua njema kabisa.

Yani kuongoza Tanzania ni sawa na kufundisha darasa la wanafunzi 200 ukitarajia kutakuwa na hali ya utulivu na ustaarabu katika kuuliza maswali na majibu ila badala yake kila mtu ananong'ona na kuropoka ovyo bila utaratibu halafu kuadhibiwa hawataki.

Wana expect wafanyiwe ustaarabu ambao wao hawana, hao ndio watanzania bana.[emoji16]
[emoji38][emoji38][emoji38]hatari tupu
 
Back
Top Bottom