James Sinclair: A Friend or Foe?

James Sinclair: A Friend or Foe?

Pia nadhani uhusiano wa USA na CANADA uliyumba mara baada ya Kuyumba kwa NAFTA.
 
hii (ishu ya madini) inaweza fanana na issue ya LLOLIONDO kama haitapatiwa ufumbuzi.
WANYAMA wamekuwa wakibebwa kupelekwa UARABUNI kutokana na mikataba isiyonufaisha TANZANIA. sasa wanyama ambao walikuwa wanapatikana TZ sasa wanapatikana UARABUNI . na hawaji kuangalia wanyama mbugani kwetu bali kwenda kuangalia wanyama uarabuni tena jangwani (zoo)
MADINI YETU JAMANI....... VIZAZI VIJAVYO VITASEMA NINI JUU YETU....? HUENDA HATA CHIF MANGUNGO KUNA WATU WALIMWAMBIA, NA SISI TUNAJUA KUSOMA NA KUANDIKA TUTAWAAMBIA NINI WAJUKUU WETU...? TUMEUZA WANYAMA NA SASA MADINI......!
MAPENDEKEZO YA RIPOTI YAZINGATIWE.....!
 
hii (ishu ya madini) inaweza fanana na issue ya LLOLIONDO kama haitapatiwa ufumbuzi.
WANYAMA wamekuwa wakibebwa kupelekwa UARABUNI kutokana na mikataba isiyonufaisha TANZANIA. sasa wanyama ambao walikuwa wanapatikana TZ sasa wanapatikana UARABUNI . na hawaji kuangalia wanyama mbugani kwetu bali kwenda kuangalia wanyama uarabuni tena jangwani (zoo)
MADINI YETU JAMANI....... VIZAZI VIJAVYO VITASEMA NINI JUU YETU....? HUENDA HATA CHIF MANGUNGO KUNA WATU WALIMWAMBIA, NA SISI TUNAJUA KUSOMA NA KUANDIKA TUTAWAAMBIA NINI WAJUKUU WETU...? TUMEUZA WANYAMA NA SASA MADINI......!
MAPENDEKEZO YA RIPOTI YAZINGATIWE.....!

Ni muhimu sana tukaipata ripoti ya madini.

Tumepiga kelele vya kutosha na ile thread ya countdown ya madini imejifilia zake mara baada ya kubadilika na kuwa hatimaye JK akabidhiwa ripoti ya madini.

Sasa nimeonelea nili approach hili swala in a different angle!

Kwamba sasa ni kweli tulikuwa na askari wetu ndani ya kamati ya madini.

Tunajuwa pia kulikuwa na MAFISADI ndani ya kamati hiyo!

Tunajuwa pia nini misimamo ya baadhi ya wjaumbe hao wa kamati kabla na mara baada ya kuteuliwa kamatini.

Hivyo basi tunajuwa mgogogoro uko kwa wanakamati,wananchi,wabunge,na Mh Rais.

Tunajuwa kuwa Sinclair alipewa ripoti kabla yetu na yeye akadai kuwa uamuzi wa Kikwete ndio wa mwisho! Ni wazi mapendekezo hayo hayakumfurahisha kabisa kwani yanataka wananchi wasitupwe pale inapokuja kwenye kunufaika na madini yao.

Ni kweli Mvutano ni mkubwa na hata kuhusu NAFTA...Ambao ni ushirikiano wa nchi za North America Canada ikiwemo ilikuwa na misuguano ambapo Clinton na kamapani yake walitaka iwepo na huku msuguano ukiendelea kuwepo na hata kupelekea wacanada hao kutoa kauli mbaya dhidi ya Obama wakati flani pale ambapo kulikuwepo na mjadala wa kuhusu NAFTA na wacanada hao wakamtoa nishai Obama ili kushushia hadhi na kumkumbatia Clinton ambaye wanamsikiliza kama Mungu Mtu.

Ni wazi JK amemkumbatia Sinclair more than anavyofanya kwa Taifa lake.

Sinclair alipopewa ripoti alidai kuwa uamuzi wa mwisho ni wa JK....!

JE...Uamuzi wa mwisho wa JK NI UPI?

TUNATAKA RIPOTI ISOMWE NA MH RAIS ATOWE MAAMUZI ILI TUJUWE KAMA BADO ANAMKUMBATIA SINCLAIR AMA MASLAHI YA TAIFA.
 
kikwete hana jeuri hiyo kama angekuwa nayo asingeipenyeza kwa swahiba wake Sinclair kwanza aipitie.
 
kikwete hana jeuri hiyo kama angekuwa nayo asingeipenyeza kwa swahiba wake Sinclair kwanza aipitie.

Na hapo ndiyo LEGITIMACY yake ya kuwa MTAWALA WA NCHI YETU INAPOKUWA HAIPO TENA!
Kama akishindwa kuyatetea MASLAHI YA TAIFA NA VIZAZI VIJAVYO...Basi HATAKIWI HATA KUGOMBEA URAISI TENA!
 
Zitto
user_offline.gif

Zitto has no status.
JF Senior Expert Member
Join Date: Fri Mar 2007
Posts: 325
Rep Power: 22
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif

Thanks: 42
Thanked 643 Times in 150 Posts
Credits: 28,429


icon1.gif
Re: GEORGE KAHAMA na ANDY YOUNG wamegombana?
........sasa hivi TZ kuna mnyukano mkubwa sana kwa ahadi za huyu kikwete kwa weupe hao alipokuja waziri mkuu wa canada haikuwa ziara nyepesi kama vyombo vyetu vilivyoripoti bali ni kubomolewa kwa ngome ya makampuni ya marekani na canada kuna kitu kimewagonganisha haya majitu, na hata hii inayoitwa kamati ya madini inatafutwa ili kumfunga paka kengele ili asilaumiwe kikwete bali mapendekezo ya kamati kikwete anayahitaji kujifichia ili afanye kinyume na yale aliyowaahidi waliomfadhili......

You cant be more right!!!!!!

Je...Paka ALIFUNGIKA KENGELE?
WAPI MAJADILIANO YA RIPOTI?
WAPI MAAMUZI YA RAIS?
 
He is a coward.Amteme alafu ale wapi?vile vitoto vyake nani ata vipa sponsorship akimtema?na walivyo wengi kama timu.Hatemwi mtu hapa hizi ni hadithi za sungura na fisi wataliendeleza gemu kwa kutuibia mpaka kesho na keshokutwa.

Plan for the best but hope for the worst.
 
SASA MACHAFUKO NA UMWAGAJI DAMU NANI ANATAKA KUSABABISHA?
Kwani hawajui gazabu ya wananchi ama?
Na jana Zitto kaugua!?
 
Ripoti ya madini moto

2008-07-10 11:49:49
Na Jackson Kalindimya, Dodoma


Bunge limekubali kupanga muda maalum wa kuijadili ripoti ya Kamati ya Rais ya Kupitia Mikataba ya Madini nchini iliyowasilishwa Bungeni na kupewa Wabunge ili ijadiliwe kwa kina kutokana na uzito wake.

Naibu Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda, alitoa msimamao huo jana, akiunga mkono shauku ya Wabunge wengi kutaka ripoti hiyo ijadiliwe kwa kina.

``Kwa sababu Wabunge wengi wameonyesha nia ya kutaka ripoti hii ijadiliwe na kutokana na uzito wake naona kuwa itapangiwa muda muafaka ili ijadiliwe,`` alisema Bi. Makinda na msimamo huo kuungwa mkono kwa makofi ya Wabunge wengi.

Hoja ya kutaka ripoti hiyo ijadiliwe, ilitolewa na Mbunge wa Mtera (CCM), Bw. John Malecela, ambaye aliwahi kushika nyadhifa za juu serikalini, ikiwemo Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, ambaye aliliomba Bunge lipange muda maalum wa kuijadili ripoti hiyo waliyokabidhiwa juzi ili waipitie.

Naibu Spika, baada ya kuona Wabunge wengi wamesimama kuunga mkono hoja ya Bw. Malecela alisema kuwa hata wao waliona kuwa lina umuhimu wa kulijadili, lakini awali halikuwepo katika orodha ya mjadala wa kipekee.

Hata hivyo, aliahidi kupanga muda maalumu wa kuijadili ripoti hiyo. Hakutaja lini.

Hoja hiyo ilitolewa mara baada ya kipindi cha maswali kukamilika asubuhi na kabla hawajaanza kuijadili hotuba ya makadirio ya mapato na matumzi ya Wizara ya Nishati na Madini iliyowasilishwa na Waziri wake, Bw. William Ngeleja.

Wabunge wengi walioisoma ripoti hiyo, waliisifu kuwa ni nzuri na imeandikwa kwa upeo mkubwa wa kutatua matatizo yaliyoko katika sekta hiyo ya madini inayolalamikiwa sana.

Baadhi ya mambo yaliyosifiwa, ni mapendekezo ya kamati hiyo iliyoongozwa na Jaji Mark Bomani, inayotaka wageni wasiruhusiwe kuchimba madini ya vito, huku miongoni mwa maudhui ya ripoti ikitaja kuwepo usimamizi duni wa rasilimali hiyo ya taifa.

Kwa mujibu wa Wabunge, kamati hiyo pia imebainisha vitendo vya udhalilishaji katika migodi mikubwa, ikiwa ni pamoja na wafanyakazi kukaguliwa na miale ya x-ray, jambo ambalo ni hatari kiafya na udhalilishaji.

Mbunge Malecelea akitoa hoja bungeni, alisema ripoti hiyo ni muhimu ikajadiliwa na Wabunge kabla ya kwenda katika hatua nyingine ya utekelezaji. Kamati hiyo iliundwa na Rais Jakaya Kikwete, mwishoni mwa mwaka jana.

Baada ya kutolewa hoja hiyo, Anne, aliyekuwa akiongoza kikao jana asubuhi, aliridhia hoja hiyo na kufafanua kuwa hata Spika Samwel Sitta, baada ya kupata ripoti, alitaka ipewe muda wa kuujadili.

Katika ratiba ya vikao vya bunge vinavyomalizika mwezi ujao suala hilo halikuwepo Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati yalipitishwa jana jioni.

Akichangia mjadala huo mbunge wa Vunjo (CCM), Bi. Aloyce Kimaro, aliungana na wenzake wanaounga mkono ripoti ya Jaji Bomani na kutaka hatua zaidi zichukuliwe ili kuanza utekelezaji.

Naye Mbunge wa Tabora (CCM), Bw. Siraju Kaboyonga, alisema hakuna sababu ya serikali kuendelea kusubiri, kwani baadhi ya mambo yaliyomo kwenye ripoti hiyo si ya kisheria, akirejea kauli ya Waziri Bw . Ngeleja, aliyesema kua sheria na sera mpya ya madini itakamilika ifikapo Aprili mwakani.

Alitahadharisha kwamba, hadi sheria mpya itakapoanza, tayari yatakuwepo mabadiliko makubwa yatakayoliingizia taifa hasara kubwa hasa ikizingatiwa kuwa wazalishaji hao wanafanyakazi kwa saa 24 na bei ya madini inapanda kila kukicha.

Bw. Kaboyonga, alitoa mfano kwamba, madini ya almasi katika kipindi kifupi kilichopita kipimo cha wakia (once) moja ilikuwa dola za Marekani 250 na sasa imepanda hadi kufikia dola 900, hali inayoashiria ongezeko la bei kwa kasi kubwa.

Ripoti ya kamati imeshauri kuwa baadhi ya mambo kama vile vivutio vya kodi viondolewe kwa wewekezaji wa madini na mirahaba wanayotozwa wachimbaji ipande.

Miongoni mwa changamoto zilizoko katika ripoti ya kamati hiyo ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi ni uharibifu wa mazingira, migogoro baina ya wawekezaji na matokeo ya uzalishaji wa madini hauna matunda mazuri kiuchumi ikiwa pamoja na kuwepo uhusiano mbaya baina ya wachimbaji wadogo na wakubwa.

Karibu wabunge wote waliochangia kutoka chama tawala na vyama vya upinzani waliisifia ripoti hiyo.

Ripoti hiyo iliyoongozwa na Jaji Mark Bomani ilifanya tatmini ya mapitio katika migodi yote mikubwa nchini, ikiwemo iliyopo katika mikoa ya Shinyanga, Mwanza,Mbeya, Tabora na Mara.

Kamati hiyo, pia ilisafiri katika nchi kadhaa kuangalia namna gani sekta ya madini inavyoendeshwa ikiwa pamoja na kupitia mikataba mbalimbali ya uwekezaji.
  • SOURCE: Nipashe
 
Alitahadharisha kwamba, hadi sheria mpya itakapoanza, tayari yatakuwepo mabadiliko makubwa yatakayoliingizia taifa hasara kubwa hasa ikizingatiwa kuwa wazalishaji hao wanafanyakazi kwa saa 24 na bei ya madini inapanda kila kukicha.

Bw. Kaboyonga, alitoa mfano kwamba, madini ya almasi katika kipindi kifupi kilichopita kipimo cha wakia (once) moja ilikuwa dola za Marekani 250 na sasa imepanda hadi kufikia dola 900, hali inayoashiria ongezeko la bei kwa kasi kubwa.
Jambo jingine pia ninalotaka kuligusia hapa kwa viongozi ni kuhusu madini ya DHAHABU!

Huu ndio wakati wakuvuna mapato ya DHAHABU KWANI KADRI DOLA INAVYOZIDI KUSHUKA THAMANI NDIVYO KADRI DHAHABU INAVYOZIDI KUONGEZEKA THAMANI NA KUPANDA BEI KWANI WATU WANA INVEST KWENYE GOLD KWASABABU YA DOLLAR'S WEAKNESS KWA KUSHUKA THAMANI...

HAKUNA WACHUMI HUKO AMBAO WAKO UP TO DATE JAMANI ILI TUJIKWAMUE KWA KUTUMIA UTAJIRI WETU?

BOTSWNA HATA WAKIMPINGA MUGABE NI HAKI YAO...

KWANI WANA MAENDELEO SANA NA MADINI YAO YAMEWATAJIRISHA NA WAMEENDELEA SANA TU!

Thats a HINT!
 
Dhahabu ina thamani kuliko pesa kwani hata kipimo cha thamani ya pesa NA utajiri wa taifa hupimwa kwa tumia dhahabu!

Hata marekani wenyewe licha ya kwamba hawachimbi dhahabu lakini UTAJIRI WAO UKO IN TERMS OF GOLD!

Na ndio maana kadri Dollar inavyozidi kushuka thamani..Wazungu huwekeza kwenye gold kwani wakati huo thamani yake hupanda na ndipo mahali ambapo una uhakika wa kupata profit hata kama UCHUMI WA DUNIA UKIYUMBA!

Hivyo basi ndugu zangu niliposema kuwa wakoloni wanarudi sikuwa nimekurupuka!

SASA HIVI UCHUMI WA DUNIA UNAKOELEKEA...NI MADINI NA MAFUTA PEKE YAKE YATAKAYOKUWA NA THAMANI KULIKO KITU KINGINE CHOCHOTE KILE...!

Hii nina maana hata UHAI WENYEWE!

KINGINE AMBACHO KINAWEZA KUWA NA THAMANI NA HATA KUTUFANYA TUONE KUWA DHAHABU YETU SI KITU NI SILAHA ZA VITA VYA WENYEWE KWA WENYEWE!

Hivo ni muhimu sana kwa viongozi wetu kuwa makini this time around na kwa mshangao mkubwa ndani ya miaka 25 ijao Tanzania inaweza kuwa PARADISE!
 
Ni wishful thinking. Kikwete hawezi kumtema Sinclair. Sinclair ni Mmarekani anayeongoza kampuni ya Barrick au Mcanada lakini anaishi Marekani. Family ya Bush wana hisa katika kampuni ya Barrick kwa hiyo hakuna tofauti kama ni Canada au Marekani katika hili. Na August mwungwana anatinga White House kwa dinner rasmi ya Bush.
 
Ni wishful thinking. Kikwete hawezi kumtema Sinclair. Sinclair ni Mmarekani anayeongoza kampuni ya Barrick au Mcanada lakini anaishi Marekani. Family ya Bush wana hisa katika kampuni ya Barrick kwa hiyo hakuna tofauti kama ni Canada au Marekani katika hili. Na August mwungwana anatinga White House kwa dinner rasmi ya Bush.

Hii yako sijuwi niite nini kama yangu ni wishfull thinking!
Sasa ngoja nikwambie...Huko Bungeni kama kweli mikataba hiyo ya Sinclair na Bush ni ya kumnufaisha mwananchi then tutasikia mapendekezo ya SINCLAIR,BUSH,NA KIKWETE DHIDI YA MAPENDEKEZO YA KAMATI AMBAYO YANAPENDEKEZA HAKI KWA MWANANCHI!
Hapo ndipo kwenye HIYO WISHFULL THINKING YANGU NA SI VINGINEVYO!
AJE TU HAPA WASHINGTON...SI NI AUGUST?

NB:Mimi nazungumzia THAMANI YA MADINI YETU NA UMUHIMU WA KIKWETE KUZINGATIA MAPENDEKEZO YA KWENYE RIPOTI NA WEWE UNALETA ZA WISHFULL THINKING!
NA WEWE THINKING ZA AINA GANI?
 
jmushi

Kile Kipindi Cha Kuwa Na Tanzania Mining Authority Kimefika, Andaa Cv Tu Najua Una Masters Ya Geology
 
jmushi

Kile Kipindi Cha Kuwa Na Tanzania Mining Authority Kimefika, Andaa Cv Tu Najua Una Masters Ya Geology

Is this supposed to be a joke?
Anyways...Kuwa na knowledge ya Geology haina maana ya kuwa na knowledge ya kuwa fisadi.
Hivi inahitaji Masters ya Geology kujuwa kuwa NCHI IMEUZWA NA HATUNA UHURU TENA?
 
Zitto atoka hospitali



na Lucy Ngowi, Dodoma



MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (CHADEMA), aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), baada ya afya kuzorota, ameruhusiwa.
Ofisa Uhusiano wa MNH, Aminiel Aligaesha, aliwaambia waandishi wa habari kuwa mbunge huyo aliruhusiwa kuondoka jana saa nne asubuhi baada ya afya yake kutengamaa.
Mbunge huyo alianza kuugua mwishoni mwa wiki alipokuwa kwenye ziara mkoani Tanga, alikokwenda kuwapongeza wanachama wa CHADEMA kwa kufanikiwa kutwaa viti vitano vya Serikali ya Mtaa wa Msikiti.
Taarifa za kuugua kwa mbunge huyo zilianza kupatikana kuanzia Jumatatu hadi juzi, zilikuwa zikieleza kuwa mwanasiasa huyo alifikishwa katika hospitali hiyo juzi saa 3:00 usiku.
Akizungumza na Tanzania Daima kwa nyakati tofauti, juzi na jana, Zitto, mmoja wa wanasiasa machachari ndani na nje ya Bunge, alisema alianza kujisikia vibaya tangu akiwa ziarani mkoani Tanga mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mabadiliko hayo ya kiafya yalisababisha Zitto ajikute akishindwa kwenda Dodoma siku hiyo ya Jumatatu, kutokana na ushauri wa daktari aliyemtaka apumzike, baada ya kuchomwa sindano moja na kupewa dawa nyingine.
Zitto ameugua wakati Bunge likijadili hotuba ya bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, ambayo alisema alikuwa na hamu kubwa nayo, kwani alitaka kuchangia mjadala wa hotuba ya bajeti hiyo, hususan katika sekta ya madini.
Kuruhusiwa kwa Zitto kutoka hospitalini hapo, kulithibitishwa pia na chama chake cha CHADEMA. Taarifa ya kuruhusiwa kwa Zitto ilitolewa na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho, Erasto Tumbo, ambaye aliwashukuru madaktari wa hospitali ya Muhimbili kwa ushirikiano na ukarimu wao, katika kuhakikisha Zitto anapata nafuu haraka. “Tunavishukuru vyombo vya habari kwa kuujulisha umma kuhusu maendeleo ya afya ya Zitto katika kipindi alichokuwa akikabiliwa na maumivu, yaliyotokana na mkusanyiko wa uchovu wa muda mrefu bila mapumziko,” alisema Tumbo.
 
Mwelekeo ni mzuri wa mjadala. Lakini swala la Msingi ni Je Sinclair alipata wapi Repoti ya Kamati ya Bomani wakati ilikuwa imekabidhiwa kwa Rais na Wabunge wamepewa tu siku ya Bajeti ya Nishati na Madini? Je ni kweli kuwa Taarifa za Rasilimali za nchi yetu inaweza kuwa siri kwa Wawakilishi wa Wananchi (Bunge) na kwa Wananchi wenyewe ambao ndio wenye mali? Je katika nchi zao kina Sinclair wananchi wanaweza kunyimwa Taarifa muhimu kama hiyo, aidha directly au kupitia Wawakilishi Wao. Tusiporekebisha haya nchi yetu itaendelea kuathirika kwa miaka mingi ijayo na mwamko uliojitokeza utayeyuka kama maua kwenye jua kali. Mwenye kufahamu Sinclair alipataje Taarifa hii nyeti tunaomba atufahamishe.
 
mi nawakumbusha tu ndugu zanguni kuwa madini sio viazi kusema yakiisha msimu huu mtasubiri msimu ujao...so tukae tukijua madini hayaoti, na yakishaisha ndo basi tena so tusicheze na swala hili
 
Dr. Slaa nadhani hilo swali angeulizwa Ngeleja au mtu kutaka maelezo kutoka kwa Ikulu kama wao ndio chanzo cha habari hiyo kwa Sinclair.
 
Inatakiwa critical thinking and analysis kabla hatujasifia Repoti ya Kamati ya Bomani. Issue siyo uzuri wa Repoti ya Bomani au hata content yake. What is the main difference between Kamati ya Bomani na ya Masha au ya Kipokola? Hizo hazikuwa nzuri ndiyo maana ziliwekwa kwenye Shelf na hapakuwa na utekelezaji japo Kamati hizo pia zimetumia fedha nyingi za Walipa kodi kama ilivyo kwa Kamati ya Bomani? Huu ugonjwa wa kuunda kila mara Kamati panapotokea jambo japo Taarifa za Kamati hizo hazielekei kufanyiwa kazi na wala hakuna anayezifanyia monitoring utaisha vipi na lini? These are core issues kabla hatujasifia hizi Repoti. Tusiingie kwenye mtego wa kusifia na hatimaye tukaumbuka kwa kukosa utekelezaji na Taifa likakosa matokeo yanayotegemewa. Niamini kwa dhati mjadala kwa sura hii utasukuma sana usimamizi wa utekelezaji wa Taarifa jambo lenye Tija zaidi kuliko kuisifu per se, kwa vile hata ya Taarifa ya Kamati ya Kipokola au ya Masha kwa walioziona hazina tofauti sana na Taarifa ya Bomani lakini tatizo ni kutotekelezwa hadi imeundwa Kamati ya Bomani . May be walionazo wanaweza kuwasaidia wale ambao hawakuziona ili zifanyiwe analysis jambo litakalosaidia Bunge kuwa na changamoto wakati wa mjadala ulioahidiwa.
 
Back
Top Bottom