Kati ya ushauri wenye hekima, huu ni mmojawapo.
Waziri Mkuu ampe uhuru usio na ukakasi Mh. Rais mpya, wa kuweza kuunda Serikali yake bila ya kuleta hisia kuwa amemfukuza Waziri Mkuu au Waziri fulani.
Rais ana mamlaka ya kuvunja baraza la Mawaziri lakini kiungwana, Waziri Mkuu akijiuzulu, ni hekima zaidi. Mh. Rais atafanya uteuzi wa Waziri Mkuu, na kisha kuanza na Serikali mpya.
Kuna watu wana fikra hasi. Wanataka kusema kuwa Serikali ya Mh. Rais Samia ni mwendelezo wa Serikali ya Hayati Magufuli, jambo ambalo, kikatiba, siyo kweli. Hii ni Serikali mpya ambayo imepatikana kikatiba kutokana na sababu ambazo zimelazimisha Serikali ya Hayati Magufuli kutomaliza muhula wake wa kikatiba.
Waziri Mkuu na Mawaziri wote wanatakiwa kula kiapo cha utii kwa Mh. Rais. Hawa waliopo waliapa lini kumtii Rais Samia?