Jamii iache kuhukumu vibaya wanaume wanao ingia kwenye mahusiano ya kimapenzi ( ndoa ) na wanawake wenye umri mkubwa kuwazidi

Jamii iache kuhukumu vibaya wanaume wanao ingia kwenye mahusiano ya kimapenzi ( ndoa ) na wanawake wenye umri mkubwa kuwazidi

Mie mwanaume wa kumzidi umri namuona kama mwanangu.
Halafu naona kama vile atakuwa "haniweki vizuri" [emoji1787]
Nadhani akinizingua naweza kumuwasha makofi.
Raha ya mwanaume anizidi umri, akili, elimu, urefu na uchumi.

#teambigboys#
Umri nambaa tuuu... Harmonize kamuweka kajalaaa mpaka kajala kapagawaaa so kuhusu kuwekwaa hilo halina shidaa
 
Maisha yako ni Nini? Maisha yako yanakuwa yako siku ukiacha kusikiliza mitazamo, maoni kutoka kwa watu wengine, utaishi kwa raha kama Mimi tu hapa
 
Mwanaume anatakiwa kunizidi kwa kila kitu isipokuwa muonekano tu
Hahahaha upo sahihi ila iwe ni muono wako ila usilazimishe wengine kuwa na mtazamo wako katika jamii icho ndio twawaomba
 
Miezi tu? Kama kweli unampenda kuwa nae. Ukifuata jamii itakuonaje hutakaa ufanye lolote maishani mwako. Zamani nilikua na huu mtazamo mpaka yaliponikuta nilimpenda mwanaume namzidi miaka 3 na nipo nae hadi sasa. Kwa hiyo rafiki amua maisha yako bila kuwaza nani atakufikiria vipi.
Congrats and congrats again you have life to enjoy not to impress.....ila jamii inatupa mishale mizito sana lazima ujiandae haswa kuwashinda hawa backbiters
 
Congrats and congrats again you have life to enjoy not to impress.....ila jamii inatupa mishale mizito sana lazima ujiandae haswa kuwashinda hawa backbiters
Walishaanza ooh mbona mwanaume mdogo nawaambiaga haya ni maisha yangu waniache.
 
Naona ushapata jimama lako Sasa unatafuta justification hapa
Oa tuu hatuwezi kukuzuia

Nyie ndiyo mtaishi pamoja
Hahaha ondoa negative thoughts mkuu.......sisi kama jamii inatakiwa tulipokee hili bila kuhukumu
 
Wewe unadhani kwanini jamii ina mtazamo mbaya kuhusu mwanamke kumzidi umri mwanaume?

Ulishawahi kuzifahamu hizi hoja.
1. Umri mkubwa zaidi ni mamlaka, hekima, busara, mwenye kustahili kuheshimiwa na kusikilizwa zaidi nk.

2. Mwanamke anazeeka mapema kisayansi (mwanamke mwenye miaka 45, tayari huyo ni mzee kisayansi, hawezi tena kuzaa au kubahatisha kuzaa, anapoteza hamu ya mapenzi, hana tena msisimko imara wa kingono nk). Wakati umri huo kwa mwanaume ndio peak ya juu katika kuutafuna ujana.

3. Kisayansi mwili na akili za mwanamke zinakuwa haraka na kukomaa mapema kuliko mwanaume, hivyo mwanaume kumzidi umri mwanamke ni ili kutengeneza uwiano wa kuleta ufanisi wa kimaisha ya kindoa na familia.
 
Kumezuka wimbi kubwa la wanaume wengi wanaozama kwenye dimbwi la mahusiano ya kimapenzi na baadae sana wanagundua wapenzi wao wamewazidi umri kitu ambacho jamii ya kiTanzania inakichukulia kama kitu cha aibu na cha ajabu mno.

Kwenye kila taasisi kuanzia ya familia, makazini na nyumba za ibada uhukumu kwa ubaya sana wapenzi hawa na mala zote anayeonekana anamuonea mwenzake ni mwanamke kisa ni mkubwa kiumri.

Kitendo hiki kikitokea kwa mwanamke kuzidiwa umri na mwanaume kwenye mahusiano ya kimapenzi kinapokelewa kama kitu sahihi na kimekamilika , mwanamke anaweza zidiwa hata miaka 10-20 na mwanaume na jamii inaona ndio kitu sahihi na wengi wa wanawake hufurahia hili lakini punde tu !! Mwanamke anapomzidi umri yule mwanaume basi hao wapenzi husakamwa na kusimangwa kwa methali na nahau na vijembe kutwa kucha.

Jamii inabidi ibadilike sasa ....nawasilisha
Mkuu kama umesoma sayansi ya viumbe(Biology), utakubaliana na mimi kwamba viungo vya uzazi vya binadamu wa kike hutangulia ama tuseme huwahi kuzeeka(kukoma) (menopause).

Usishauri vijana wa kiume kuparamia wamama kuwaoa isipokuwa wawatumie kwa mahusiano ya kimapenzi pekee maana wanafaa sana.

Ni hasara kubwa kwa kijana wa kiume kuoa mwanamke aliyemzidi umri na makamo kutokana na sababu nilizozitaja hapo juu.

Inashauriwa watafute wenza wa kike wa kuoa wanaowazidi umri takribani kuanzia miaka mitano na kuendelea, umri huo ndiyo wataweza kuzeeka kwa pamoja kibaiolojia.

Na nani aliyekwambia, na tangu lini kipya kikathamanishwa na mtumba?
 
Mie mwanaume wa kumzidi umri namuona kama mwanangu.
Halafu naona kama vile atakuwa "haniweki vizuri" 🤣
Nadhani akinizingua naweza kumuwasha makofi.
Raha ya mwanaume anizidi umri, akili, elimu, urefu na uchumi.

#teambigboys#
Umeyasikia haya mtoa mada ewe mtakatifu Mwakyoma?
 
Back
Top Bottom