Na kwa mihemko hii ndio maana mnaigawa nchi, kwanza hakuna hicho ulichokiita "mission yako" katika nchi. Ni kukosa utashi wa kiuongozi pale unapotegemea kati ya waTz 61M kusema ndio kwa kila utakachokisema bila kuwepo wa kukupinga kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.
Kama mnajijua hamna utashi huo wa kiuongozi basi bakini makwenu muongoze familia zenu hakuna atakayekuja kuwahoji, msije huku halafu mkipingwa mnaanza kulia lia na kunyamazisha watu kwa mabavu, tuko karne ya 21.
Watu kama nyie mngekuwepo kupindi cha biashara ya utumwa na ukoloni mpaka leo tungekuwa hatujapata uhuru. Kupingwa kupo tangu enzi za mitume, mje kwenye uongozi mkiwa mmejiandaa na hilo, kinyume na hapo bakini huko hakuna mtu anayeombwa kuja kugombea, ni mambo yenu binafsi tu ndio yanayowasukuma kutafuta uongozi kwa damu na machozi.