Labda uniambie Allah hakusema kweli !! (Allah apishe mbali), lakini kama kasema kweli basi tumtafute mtu aliyedai utume na akadai kwamba ametumwa na Allah kufundisha aya za Qur'an na amefanya kila juhudi kuonyesha jinsi alivyofundisha hiyo Qur'an, tumtafute huyo mtu leo hii, huwezi kumpata isipokuwa ni Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad (as) ambaye ameandika vitabu 84 vyote hivyo vinahusu mafundisho ya Qur'an na dini ya Uisilamu kwa ujumla hivyo mafundisho yake yapo na kwakuwa yapo na yanafundishwa na Makhalifa wake basi hiyo ni sawa ukisema ni yeye anayetufundisha kupitia huyo khalifa, mfano ni sawa leo ukisoma Qur'an aya inayosema "Usikaribie zinaa" na ukasema kwamba Allah anatufundisha kupitia Mtukufu mtume Muhammad (saw) kwamba tusikaribie zinaa, je hapo kuna kosa??! kwasababu Allah haonekani na Mtume (saw) kishafariki lakini bado tunasema wao wanatufundisha kupitia Qur'an na ni hivyohivyo kwamba mafundisho sahihi ya Qur'an utayapata kupitia vitabu vya hadhrat Ahmad (as) kwa kusoma vitabu vyake na kumsikiliza khalifa wake hiyo ni sawa na yeye kutufundisha.
Leo, Ukisubiri ili umpate mtume aje akusomee aya za Qur'an utakesha kumtafuta na usimpate kwani tayari alikuja na akaanzisha jumuiya kwa amri ya Allah ambayo imekuwa ikifanya kazi hiyo hata leo hii, ni Jumuiyya ya Waisilamu wa Ahmadiyya iliyoanzishwa na Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad (as) mtume mfuasi wa mtukufu Mtume Muhammad (saw) ndiyo imekuwa ikifundisha Qur'an kwa usahihi.