James Rugemalira aachiwa huru, DPP hana nia ya kuendelea na mashtaka

[emoji419][emoji419][emoji1787][emoji23]
 
wakati wa sakata maarufu kama escrow ambalo liliwapatia hawa ndugu zetu mabilioni..kulikuwa na pande mbili zikibishana.
upande wa kwa kwanza ulikuwa wa serikali ukiongozwa na aliyekuwa kiongozi mkuu wa serikali waliosema "hiyo pesa siyo ya umma"
upande wa pili ulikuwa wa wabunge wengi wa kipindi hicho wakati Bunge likiwa bado Bunge la wananchi likiongozwa na mama semamba na baadhi ya viongozi wa serikali...hawa walisema " pesa hizo ni za umma"
mabishano hayo yaliendelea kwa kipindi kirefu sana..hata hivo waliokuwa wanasema pesa si ya umma walikuwa wanaongoza serikali,basi watuhumiwa hawakufanywa kitu chochote
Baada ya muda,baadhi ya waliokuwa wanaamini kuwa pesa ile ni ya umma,wakashika madaraka 2015, wakawatia ndani watuhumiwa kutokana na imani waliyokuwa nayo kuwa pesa ni ya umma
kwa bahati nzuri kwa watuhumiwa,baadhi ya wale walioamini kuwa pesa ni ya umma, hawapo tena madarakani, madaraka yamerudi kwa wale walioamini kuwa pesa si ya umma,hapo lazima huyo DPP aagizwe asiendelee na kesi.
tusubiri watakapoingia madarakani wale wa imani ile nyingine,labda DPP ataagizwa tena aone sababu ya kuendelea na kesi
Lakini hata hivo mjadala unapaswa kuanza tena kuwa ile pesa ilikuwa ya umma au siyo ya umma, na wala siyo kuimba wimbo wa DPP ambao tunaamini ameagizwa aimbe walau kwa sasa
 
Reactions: Qwy
Fair analysis.
 
Kwa nini hakuyafunga wakati wake? Miaka minne alikuwa anasubiri nini hadi akafa?
Watanzania hatuna jema
Yule aliyepinga wizi leo majizi yanaachiwa tu.
Hakuna anayejali.
Tz ni kichwa cha mwenda wazimu, maendeleo tutabaki kuyasikia tu.
 
Unajua shida ni kuwa sisi ndio tulitaka waliohusika wawajibishwe.
Na kufanya hivyo kikwete alimfuta uwaziri mama tibaijuka.
Anyway, nilichoona wengi hatupo serious. Hii itapelekea nchi kuendelea kuibiwa maana wanajua hakutakuwa na kesi Wala kufungwa
Huwezi kumuwajibisha mtu bila ushahidi na ndio maana Sethi na Ruge wamekaa miaka minne mahabusu bila kufungwa. Kama ushahidi ungekuwepo kwa namna jiwe alivyokuwa amewapania wangekuwa wameshapewa hukumu zao muda mrefu sana.
 
Tibaijuka aliwajibishwa kwa sababu mtumishi wa umma hasa kwenye ngazi ya uwaziri anayehusika katika kumshauri Rais, kutunga sera na kufanya maamuzi makubwa kuna taratibu zake za kupokea na kuripoti zawadi kutoka kwa watu/mashirika/kampuni binafsi ili kuondoa migongano ya maslahi.

Tibaijuka hakuwajibishwa kwa sababu amehusika na wizi bali kwa sababu ya taswira mbaya ya kisiasa, na pia alifanywa kama mbuzi wa kafara tu kwa ajili ya kuzuia kelele zisiendelee.
 
Wizi wa Escrow haukuwa katika pesa kutoka bali ulisukwa kitaalamu kwenye mikataba ya IPTL na Tanesco na migogoro kati yao.
 
Kama Miaka minne wameshindwa kupata ushahidi wa kutosha kuwafunga Sethi na Ruge unafikiri walihitaji miaka mingapi zaidi?

Chadema hawataki huo mtindo wa kuwa na makosa yasiyo na dhamana, wanataka makosa yote yawe na dhamana.
 
Besti kufa kufaana. Ila najiuliza Jiwe alishindwa kweli kumpora hela zake hadi yeye akubali? Kama TRA tu walipora hela st jude account bila ridhaa yao Jiwe angeshindwa kwa rugee kweli?
Labda pesa zake alizificha huko kwenye akaunti za nje ya nchi.
 
Tupate katiba mpya.
 
Huo ndio ukweriii ndugu zangu
 
Wewe kilaza, Zitto, Kafulila, Lissu na CAG ndio waliomuambia DPP awakamate Sethi na Ruge? Mbona basi hawakukamatwa enzi za JK wakaja kukamatwa na kuwekwa gerezani bila hukumu enzi za utawala wa giza wa jiwe?
 
Mwambieni huku nje kuna hukumu ya COVID-19.

Asifanye mzaha, hukumu hiyo haitenguliwi na yeyote.

Tanzania imekuwa nchi ya kuoneana kwelikweli, sijui tutafika wapi na hali ya namna hii!
Gerezani ndio ilikuwa mahali rahisi zaidi kwake kupata hukumu ya COVID-19, huku nje ataagiza Chanjo ya Moderna kutoka US dk 0
 
Huu ni ukweli mchungu wengi hawataki kuuona, kuusikia au wamesahau.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…