Jamii inayonizunguka inanipa mawazo sana ndugu zangu

Sikushauri uachane na huyo demu,Ila fanya Kama ume bet,ni wasichana wachache Sana wanao weza kukwepa mishale ya chuo,
Demu akikoswa na lectures atapigwa na vipanga wa class,akikoswa na hao atapigwa na mabishoo wa chuo.
 
kamwe usifanye kitu kwa kuangalia shinikizo la ndugu/jamii inayokuzunguka, hayo mashinikizo yachukulie kama changamoto coz changamoto ni sehem ya maisha, umenifurahisha kuona haubagui kazi, kwa huu uthubutu wako soon mungu atakubarikia na kila kitu kitakua sawia.

huyo dada we msubirie kwa sababu ameonesha nia coz anaijua hali yako vyema
 
Nimeona kama wewe ndio tatizo....

Kuna tatizo labda unalo ile kwavile sisi wanadamu ni bias hua tunaamini sisi hatuna matatixo,wenye matatizo ni wale wengine wanaotuzengua
 
umesema kutoka umerudi ukweni mapenzi yameongezeka niwazi wazazi wake wamekukubali kubwa ondoa hofu na mawazo yako yaelekeze kwenye kutafuta kz au pesa km ulivyoeleza jinsi ulivyosoma kwa tabu bila kukata tamaa basi na kwenye maisha pia usikate tamaa mtangulize Mungu wako.
 
Reactions: Cyb
Mkuu komaa kutafuta mtaji kama ulivyokomaa kutafuta ada yachuo..... Kwasasa ukiwekeza nguvu nyingi kutafuta kazi utajichosha bure namuda haukusubiri
 
Reactions: Cyb
MKUU nenda kijijini kwenu msimu huu wa maoteo muombe mtu utamsaidia kumsafishia shamba lake naimani utafanikiwa fanya hivo mkuu
 
Nimesoma uzi wako mpaka roho imeniuma umeandika kiunyonge sana mkuu.

Ushauri wangu.
1. Endelea kupambania kombe upate hela mzee.
2. Hakuna umri sahii wa kuoa usiteseke na mafanikio ya wenzako kuna waliofanikiwa na umri wa 25 na wakafilisika na umri wa 35. Na kuna waliofanikiwa at their 60's.
3. Binti lazima aende kusoma wakati ndio huu kuhusu hali ya chuo tumuachie maulana chochote kitatokea. Ila usipunguze uaminifu kwa kuwa yupo chuo. Big mistake.

I am at my mid 30's sijaoa ingawa nina watoto. Sijui naoa lini but kila nikitaka kuoa mambo yangu yanaharibika[emoji848][emoji848][emoji848].... So pambana
 
Huyo binti mwingine utamuoa bila kua na hela? Yaan wewe unahisi maisha ni sherehe ya harusi tu ambayo pesa yake huna hufikirii maisha halisi ya wewe na mtoto wa watu mtakayoanzisha,

Shida yako ni binti kwenda chuo unahisi utapoteza muda wa wewe kuoa na kuzaa kama ambavyo jamii yako inataka au shida ni binti kutaka sherehe?
 
Hahaaa halafu eti binti anamwambia haitaji pesa kwake ila apambane waishi maisha mazuri. Hivi hayo maisha mazuri yapo kweli bila pesa?
Haitaji pesa kwa sasa ndio maana hampigi mizinga ila anamshauri apambane atafute pesa sababu wana ndoto za kuanzisha familia, hao watoto wakija kuwaleta wataishi vipi kama wazazi wao hawana pesa?

Huyo Manzi ana akili sana, alipaswa amuoe huyo tena kabla hajaenda chuo, yaani yupo chuo tayari ni mke wake.
 
NGOSWE PENZI KITOVU CHA UZEMBE. HTOFANIKIWA KIMAISHA KAMA UTAENDEKEZA MAPENZI.

MUDA AMBAO AKILI YAKO INABIDI IFIKIRIE KUTAFUTA HELA NA KUBUNI MRADI WEWE UTAKUWA UNAWAZA MAPENZI TU.

UKIPENDA KUPITILIZA HATA UWEZO WAKO WA KUFIKIRI UNAPUNGUA SANA.

huyo binti akimaliza chuo na wewe ukiwa bado huna direction atakuacha, huyo ni mtu wa kaskazini anahitaji mtu mpambanaji.

Sent from my Infinix Zero 3 using JamiiForums mobile app
 
Akienda chuo msahau tu huna chako hapo , kwanini uwe unapata shida tafuta binti wa level yako mbona wanawake ni wengi tu,hatukuletwa duniani kuteseka furahia maisha uliekuwa nayo sasa
 
Mkuu usiwe na shaka, kikubwa zidisha ukaribu kwa kipindi chote atachokuwa chuoni, usitangulize hisia za fedha bali tanguliza hisia za kuushika moyo wake zaidi! Huyo anaonekana amekupenda kutoka moyoni.

NB: vyuoni kuna mambo mengi, jitahidi uwe unamtembelea mara kwa mara asipate upweke
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Brother pole bhan maana stori yako inafurahisha ingawa we unasema unakosa amani, ila chanzo kikuu cha ww kukosa amani ni umasikini tu wa kukosa pesa wala si mahusiano yako, yani ww stress zako zinasababishwa na kukosa pesa tu na wala si mahusiano yako wala umri wako, dat's all πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚, we binti ameshakaa poa kabisa yuko tiari kuishi na ww sasa sijui we unakwama wapi, tena umesema mwaka huu anaenda chuo kuchukua degree ambapo atatumia miaka si chini ya mitatu na huu muda wa miaka mitatu unatosha kabisa we kutafta pesa broo ili akimaliza tu unamweka ndani, nashindwa kuelewa unafeli wapi ww stress zingine unaendekeza mwenyewe alafu ukizingatia ww ni mtoto wa kiume hupaswi kuwa ivo broo.... Vijana kibao tuna degree tupo mtaani na hali halisi ishajulikana ajira hamna lakini sasa kama hajira hamna isikufanye ww uchanganyikiwe kiakili, umri n namba tu tafta pesa broo, we mtoto wa kiume unashindwa kabisa kutafta hata million moja kwa mwaka mpaka miaka mitatu dem wako anamaliza chuo unakuwa hata n million 3 unaanzisha kibiashara chako hapo huwezi lala njaa na dem wako broo.... Amka kifkra aisee usiisubiri serikali ikuamshe, hakuna ajira serikalin saiv, tena bora utafte pesa hata dem ukaja kumkosa badae ( maana madem wakiendaga chuo hubadilikia huko huko) ingawa ni probability ila sasa kuliko kukosa pesa alafu na dem ukamkosa ni hatari sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…