JamiiForums: Unaweza kuwa VERIFIED, fuata hatua hizi

JamiiForums: Unaweza kuwa VERIFIED, fuata hatua hizi

Maxence Melo

JF Founder
JF Staff
Joined
Feb 10, 2006
Posts
4,324
Reaction score
13,967
Wakuu,

Kumekuwa na maombi kadha wa kadha ya watu kutaka kuwa verified.

Tumeona vema tuweke urahisi wa mtu kuomba kuwa verified badala ya utaratibu wa awali. Kuwa verified kwako ni kwa hiari yako. Unaweza kusoma Sera yetu ya Faragha kama una concerns zozote > Privacy policy ambayo ina ufafanuzi wa kina.

Kwa wanaotaka kuwa verified, utaratibu utakuwa kama ifuatavyo:

Utabonyeza (ukiwa kwenye web browser) sehemu imeandikwa Account, kisha fuata utaratibu huu:

89C8D037-99A8-4DD3-B1AF-035A03EFDF0B.jpeg


Utabonyeza "Request Verification Badge". Utaweza kuona sehemu inakuja na eneo la kuweka ujumbe wa kuwasiliana nasi ukiambatanisha na copy ya ID inayothibitisha majina unayotaka yawe verified ni yako

Screen Shot 2021-08-19 at 12.24.49.jpg


Ukishatuma request, vumilia kidogo kwani itakuwa processed na ikiwa ina changamoto progress itaonekana kwako baada ya sisi kuwasiliana nawe kuhusu ombi lako.

Profile yako au ya mdau mwingine, ukipeleka cursor itaonyesha maandishi haya (mfano):

Screen Shot 2021-08-19 at 14.30.45.png


ILANI:
1) Kwa waliokuwa verified awali, huna ulazima wa kufanya mchakato huu, lakini ikikupendeza kujaribu - UNAKARIBISHWA
2) Unaweza kuwa verified ukiwa na ID yako ya JF (not a real name) endapo tutajiridhisha kuwa ID ni mtu tunayefahamiana naye na maudhui ya akaunti yake hayashushi hadhi ya badge husika; mfano wa waliokuwa verified kwa IDs kawaida ni Bujibuji na Madame B.

Wanachama ambao ni VERIFIED wataonekana hapa: Verified Members

NB: Napokea requests nyingi za kubadili majina, tafadhali fanya hivyo mwenyewe kwa kutembelea https://www.jamiiforums.com/account/username

Asante
 
Back
Top Bottom