Mokaze
JF-Expert Member
- Aug 3, 2018
- 14,370
- 14,929
Mimi sikubaliani na hayo maelezo ya heaven and earth kutoka kwa dini yako wala summerian kwamba ni maelezo yanayoelezea bing bang
Kama hukubaliani kwamba maelezo hayo ya Summerian yanahusu the big bang kwanini uliyaleta hapa na kuyahusisha na Qur'an katika Subject matter ya the big bang??!----kumbuka topic ni the big bang katika Quran sasa kwanini uingize vitu visivyohusika??!!.
Kwa hiyo hoja yeyote inayohusiana na hizo aya napinga kwamba zimeongelea bing bang, ifahamike hivyo kwanza.
Kwahiyo hata hayo maandishi ya Summerians unayoyashadidia kwamba Qur'an imeyakopi nayo sasa hayafai??, sasa yamekuwa ya uongo na sio ukweli tena?!!
Halafu nikija sasa kwenye hoja yako ya kuhusu kuandika habari ambayo ilishawahi kuandikwa before au kutafiti vyanzo vya vitu ambavyo viliwahi kuandikwa kwenye source nyingine kabla, kuhusisha jambo hilo na dhana ya kukopi taarifa bila shaka hoja hiyo imeletwa humu na wewe.
Hiyo hoja ya kukopi ni wewe ndiye uliyeileta wala sio mimi, ni wewe unayesema au uliyesema kwamba Qur'an imekopi hiyo habari ya the big bang kutoka katika Holy scripts za dini ya kale ya Kipagani ya Summerians!!, iweje sasa unaniangushia mzigo wako mimi??!, mimi nilikupa hoja; 1--- ukweli unatoka kwa Mungu na hata kama ukweli utoke kwa "Muongo" bado utabaki kuwa ukweli licha ya yeye kuwa na tabia ya uongo, uongo unatoka kwa shetani hivyo hao Summerians licha ya upagani wao lakini hatuwezi kupinga Ukweli wao, 2--- Nikakupa hoja kwamba; kama unasema Qur'an ilikopi kutoka kwa hao Summerians vipi na mimi nikisema kwamba hao Summerians na wao walikopi habari hiyo kutoka kwa Watakatifu wa Mungu katika zama hizo waliofunuliwa hiyo habari ya the big bang ambayo hivi sasa unaikanusha??!, 3--- Hoja nyingine niliyotoa ni; Mungu/Allah ni yeye kwa mujibu wa Qur'an aliyeanzisha hiyo the big bang na aliianzisha hata kabla hajawaumba hao Summerians na viumbe hai wengine sasa utasemaje maandishi ya the big bang ndani ya Qur'an awe amekopi?!, akopi habari ya jambo alilofanya mwenyewe kutoka kwa Summerians??!!, labda upinge Qur'an sio ufunuo wa Allah ambayo hiyo ni mada nyingine.
Wewe ndiye uliyedai kwamba sayansi inatumia Quran kufanya majaribio yake kwasababu kipindi Quran inaandikwa hakukuwahi kuwepo na sayansi
Madai yangu ni haya; wanasayansi wamekuwa wakivumbua baadhi ya mambo ambayo tayari yalikwisha elezwa na Qur'an tangu miaka 1400 iliyopita na katika hilo kuna baadhi ya wanasayansi wamekuwa wakisoma Qur'an ili kupata chochote kitakachowasaidia katika mambo yao ya kisayansi na nimekupa mfano hai wa Mwanasayansi nguli (international calibre) ambaye alikuwa anadai kuwa theory zake za kifizikia (base) alikuwa anazipata kutoka katika Qur'an jambo ambalo wanasayansi wenzake walikuwa wanashangaa sana wakiangalia U genious wake na jambo analoliongea na hata baadhi yao ilibidi waanze kusoma Qur'an.
Mimi ndo nimekuuliza kama ndio hivyo basi hata Quran itakuwa ime kopi maelezo ya hiyo aya kutoka kwenye dini ya kale ya summerian kwa maana ilikuwepo miaka elfu kabla ya uislam.
Kama wewe unaleta dhana hiyo ya kukopi na mimi usinipinge nikisema; hao Summerians huenda nao walikopi habari hiyo kutoka kwa watakatifu wa Mungu katika zama hizo kwani UKWELI WOTE hutoka kwa Mungu na Uongo wote hutoka kwa shetani, licha ya hao kuwa wapagani huwezi kupinga kwamba hata siku moja hawakusema jambo la ukweli.
Sasa nataka nijue msimamo wako hapa ni upi, unakubali kua sayansi haifanyi majaribio kwa kuangalia kilichoandikwa kwenye Quran bali ni kwa utashi wake, au inafanya hivyo kwa kufata muongozo wa Quran halafu baadaye ulazimike kukubali kua Quran ilikopi maelezo kutoka kwenye dini nyingine?
Mimi sijasema kwamba sayansi (wanasayansi) YOTE inafuata kilichoandikwa ndani ya Qur'an kwani kuna Wanasayansi wengine hata hiyo Qur'an hawaiamini sembuse hata kuisoma!!!, ninachosema ni hichi; wanasayansi wamekuwa wakigundua/vumbua mambo ambayo Qur'an imeisha yaeleza kabla na wapo wanasayansi ambao kwa kauli zao wenyewe wanasema wameweza kujifunza na kugundua habari zilizowasaidia katika mambo yao ya kisayansi.
Na kama sayansi imetafiti bing bang utajuaje kama ilitumia mungozo wa kitabu chako na sio summerian holy texts ya miaka ya zamani kabla ya kitabu chako?
Yote kwa yote, tufanye hao wanasayansi walifuata hiyo Summerians holy texts kutafiti the big bang, niambie UKWELI unatoka kwa Mungu au unatoka kwa shetani??!, kama kitabu cha Summerians kimeandika habari ya ukweli na Qur'an imeandika habari hiyo hiyo ya Ukweli kosa hapo nini??, Kosa ni Qur'an kuurejea huo kuandika UKWELI??!.
Wewe ndugu nimegundua upo hivi; "kama nduguyo ni Muongo upo radhi kutetea uongo wake kwa kuwa ni nduguyo lakini haupo radhi kutetea ukweli wa adui asiye nduguyo".--- huo sio uadilifu na Mungu hapendi jambo hilo.
Huyo mwanasayansi au sheikh?
Unataka kujua Abdus Salam ni Shk au Mwanasayansi??
Huyo alikuwa ni mwasayansi wa International calibre, anao mchango katika fani ya Physics, yeye alipata nishani ya Nobel katika physics in Electro weak forces unification, yeye ndiye aliyeanzisha Department of theoretical physics katika Emperial college London, yeye ndiye aliyesaidia kugunduliwa kwa God particle/Higgs bossin particle kwa kubuni (formulations ) the biggest and expensive particle accelerator (Hydron collider) huko Swiss, yeye ndiye aliyejenga kituo cha kisayansi kwa ajili ya nchi zote zinazoendelea huko Trease Italy, yeye alikuwa prof, katika Cambridge university, kafanya tafiti nyingi za kisayansi kwa ajili ya makampuni makubwa mbalimbali duniani, kaandika Theories nyingi sana hadi leo hii hakuna mwanasayansi aliyezigusa hadi Colleagues wenzake walimuambia hadi Einstein afufuke ndiye anaweza ku comment katika theories zake, kaandika vitabu kadhaa kuhusu Physics, anazo nishani dozens kutoka katika vyuo vikuu na taasisi mbalimbali duniani, Kwakweli huyu mtu anayo profile kubwa sana, ila dunia labda haimpendi kwa kusema kwake; "Theories zangu zote nimezipata kutoka katika Qur'an tukufu"--- huyo ndiye Marehemu Prof Abdus salam aliyepata kuja Tz miaka ya 1979?? na akapokewa ikulu kwa heshima na Mwalim Jk nyerere pia alitoa muhadhara UDSM kuhusu sayansi nk,, huyo ndiye aliyepata kupikiwa chai na Waziri mkuu wa zamani wa India Bibi Indira Ghandi pia alimuomba abadilishe uraia wake na awe indian badala ya Pakistan, anayo historia ndefu ambayo hatuwezi kuimaliza hapa.
Hatajwi sana kwasababu ya Uisilamu wake.