Uturuki anafanya haya kulinda haki ya mipaka yake, hasa ardhi, ajira, usalama na fursa kwa kuhitaji kudhibiti wakimbizi toka Syria, Iraq na Libya. Uturuki ndio taifa pekee duniani lenye idadi kubwa ya wakimbizi, wakimbizi wanaoruhusiwa kuishi na jamii na sio katika kambi, wakimbizi wanaopatiwa fursa za ajira, afya na elimu sawa na raia.
Rasilimali ya taifa inahusika kufaidisha watu zaidi wasiokuwa wahusika, huku wenye chanzo hawapatwi na dhahma hii.
Uturuki kufanya haya pasi ya kuguswa ni kuwa wenye uwezo wa kumgusa wanaofahamu nini anafanya, ubabe wa baadhi ya mataifa katika Syria, Iraq na Libya ndio chanzo cha Uturuki kuingiliwa na wakimbizi hivyo Uturuki anapiga na hao wahusika indirectly.
Dunia ya sasa haitaji upole wala ukarimu uliozidi maana utaendeshwa tu, huku wengine (Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ubelgiji, Ujerumani, Japan, Uchina na Uhindini) wakionekana ndio wenye haki ya kuvamia pasi ya sababu za msingi maeneo na mataifa ya watu.