Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nani huyu?

Sio raia wote wenye dini, kuna wengine ni wapagani pia.
 
Wasio na dini wasalimiajwe?
 
Ni jambo jema sana kutoingiza mambo ya dini katika serikali. Nchi yetu inapaswa kuwa secular kadri iwezekanvyo kama tunataka utangamano wa muda mrefu zaidi.
Tunakwepa kutamka “Tumsifu Yesu Kristu “ na “Bwana Yesu asifiwe “.
 
Ukisalimiwa salamu ya dini yako ndio unaona umeheshimiwa?
Una point hapo. Sasa Rais lazima kupenda na kuheshimu dini za wananchi wote. Basi anagalau abadilishe kidogo aseme ""Msifuni Yesu Kristu!"
 
Awasalamie watu hamjambo ndugu zangu/habari zenu/ habari za wakati huu n.k
Salamu za dini ziwekwe mbali kabisa na mambo ya serikali, ni ushamba.
 
Ni jambo jema sana kutoingiza mambo ya dini katika serikali. Nchi yetu inapaswa kuwa secular kadri iwezekanvyo kama tunataka utangamano wa muda mrefu zaidi.

Ungeyatamka haya wakati huo
 
Kwenye kamusi pia hakuna salamu ya Bwana Yesu asifiwe au tumsifu Yesu Kristo
Hakuna mantiki yeyote kwenye hoja yako,

Hata kwenye kamusi ya kiswahili hakuna salamu ya namna hiyo.
 
Wasio na dini wasalimiajwe?
Ni jambo jema sana kutoingiza mambo ya dini katika serikali. Nchi yetu inapaswa kuwa secular kadri iwezekanvyo kama tunataka utangamano wa muda mrefu zaidi.

Nakubaliana na wewe 100% kwamba religion and politics must be separated. Kosa analofanya Bi Mkubwa kwenye salamu hii ni kuondoa mamlaka ya Mungu kwenye mahali husika pa msingi (^Nakusalimieni kwa jina la Yesu^) na kuweka ile nyingine ya kibinadamu -- JMT, huku akitegemea raia anaowaongoza ambao wana imani zao wakubaliane nayo.

Ukishaanza kutumia mstari huo tu (^Nakusalimieni kwa jina la ...^), kwa MKristo yeyote yule huwa inaprovoke feelings za kumsabihi Muumba ama Mola. Sasa kinapopachikwa kipande kingine (JMT), ni wazi Wakristo huamini kwamba wanalazimishwa mchwaha (indirectly) kuabudu mungu sanamu yaani, JMT.
 
Wakae kimya, sio lazima kuitikia, Halafu wajue mama ni muislamu safi, hawezi kumkana Allah wake kwa mungu mwingine ambao hao Wakristo wanaamini ni JMT.
 
Mmeanza chokochoko wanaume wazima mnakuja humu na mada za kitoto.au mmetumwa? Hapo tatizo lipo wapi au ilimradi karaha tu mtafute pakuhemea? Shame on you!!
 
Ni jambo jema sana kutoingiza mambo ya dini katika serikali. Nchi yetu inapaswa kuwa secular kadri iwezekanvyo kama tunataka utangamano wa muda mrefu zaidi.
Ungeileta hii hoja wakati huo.
View attachment 1823101
Ungeyatamka haya wakati huo
Actually, tunaposema serikali haina dini maana yake ni kwamba mtawala yeyote aliyepewa dhamana ya uongozi, mathalani Rais wa Nchi, hatatumia nafasi yake ya Urais KUSHURUTISHA dini yoyote kwenda kinyume na misingi ya imani ya dini husika ambayo haipingani na kanuni za haki, usawa, utu na ubinadamu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria.

Lakini pia ni wajibu wa viongozi hawahawa kuwafuata wananchi kule waliko -- yaani, kwa muktadha huu, kuwasiliana nao katika ^lugha wanazofahamu na imani wanazoshikilia.^ Mbona wakati wa kampeni za uchaguzi huwa hakuna mtu anayewafundisha hawa viongozi namna ya kuenenda, kuzungumza na hata kutenda wanapohitaji kuwasiliana na raia!??? Na huwa wanafanya vizuri sana!!!

Hitimisho: It's the leaders who should be flexible not their subjects, with regard to the mode of conversation and communication.
 
When you go places, go places with style. Mama amebuni Salamu na akatuelekeza jinsi yakuijibu. Hiyo ni maalum kwa ajili yake baada ya hapo endelea na utamaduni wako, tatizo lipo wapi?
 
Mmeanza chokochoko wanaume wazima mnakuja humu na mada za kitoto.au mmetumwa? Hapo tatizo lipo wapi au ilimradi karaha tu mtafute pakuhemea? Shame on you!!
Wewe mwenzao unaona kuwa ni ^mada za kitoto,^ lakini wenzangu na mie tunaona ni ^mada za moto^ Umeelewa sasa, au umelewa na kuelemewa!???
 
Mbona sioni watu wengi masokoni na sehemu nyingine mitaani wakisalimiana Tumsifu Yesu Kristu au Asalamaleku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…