New Designer
JF-Expert Member
- Aug 8, 2025
- 551
- 879
JamiiClub Sasa Rasmi Play Store: Live Streaming na Fursa Mpya kwa Watengeneza Maudhui
JamiiClub, bidhaa mpya rasmi na sasa inapatikana kwenye Google Play Store. Watumiaji wanaweza kuipakua na kuanza kuitumia.
JamiiClub inalenga kutoa suluhisho mbadala katika huduma za mitandao ya kijamii, ikiwemo Live Streaming kwa ajili ya kushirikishana taarifa na matukio kwa haraka ili kusaidia jamii kufanya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi
Platform hii inajumuisha vipengele vya Reels (video fupi), Live Streaming, Polls, Stories, Messages, na Music. Reels inalenga kuwapa watengeneza maudhui, hususan vijana walio jiajiri mitandaoni, nafasi ya kukuza ubunifu wao, kujenga hadhira na kutafuta fursa za kiuchumi kupitia maudhui ya kidijitali.
Pia, JamiiClub inaunga mkono matumizi ya Username, yanayorahisisha kujenga utambulisho wa kidijitali na kushirikisha viungo vya akaunti au biashara, kwa mfano: jamiiclub.com/Username. Hii inaweza kurahisisha wateja kuzipata biashara na kusaidia kujenga uaminifu mtandaoni.
Maono
Kwa muda mrefu, jamii yetu imekuwa ikitegemea platform za kimataifa kwenye live stream, kujiajiri (content creator), kupata habari za haraka kama Facebook, Instagram na TikTok. Dhamira ya JamiiClub ni kuchangia mabadiliko hayo kwa kuwezesha jamii ya Kiswahili kuwa si watumiaji wazuri tu wa teknolojia pekee, bali pia wabunifu wa suluhisho zinazoweza kushindana katika medani za kimataifa na kuchangia ukuaji wa uchumi wa kidijitali.
Baadhi ya picha za JamiiClub
Ofa kwa watumiaji wa mapema:
Watakaojiunga mapema na kuweka profile halisi za biashara zao na kuonesha bidhaa zao halisi watapewa verification badgebbila malipo au hawata hitaji kuhangaika kutuma verification badge requests.
JamiiClub ni hatua nyingine katika kujenga teknolojia inayotokana na ubunifu wetu, inayohudumia jamii yetu na yenye uwezo wa kukua kimataifa.
JamiiClub sasa inapatikana Google Play Store. Karibu ujaribu na uwe sehemu ya safari hii.
JamiiClub - Live stream - Apps on Google Play
Post stories & reels. Enjoy news, live streams, video calls, and connect.