Jamhuri ya Uturuki | Türkiye Cumhuriyeti

Jamhuri ya Uturuki | Türkiye Cumhuriyeti

isajorsergio

Platinum Member
Joined
Apr 22, 2018
Posts
4,143
Reaction score
6,560
Jamhuri ya Uturuki, Türkiye Cummhuriyeti au Republic of Turkey

Uturuki
ni taifa lenye mipaka baina ya Asia na bara Uropa, asilimia 97 ya taifa limelalia upande wa Asia huku 3 ikiwa Ulaya. Uturuki yenye mipaka na bahari ya Mediterrania 'Mediterranean Sea', bahari ya Aegea 'Aegean Sea', peninsula za Anatolia 'Anatolian Peninsula' na Balkan.

Turkey Flag.jpg

Bendera ya Jamhuri ya Uturuki

Uturuki yenye ukubwa wa eneo zipatazo kilomita za mraba 780,580 sawa na maili za mraba 301,384 jirani na mataifa ya Armenia, Azerbaijan Nakhchiuan, Bulgaria, Cyprus, Uajemi, Uyunani na Syria. Uturuki ni nyumbani kwa watu takribani millioni 84,453,113 kufikia Agosti 17, 2020.

Turkey Region.png

Ramani yenye kuonesha kanda na mikoa ya Uturuki

Lugha rasmi ya taifa ni Kituruki, pesa rasmi ni Lira - Lira ya Kituruki 1 ni sawa na Kurus 100. Mji mkuu ni Ankara, mji wenye kuhodhi shughuli za kiserikali na kitaifa. Mji mkubwa na wenye maendeleo zaidi ni Istanbul, jiji kubwa zaidi bara Uropa kwa idadi ya watu, jiji la tatu kwa ukubwa wa eneo na jiji pekee lenye mipaka baina ya mabara mawili.

Ankara City.jpg

Jijini Ankara, Anatolia ya kati. Makao makuu ya taifa


Taksim Square.jpg

Taksim Square - Istanbul

Uturuki ya leo ndio iliyokuwa himaya ya Ottoman ' Ottoman Empire ' himaya kubwa zaidi, tajiri na yenye nguvu kuwahi kutokea duniani, himaya iliyotawala bara Ulaya, Asia na Afrika Kaskazini na Kati, nyumbani kwa mfalme wa wafalme, mfalme Süleyman, Pargalı Ibrahim Pasha na Fuat Pasha.

Uturuki iliyoasisiwa mwaka 1923 baada ya anguko la himaya ya Ottoman chini ya Mustafa Kemal Atatürk, ndio mwanzo wa taifa lenye nguvu, maendeleo na ushawishi kimataifa.

Atatürk kiongozi wa kwanza wa taifa aliyeingia na sera ya usawa na maendeleo ya waturuki, ikishuhudiwa usawa katika madaraka na baina ya jinsia, utawala bora na ukuaji wa kidiplomasia na uchumi.

Uchumi, Biashara, Utalii, Kilimo Uwekezaji na Maendeleo

Uturuki taifa la 19 kwa uchumi imara ikiwa ni taifa la 10 kwa mapinduzi ya viwanda, nafasi ya 14 katika uzalishaji wa vyombo vya moto na vifaa vya atomatiki.

Viwanda ndani ya taifa ni vyenye kuzalisha vifaa vya kielektroniki, vifaa vya majumbani, vifaa vya umeme, chakula na vinywaji. Uchumi ukichagizwa pakubwa na masuala ya kibenki, mawasiliano, teknolojia, uchimbaji, kilimo, utalii, ujenzi, vitambaa na mavazi.

Konya Town.jpg

Mji wa Konya, Anatolia ya kati.

Mifumo ya ujenzi ya Kituruki ni ya hali juu ikiwa imebobea katika aina tofauti ya ujenzi na ushiriki ndani ya mataifa ya Morocco, Georgia, Armenia, Syria, Uyunani, Ethiopia, Ureno na Somalia. Uturuki kupitia kampuni ya ujenzi Yerpı Markezı mjenzi wa bwawa kubwa Afrika ya Mashariki na Kati, bwana la kufua umeme la taifa - Tanzania.

Kampuni za vifaa vya kielektroniki, majumbani, vyakula na umeme Beko, Vestel, ÜLKER, Caykur na Lactaris zote ni chapa ya Kituruki. Biashara kubwa hufanyika baina ya mataifa ya Ujerumani, Uingereza, Umoja wa Falme za Kiarabu, Uhispania, Iraq, Uajemi, Italia, Ufaransa, Urusi na Marekani.

Tarim Farm.jpg

Tarim Farm - Antalya

Kupitia kilimo Uturuki ni kiongozi wa kilimo cha choroko na maua ya tulip huku ikitegemea mtama, ngano, miwa, karanga, matunda, mboga mboga, pamba, viungo mbalimbali, chai na mafuta ya zaetuni.

Bazaar-Turkish-Sweets.jpg

Viungo na vyakula mbalimbali katika soko la Kapalıçarsı ©ThemiShots

Uwekezaji ndani ya taifa ni kupitia shirika kubwa la usafirishaji, shirika lenye kuongoza kwa safari za anga katika maeneo 250 chapa ya Kituruki Turkish Airlines lenye maskani makuu Istanbul Atatürk Airport - kiwanja chenye kuunganisha mataifa 123, maeneo 250 na viwanja vya ndani 22 vyenye uwezo wa kimataifa.

Turkey_DNA-00.jpg

Nembo ya Shirika la ndege la Uturuki ©Tukish Airlines

TA.jpg

Ndege ya Turkish Airlines ©Turkish Airlines


Maendeleo yanaonekana zaidi kupitia ujenzi wa makazi bora, usawa baina ya vijiji na miji, barabara, viunganishi, treni na magari nyaya 'Cable Car's' kupitia maendeleo haya na asili ya historia, maendeleo zaidi ndani ya Istanbul, Ankara, Antalya, Bursa, Konya, Adana, Gaziantep, Sanliurfa, Diyarbakir, Erzurum, Samsun, Van, Malatya, Kayseri, Eskisehir na Trabzon hupelekea utalii.

csm_BursaI_II.jpg

Magari nyaya jijini Bursa ©Bursa Hebar

Utalii kupitia taifa ni sawa na rasilimali isiyokuwa na mfano, taifa lenye kupokea zaidi ya watalii millioni 50 kwa mwaka.

Suleymaniye-Mosque.jpg

Msikiti wa Süleymaniye ©Turkish Tourism Today

Utalii hufanyika pakubwa katika milima ya Taurus, mlima Arafat, maeneo katika uwanda wa Mesopotamia, mito Euphrates, Tigris na Aras. Maeneo ya kihistoria Istanbul, Cappadocia, Catalhöyük, Hattusa, Pergamon, Hierapolis - Pamukkale, Mlima Nemrut na Göbekli Tepe ni hifadhi za kihistoria zinazotambulika na UNESCO.

Southeastern Anatolia.jpg

Daraja la Kheril, Anatolia Kusini ©Turkiye Feim

Ufikapo Uturuki tembelea soko kubwa zaidi duniani Grand Bazaar ' Kapalıçarsı ' kuanzia mitaa ya Fuata Pasa Caddesi soko lenye kuchukua mitaa 61, likiwa na maduka zaidi ya elfu 4,000. Pitia Spice Bazaar ' Mısır Çarşısı ' lenye maana ya Soko la Kimisri, soko lenye shehena ya viungo mbalimbali kuwezesha kulisha dunia nzima kwa miaka mitano.

Grand-Bazaar.jpg

Soko la Kapalıçarsı (Grand Bazaar) ©ThemiShots

Sogea mbele uione Bosphorus Strait kiunganishi cha Uturuki ya Ulaya na Asia, utenganisho wa jiji la Istanbul kupitia daraja la Bosphorus lenye kutenganisha Karaköy na Kadıköy. Hapo fika Üsküdar uone mnara wa Kız Kulesi ' The Maiden Tower ' kupitia bonde la Camlica na wilaya ya Beyoğlu utizame Hagia Sofia.

Maiden-Tower.jpg

Mnara wa Kız Kulesi, Üsküdar ©Touropa

Hagia-Sophia.jpg

Hagia Sophia ©Touropa

Usisite sogea Ortakoy uitizame Hoteli Kempinski ya Istanbul, huku jioni yako ukitembelea kiwanja cha Babylon Spot hadi Club-Resort ujumuike na damu changa. Safari ya kilomita 91 itakufikisha jijini Bursa ukitokea Istanbul, fika Bursa Town Hall eneo lililokuwa la mikutano ya kiongozi Atatürk. Tembelea misikiti ya Bursa Grand Mosque na Green Mosque iliyonakshiwa na vigae vya kuchora.

Kusadasi City.jpg

Kusadasi ©Zulfika Haylam

Chukua picha katika daraja la İgandi ' İgandi Köprüsü ' huku ukitizama mto Nilufer. Hapa sogea Hotel Berussa katika mlima ushuhudie maajabu ya jua likizama huku mbingu ikibadili rangi ya bluu, zambarau na pink.

Utashuhudia gari nyaya ' Cable Car's ' zikiunganisha jiji la Bursa kupitia milima ya Uludag - Magari nyaya haya ndio yenye kuongoza kwa mtandao mrefu wa safari na uwekezaji duniani.

Elimu, Sayansi na Teknolojia

Elimu kwa taifa ni lazima ikiwa na ubora wa asilimia 94 nyuma ya Ujerumani, Uingereza, Uswissi, Uswidi, Marekani, Brasil, Korea Kusini na Japan. Mfumo wa elimu umegawanyika katika awali, msingi, upili na elimu ya juu.

Middle East University, Bilkent University, Istanbul University, Koç University, Boğaziçi University na Marmara University ni mfano wa vyuo bora ndani ya Uturuki.

Kupitia mtaala wa elimu “Theory of Evolution” imeondolewa huku kuanzia 2022 nadharia za dunia duara “Spherical/Globe Earth” na nadharia ya dunia yenye kipeuo cha usawa “Flat Earth” zote zitafundishwa na mhusika atachagua ni kipi che usahihi.

Uwepo wa elimu bora kumepelekea taifa kujenga vinu vya nyuklia Akkuyu Nuclear Power Plants pia kuwezesha urushaji wa satelaiti chapa Gökturk - 1, Gökturk - 2, Gökturk - 3, Türksat, BİLSAT -1 na RASAT.

Teknolojia ya anga na ulinzi inabebwa pakubwa na Turkish Aerospace, ASELSAN, Havelsan, ROKETSAN na MKE. Teknolojia inavyozidi kukua taifa linaanzisha gari chapa TOGG - Türkiye'nin Otomobili Girişim Grubu A.Y magari ya umeme, gesi na jua.

Bilişim Vadisi ni eneo na kambi ya teknolojia, mifumo ya tarakilishi na sayansi ya kompyuta sawa na ilivyokuwa Silicon Valley.

Kupitia sayansi dunia umeshuhudia mkemia wa Kituruki Bw. Aziz Sancar, mgunduzi wa ugonjwa wa Behçet Bw. Hulusi Behçet na mwanamahesabu Cahit Art wenye tuzo za Nobel.

Michezo, Sanaa na Muziki

Uturuki imetambulishwa kimataifa kupitia michezo na sanaa shukrani kwa katiba ya taifa yenye kueleza ni lazima serikali ya jamhuri kumuwezesha yeyote mwenye kipaji na talanta hadi kufikia ndoto zake.

IMG_20200819_221239.jpg

Mesut Mustafa Özil ©Mesut Özil kupitia Twitter

Mchezo pendwa ni mpira wa miguu ukiwakilishwa vyema na timu ya taifa ya Uturuki, vilabu vya Beşiktaş, Bursaspor, Fenerbahçe na Galatasaray. Nyumbani kwa wachezaji Arda Turan, Mustafa Imran, Hassan Sas, Hakan Sukur, Hamza Uzer, Rayci Tönker, Ceguz Ünder, Emre Can na Mesut Özil.

Kupitia sanaa ya uchoraji na uandishi Uturuki inawakilishwa na Bedri Rahmi, Burhan Doğançay, Fahrünnisa Zeid, Cemal Tollu, Nâzim Hikmet na Orhan Veli. Wabunifu Ege İslekel na Kadir Kiliç.

Irmak_ARICI_18_663801.jpg

İrmak Arıcı akiwa studio ©Yalsın Sasi

Muziki ni haiba na asili ndani ya taifa likisheheni waimbaji na wanamuziki mifano ya Karem Görseu, Emre Aracı, Nükhet Rucan, Hadise, Mustafa Ceceli, Bilal Sonses, Aleyna Dalveren, Ece Mumay, Ece Seçkin, Feride Hilal Akin na Ahmet Ertegun mtayarishaji, mkurugenzi na mmiliki wa Atlantic Records.



Hande Yener - Bela

Nyumbani kwa malkia wa muziki wa pop ya Kituruki Hande Yener - muimbaji, mtayarishaji, muongozaji, muigizaji, mchoraji, muandishi na mbunifu anayetamba na nyimbo mfano wa Seviyorsun, Havaalanı, Kişkişş, Alt Dudak, Krema, Kus, Kuş, Pencere na Bela.



Hande Yener - Kuş

Kupitia wimbo Kuş wake Hande wenye maana ya ndege, ulitayarishwa vyema kwa asilimia 98 ndani ya Tanzania chini ya watayarishaji Ümit Kuzer, Altan Çetin, Howie Weinberg, Martin Spencer na Gülşen Aýbaba.



İrmak Arıcı - Yağmurum OI

Wanamuziki wengine ni mdada İrmak Arıcı mwenye nyimbo Yağmurum Oi, Mühür, Meuzum Derin na Kula Bela.

genc-sarkici-irmak-arici-emrullah-gul-un-konu-12779215_amp.jpg

İrmak Arıcı akiwa na mturuki mwenye asili ya Tanzania Genc Sarkici Saïd ©Yalsın Sasi

Genc Sarkici
ni mtayarishaji wa muziki mturuki mwenye asili na mzaliwa wa Tanzania, muandaaji wa wimbo Bela wake Hande na nyimbo kadha wa kadha chini ya netd müzik.

IMG_20200820_123115.jpg

Mtayarishaji Ümit Kuzer akiwa Virus Studios ©Kadir Kiliç

Watayarishaji nguli Ümit Kuzer, Altan Çetin, Sibel Alaş na Akin Onur Baytan wakiwakilisha Uturuki. Poll Production na netd müzik kampuni za muziki, filamu na uchapaji ni chapa ya Kituruki.

Hii ndio Jamhuri ya Uturuki 🇹🇷
 
asante sana mleta mada hakika nimepata kufahamu nisichokijua kuhusu uturuki.
sijajua sisi huku tunakwama wapi kwa kweli hakuna tunachoweza kujivunia mbele za watu.
utruki ni taifa la kiislam nadhani, lakini hatua ilzopiga sio ndogo kwa kweli na ni nadra sana kusikia mchafuko huko.
pia hata ukiangalia kazi zao sio za ubabaishaji.
nadhani ndio wenye feza schools, ona matokeo yake kwa kweli wapo juu mno itoshe kusema.
 
asante sana mleta mada hakika nimepata kufahamu nisichokijua kuhusu uturuki.
sijajua sisi huku tunakwama wapi kwa kweli hakuna tunachoweza kujivunia mbele za watu.
utruki ni taifa la kiislam nadhani, lakini hatua ilzopiga sio ndogo kwa kweli na ni nadra sana kusikia mchafuko huko.
pia hata ukiangalia kazi zao sio za ubabaishaji.
nadhani ndio wenye feza schools, ona matokeo yake kwa kweli wapo juu mno itoshe kusema.
Hakika,

Uturuki ni sawa na ubora na kuna miradi mingi inatekelezwa au kuendeshwa na Uturuki.
 
Back
Top Bottom