James Mbatia amtaka Majaliwa ajiuzulu Uwaziri Mkuu

James Mbatia amtaka Majaliwa ajiuzulu Uwaziri Mkuu

Rais Mpya atatushangaza Watanzania na dunia kwa ujumla iwapo ataendelea kufanya kazi na Baraza la Mawaziri ambalo hakuliapisha yeye kama Rais!
Baraza lile liliapa kumtii na kumsaidia rais mwingine mwenye personality, mtazamo, muonekano, sababu na malengo ya kuwateua na haiba tofauti kabisa na Rais Samia. Kama atapenda aendelee nao hawa mawaziri wa JPM lazima awateue upya na awaapishe yeye upya kuwa watamtii yeye rais, katiba na muungano hadharani mbele ya umma.
 
Mbona mnamlazimisha sana wazee, mnataka mama abaki pekeake ili mumpelekeshe jinsi mnavyojiskia 😁😁😁!!?

Sasa kwa taarifa yenu atajiuzulu kisha atateuliwa upya acheni utoto!
Kumbukeni Mzee majaliwa alihakikisha kuwa anapita bila kupingwa kwenye jimbo lake na hakuna wapinzani waliothubutu kwenda kupiga kampeni jimboni kwake Luwangwa. Huyu anaweza kuwa mbaya sana kwa demokrasia kuliko hata JPM.
 
Kwahiyo mnataka nijiuzuru ili nikose kupigiwa Vigeregere na akina Mama si ndio??. Sasa mshanitibua, hapa sijiuzuru na Waziri wa Afya Mama Gwajima naye atafuata mfano wangu..
HANG'ATUKI MTU HAPA...Tumbo halijashiba bado.
 
Kwani JF haina nguli wa sheria watutoe tongotongo?
 
Safii
Hata ukivaa viatu vya Serikali unaona kabisa Wakati mwengine inawabidi wawe wakatili ili Mambo yaende

Maskini Nchi yangu
Una maanisha kuua? Si sawa kbs haiitaji kuwa katili serkali ili mambo yaende. Inahitaji ueledi basi.
 
Mama Samia kazi anayo hii nchi ina watu vichwa ngumu!
Hii nchi inawajuaji wengi sana, kuna wengine utakuta hawajui chochote ila wanataka waishauri serikali[emoji28].Samia akitaka aiweze hii nchi, azibe kabisa masikio Ili afanye mambo kwa kadri awezavyo. Akisema asubiri ushauri wa Kila mtu atachelewa sana kufika.
 
Majaliwa anatakiwa aonyeshe njia, anapaswa kujiuzuru ili kumpa nafasi mama Samia kuunda baraza lake la mawaziri.

Kitendo cha Majaliwa kung'ang'ania madaraka ni kitendo cha aibu kwa taifa na kinaweza kutoa ishara kuwa huenda Majaliwa ni mmoja ya wahusika wa lile genge lililohisiwa kuwa linataka kumpora mama madaraka ya kiti cha urais.

Majaliwa onyesha njia sasa.
Jiuzuru haraka iwezekanavyo.
Wewe unashauri kama nani, hapa nchini? [emoji28]

Nilichogundua mimi ni kwamba, watu wanamuogopa sana Majaliwa. Wanafikiri ataingia na ile kasi ialiyowahi kuanza nayo kipindi kile kabla hajazuiliwa na mzee baba.
 
Kati ya ushauri wenye hekima, huu ni mmojawapo.

Waziri Mkuu ampe uhuru usio na ukakasi Mh. Rais mpya, wa kuweza kuunda Serikali yake bila ya kuleta hisia kuwa amemfukuza Waziri Mkuu au Waziri fulani.

Rais ana mamlaka ya kuvunja baraza la Mawaziri lakini kiungwana, Waziri Mkuu akijiuzulu, ni hekima zaidi. Mh. Rais atafanya uteuzi wa Waziri Mkuu, na kisha kuanza na Serikali mpya.

Kuna watu wana fikra hasi. Wanataka kusema kuwa Serikali ya Mh. Rais Samia ni mwendelezo wa Serikali ya Hayati Magufuli, jambo ambalo, kikatiba, siyo kweli. Hii ni Serikali mpya ambayo imepatikana kikatiba kutokana na sababu ambazo zimelazimisha Serikali ya Hayati Magufuli kutomaliza muhula wake wa kikatiba.

Waziri Mkuu na Mawaziri wote wanatakiwa kula kiapo cha utii kwa Mh. Rais. Hawa waliopo waliapa lini kumtii Rais Samia?
 
Majaliwa anatakiwa aonyeshe njia, anapaswa kujiuzuru ili kumpa nafasi mama Samia kuunda baraza lake la mawaziri.

Kitendo cha Majaliwa kung'ang'ania madaraka ni kitendo cha aibu kwa taifa na kinaweza kutoa ishara kuwa huenda Majaliwa ni mmoja ya wahusika wa lile genge lililohisiwa kuwa linataka kumpora mama madaraka ya kiti cha urais.

Majaliwa onyesha njia sasa.
Jiuzuru haraka iwezekanavyo.
Acha kuropoka wewe
 
Kwahiyo mnataka nijiuzuru ili nikose kupigiwa Vigeregere na akina Mama si ndio??. Sasa mshanitibua, hapa sijiuzuru na Waziri wa Afya Mama Gwajima naye atafuata mfano wangu..
HANG'ATUKI MTU HAPA...Tumbo halijashiba bado.
Yule gwajima wa malimao na pilipili kichaa?
 
Atakushangaza wewe na watu wa caliber yako, sio Watanzania.
Naona umetumwa rasmi kuja kumtetea huyo bosi wako. Ila sidhani kama itasaidia! Hata kama ataachwa kwenye hiyo nafasi, ukweli utabakia palepale!

Ameshapoteza mvuto kwa jamii ya wapenda haki na ukweli kutokana na vitendo vyake vya kupenda kusema uongo na kuwadanganya watu wazima kama watoto.
 
Wazir mkuu anavyoteuliwa yanakuwa ni makubaliano Kati ya Rais na Makamu wake kuwa ni nan tumteue
 
Majaliwa anatakiwa aonyeshe njia, anapaswa kujiuzuru ili kumpa nafasi mama Samia kuunda baraza lake la mawaziri.

Kitendo cha Majaliwa kung'ang'ania madaraka ni kitendo cha aibu kwa taifa na kinaweza kutoa ishara kuwa huenda Majaliwa ni mmoja ya wahusika wa lile genge lililohisiwa kuwa linataka kumpora mama madaraka ya kiti cha urais.

Majaliwa onyesha njia sasa.
Jiuzuru haraka iwezekanavyo.

Yaani kirahisi rahisi tu ajiuzulu?

Na vile ving'ora amwachie nani?

Kwanza hana Uhakika kama Mama atamrudisha tena kwenye U-PM.. Kwa hiyo kuliko ajitege mwenyewe ameona bora aendelee kumtega Mama..
 
Back
Top Bottom