Jamii ya wahadzabe ilindwe, baada ya miaka 8 hawatokuwepo tena

Unawalinda ili iweje ikiwa wenyewe hawataki kulindwa? Wanataka kuishi maporini na kula vya bure na hawataki kulipia LUKU.
 
Wanyama wanapokuwa wapo hatarini kutoweka, serikali na wanasayansi huwa wanafanya utaratibu wa kuwachukua waliopo na kuwatengenezea (simulate) artificial environment ili wazaliane (rejea vyura vya Kihansi).
Labda wafanye hivyo pia kuokoa jamii ya wahadzabe sambamba na kupunguza mwingiliano na jamii hiyo.
 
Mbona ni mawazo kandamizi sana haya.
Ni sawa na Mwenyekiti yule kukalia chama miaka na mikaka.
Hayafai
Ni sawa na M7 kubakia miaka na mikaka madarakani,Haifai.
 
Hivi hawa jamaa, jamii yao Kuna familia/koo mbalimbali zikijitegemea au ni kundi Moja tu Lina move pamoja?
 
Soma post #4, mimi na wewe tuna fikiri sawasawa
 
Wasipewe Cocacola, kompyuta. Ni sawa na kuwanyima haki ya kuishi
Upuuzi mtupu kwani waliwahi kuja kuwaomba hizo coca-cola na kompyuta zenu?

Au bila hizo wao hawatapata furaha maishani mwao?

Wewe unayekunyw coca-cola na kompyuta mbona unalalamika maisha magumu kila siku?
 
Kudadadeki natamani nikutukane bongesa la mtusiiiii

Wewe huyo Charles Darwin umewahi kumuona?
Amekusaidia kwenye kupunguza ugumu wa maisha?

Pumbavu zako
 
Huwezi kushindana na usasa, hata wafichwe vipi watakutana tu na usasa......wao sio wanyama!
Wasilazimishwe waache waufuate wenyewe huo usasa
Wako huru na maisha yao msiwaingilie
 
Yan watu hamna akili,
Kwa hio wew upo happy binadamu kuishi vile karne ya 21?
Wale inabid wafanyiwe forced civilization kabisa, wapelekewe shule, hospital, wafanyiwe forced education, mpaka waelewe, tunapoteza madaktar wengi kwa kujifanya tunatunza asili za wamasai na wahadzabe
 
Kutaka Wahandzabe waendelee kuishi maisha ya kijima ili kulinda historia yao ni roho mbaya sana
 
acheni ujinga hatuwezi kuwaacha vile yani mtu anang'ata kopo la fanta tusimuelekeze namna ya kuifungua!!!
nao wanastahili kula,kulala pazuri na maisha standard binadamu tumeshatoka huko aisee!.
nao wanastahili elimu, na mambo mengine
 
Wewe una mawazo ya kishamba sana, kuwa civilized ndo nini?
Ndo kuishi katika ubepari? Mfumuko wa gharama za maisha na kupambana na magonjwa ya maabara?
Au kuhangaikia ajira ndo kuwa civilized?

Kuna ulazima gani kuishi katika "kuwa civilized" ikiwa wao wenyewe Wana furaha na maisha yao?
 
Yule mpishi anavyolamba mwiko hapana kwakweli, halafu wanapika utumbo wa Nyani ptyuuu .!!
 
Hayo maisha yao ni mazuri kwa upande wao
Hakuna stress kabisa
Hiki ndicho tunachokupigania
Waachwe, maana hata sisi tunaojiona tumestaatabika maisha yetu hayana nafuu yoyote zaidi ya Sonona na kuwafanyia kazi mabepari
 
kuna jamaa nilisoma nae ni muhazabe aisee jamaa nywele za kichwani zilikua hazioti kabisaa anakwambia anaweza kunyoa mara mbili tuh kwa mwaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…