Namaanisha Uturuki sasa hivi imekuwa na tabia ambazo tume zoea kuziona kwa mataifa ya kibeberu.
Uturuki ukiiangalia kwa juujuu utaliona ni taifa la kawaida,lakini ukijaribu kuichimba kwa undani ni tofauti kabisa.
Uturuki siku hizi imekuwa mjunjaji mzuri wa sheria za kimataifa na mbabe kupita kiasi lakini hakuna anaye chukua hatua dhidi yake.
Uturuki inayakalia kwa nguvu maeneo ya Syria na Iraq lakini hakuna anaye thubutu kumchulia hatua.
Anaikalia kwa nguvu ardhi ya sypulas kusini na hakuna anaye dhubutu kumgusa.
Juzi juzi kaenda bahari ya Mediterranean kwenye maji yanayo milikiwa na Ugiriki kaanza kuchimba mafuta kibabe na wakati ni mwanachama mwenzake wa NATO.
Umoja wa mataifa umeweka vikwazo vya kuingiza silaa nchini Libya ,lakini uturuki kila kukicha meli za uturuki zina pereka silaha nchini Libya na hakuna anaye thubutu kuzigusa.
Hii kwakweli imekuwa ikinifikilisha sana.