James Mbatia amtaka Majaliwa ajiuzulu Uwaziri Mkuu

James Mbatia amtaka Majaliwa ajiuzulu Uwaziri Mkuu

Hata wewe ukioa mwanamke akaja na watoto kutoka ndoa yake ya huko unaanza kuzaa nae wa kwako Hausemi ohh mtoto ni mtoto hapana.Unaweka mimba zako unaanza wako.

MAMA SAMIA kwasasa atapanga serikali yake mwenyewe.
 
Tutamkumbuka sana yule mzee hata kama sio HADHARANI basi NAFSI zetu zitatusuta I SWEAR

Hivi kaka unaweza kuniambia watanzania wanataka nini ? SIJAJUA nini kimelikumba Taifa hili Mimi sijui kwa kweli
Naona tuna ambaa ambaa tuu
Utamkumbuka wewe na familia yako,mm sina cha kumkumbuka asilani
 
Hata kama atajiuzuru tegemea kurudishwa kwenye wadhifa wa waziri mkuu
 
Afu kama ni kutakiwa kujiuzuru walitakiwa watu wengi Sana kipindi cha Jiwe na wakamtaka Rais awafute Kazi ndio akajibu yeye hapangiwi kwa hiyo hakuna shida kwa Mbatia kutoa maoni

Sio mara ya kwanza huyu PM kutakuwa kujiuzuru tangu kipindi kile cha mashangazi,sema ishu ya kujiuzuru bongo ni ngumu na hawezi unless Rais ndio amtake kufanya hivyo maana bongo madaraka ni ulaji sio kutumikia watu
 
Tofautisha kupinga na ujuaji, ondoa fundo la ujinga huo. Baba yako anapoweka utaratibu wa kuendesha nyumba yake ikasimama ni mfano halisi wa uongozi thabiti. Asingekuwa imara pengine ungepewa mimba ukiwa form 2 ukaishia kuteseka kimaisha tu.

Ni sababu ya ukali wake na msimamo ambao mlikuwa mnauita ukoloni ndio uliopelekea nidhamu yako kuwa kubwa katika maisha. Ndio maana leo umefikia mafanikio uliyo nayo na una uwezo wa kuja JF ata kuchapisha bandiko. Ni wazi kuwa unampenda sana baba yako au mama sababu ya guidance aliokupa tangu awali.

Heshima ni kitu cha bure tu na unapswa kujiheshimu ili uheshimiwe. Sasa majority ya wabongo wasio na nidhamu hili linawapa shida.
acha kukwepesha kwani huyo mbatia katoa ni amri au ushauri
 
Katiba iko wazi kabisa, ni kwa wale wasioisoma au wale wanaoisoma kwa kupindishapindisha tu kwa ajili ya ajenda zao tu. Angalia, katiba yetu inasema hivi:
View attachment 1736040
View attachment 1736041
View attachment 1736043View attachment 1736044
View attachment 1736045

Angalia kifungu kidogo hicho cha (10) nilichowekea rangi, kuwa mtu atakayechukua madaraka ya urais ama kwa kurithi kutokana na kifungu kidogo cha (3) (yaani rais kuondolewa madarakani na baraza la mawaziri) hadi kifungu kidogo cha (5) (yaani rais akifariki), hana madaraka ya kuvunja Bunge au Baraza la mawaziri au kutengua teuzi za rais aliyekuwapo.
Katiba haitafsiriwi tuu kwa muktadha wa kifungu hicho kimoja ulichokichagua.

Kama ni hivyo mkuu inamaana Rais atakuwa anawaogopa mawaziri na hawezi kuwawajibisha kitu ambacho hakina mantiki
 
Watu wanamuogopa sana waziri mkuu wetu Majaliwa kwasabababu ni mchapakazi hodari, sasa wanataka mama Samia hasiwe na nguvu ili wampelekeshe wapendavyo, mimi namwomba huyu mama hawe mkali na mwenye msimamo.
Nchi hii mchapakazi ni Majaliwa tuu? Kwani Rais sio mchapakazi?

Nani ana rekodi nzuri ya utendaji Serikalini Kati ya Rais na PM kwa serikali zote zilizopita?
 
Majaliwa anatakiwa aonyeshe njia, anapaswa kujiuzuru ili kumpa nafasi mama Samia kuunda baraza lake la mawaziri.

Kitendo cha Majaliwa kung'ang'ania madaraka ni kitendo cha aibu kwa taifa na kinaweza kutoa ishara kuwa huenda Majaliwa ni mmoja ya wahusika wa lile genge lililohisiwa kuwa linataka kumpora mama madaraka ya kiti cha urais.

Majaliwa onyesha njia sasa.
Jiuzuru haraka iwezekanavyo.
Mimi nadhani tunamuonea bure Waziri Mkuu, hivi Kwa situation kama Ile angejiuzuru saa ngapi?.. wakati yeye ndiye Mwenyekiti wa kamati ya Mazishi/maafa ya Kitaifa?.. nadhani tumpe muda Bunge lirejee na yeye atafanya ustaarabu huo ili kumpa Rais nafasi ya kuteua cabinet yake na uenda akateuliwa yeye tena Kwa mara ya Tati ili kumpa confidence ya Rais. Tukumbuke kwamba hakuna scandal iliyothibitishwa ambayo imetokea Chini ya usimamizi wake inayotutaka tumlazimishe ajiuzulu mara moja popote alipo..PM alipigiwa Kura na wabunge wenzake basi tumpe japo heshima ya kujiuzuru mbele yao na si vichochoroni kama wengi wetu tunavyotaka.
 
Mambo marahisi unayafanya kuwa magumu- ukirithi kampuni hubadilishi hati ya usajili.

Akili yako kiazi sana, nchi na kampuni wapi na wapi.
Afu Rais lazima uwe controversial na uonyeshe utiisho Ili ukikohoa watu waitike naam mheshimiwa Rais.

Akiwaacha hao watakuwa na kiburi
 
Katiba haitafsiriwi tuu kwa muktadha wa kifungu hicho kimoja ulichokichagua.

Kama ni hivyo mkuu inamaana Rais atakuwa anawaogopa mawaziri na hawezi kuwawajibisha kitu ambacho hakina mantiki
Inawezekanma hutambui kuwa serikali yetu ni ya Jamhuri, siyo ya kifalme. Kwa hiyo mtu kuwa rais, haina maana kuwa mawaziri ni wtumishi wake, bali mawaziri ni sehemu ya serikali anayoongoza.
 
Itapendeza kama rais ataunda baraza lake la mawazir na kula kiapo cha utiifu mbele yake badal a ya kufanya kazi na barazq ambalo hajalichagua yy
 
Majaliwa anatakiwa aonyeshe njia, anapaswa kujiuzuru ili kumpa nafasi mama Samia kuunda baraza lake la mawaziri.

Kitendo cha Majaliwa kung'ang'ania madaraka ni kitendo cha aibu kwa taifa na kinaweza kutoa ishara kuwa huenda Majaliwa ni mmoja ya wahusika wa lile genge lililohisiwa kuwa linataka kumpora mama madaraka ya kiti cha urais.

Majaliwa onyesha njia sasa.
Jiuzuru haraka iwezekanavyo.
Ni siku tu baba akifa kwenye familia tutasema watoto, wauliwe wote mama azae wengine ili aweze kuwatunza na kuvontrol hao watoto wapya....

Basi kama ni hivo sio baraza la mawaziri tu, wakuu wa mikoa na wilaya, ded, katibu tawala, wakuu wa taasisi zote waondolewe halafu mama aweke wengine. Is it that simple. Wakati mwingine hakikisho la kazi huongeza uwajibikaji na kujituma otherwise unataka mama aanze kujitengenezea maadui mapema tena bila sababu za msingi.

Vijana chapeni kazi
 
Rais Samia kwa hali ya kawaida tuu inabidi avunje baraza kwani kutokuvunja hatapata ajiandae kufanyakazi na wasaidizi wasiokuwa na utii usiotukuka juu yake na taifa kwa ujumla.
Unahitajika makini kwa hili lasivyo uongozi wake utakuwa na changamoto ya kiuongozi ni muhimu azingatie ili apate utii kwa atakao waapisha.
 
Ni heshima kufanya hivyo, unapokuwa kiongozi ni wajibu kuonesha njia.
Mh. Waziri Mkuu akijiuzuru na baadae kuteuliwa atakuwa amezaliwa upya na kuonesha nidhamu na heshima kwa Mkuu wa Nchi mpya.
Mh.Kasimu Majariwa Mb.jiuzuru you can become One of the icon na nyota yako itang'aala tofauti na sasa.
Umesahau la Lowasa
 
Majaliwa anatakiwa aonyeshe njia, anapaswa kujiuzuru ili kumpa nafasi mama Samia kuunda baraza lake la mawaziri.

Kitendo cha Majaliwa kung'ang'ania madaraka ni kitendo cha aibu kwa taifa na kinaweza kutoa ishara kuwa huenda Majaliwa ni mmoja ya wahusika wa lile genge lililohisiwa kuwa linataka kumpora mama madaraka ya kiti cha urais.

Majaliwa onyesha njia sasa.
Jiuzuru haraka iwezekanavyo.
Uzuri wa kuijuzuru mwenyewe kuna heshima zake kuliko kuvuliwa
 
Mbona mnamlazimisha sana wazee, mnataka mama abaki pekeake ili mumpelekeshe jinsi mnavyojiskia 😁😁😁!!?

Sasa kwa taarifa yenu atajiuzulu kisha atateuliwa upya acheni utoto!
Kabisa, watu wanataka ccm wavurugane, hapo sasa..
 
Back
Top Bottom