Kaka, umewahi kumsikia huyo Nyerere akizungumza Kiingereza? Na yeye anachapia kama kawa, anasita kutafuta neno kama non-native English speaker wengi tulivyo. Tena kwa bahati niliyopata ya kuishi ng'ambo sana, naweza kusema Nyerere na Mkapa Kiingereza chao ni kibovu kuliko cha kwangu mara kumi, lakini hawa watu siwezi kufunga kamba za viatu vyao kwa upeo wa uelewa, busara, usomi n.k. Sasa tukianza kusema Kiranga ni genius kwa sababu anaongea lugha nne, babaake Msandawe, mamaake Mpogolo, kakulia Magomeni Kwa Bi Nyau, kasoma mpaka chuo kikuu, na anapenda penda lugha, of course atakuwa anajua lugha nne! Unajua?
Sio tu hayatumiki katika lugha ya kawaida, bora ingekuwa hayatumiki katika lugha ya kawaida. Kiingereza cha Kiranga mara nyingi kinavunja misingi ya sarufi, ni broken!
Kwa mfano:
Kiranga: The sheer parochial absurdity of this stale regiment of a thinly disguised chicanery exposes a poor attempt -if not grave wanton for respect of individuals- at humorous serendipitous eccentricities of Piddletrenthide proportions.
Neno "wanton" mara nyingi ni adjective, lazima lifatiwe na noun, hicho kinachosifiwa. Huwezi kusema, kwa mfano, the guy is wanton! Wanton what? Au, ukitaka kulitumia kama noun, lazima liwe lina discribe mtu, sasa hapa kinachosemwa ni wanton ukirudi nyuma unakuta ni neno attempt. Kusema "attemp wanton" ni broken English!
Halafu kingine, kwenye kiingereza kilichoandikwa vizuri huwezi kukuta sentensi ina of, of, of zaidi ya mbili. Cheki alivyosema: of this stale regiment ... of a thinly disguised ....of Piddletrenthide proportions. Unaona kuna ka tatizo hapo? Sijui unanielewa?
Halafu anapenda kujirudia rudia bila sababu: Kiranga: and evade eerie effable ephemeral enchantments with enviable equanimity while embarking from this putrid pungent pugilists pantomime, to a somber soliloquy of solitary sanity..... hapa keshasema ana evade hizi enchantments with enviable equanimity, yani kwa aina fulani ya ukimya, utulivu, halafu mwisho wa sentensi anarudia tena kusema anakwenda kwenye utulivu fulani, upweke wake...somber soliloquy of solitary... kasahau alipoanzia, anaanza kujirudia. Pia neno neno putrid na pungent hapa yana maana ile ile tu.
Kwa hiyo kwa sababu ya haya mapungufu ya kisarufi, kimantiki, kukosa viima na viarifu kwenye sentensi zake, Kiingereza hiki sikioni kama kina umakini sana. Sasa ukiandika hivyo halafu ukawa unasomwa na kina J Mushi, you know, mchaga wa milimani Machame huko sijui wa wapi huyu, of course atamuita genius! Sijui unanielewa? Wewe Nyani huwa nakuona unaandika andika viingereza viingereza hapa, lazima una vi idea idea na ninachokisema, nadhani unanielewa....