JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

[emoji87] [emoji87] [emoji87] sawa mlinzi wa zamu...kumbe tunakupa kampni ee
Tena for free kabisaa,cha msingi nahikisha nna ile dawa ya mbu ya kupaka tu hapo ni full kukesha tu
 
Ni kweli kabisa ila mkuu ukikosa usingizi plus upweke ni hatari kabisa kama hapa naona chumba kimeongezeka ukubwa

sent from kuzimu
Aisee kama ni upweke basi ni mwendo wa kutafuta company ya jinsia ya upande mwingine tu.
 
Hivi kuna tofauti sana kati ya upweke na msongo wa mawazo au lipi lina afadhali kiasi?

Upweke unaweza kupelekea msongo wa mawazo, kwa mtazamo wangu afadhali ya upweke kuliko msongo wa mawazo. Ukitafakari sana, yote ni mambo ya kufikirika tu! Upweke unakuaje? Mbona wengine wanapenda upweke na ndio maisha wanayoyafurahia?

Msongo wa mawazo hali kadhalika, jambo unaloliona mzigo au kikwazo kiasi cha kukukatisha tamaa kwa mwingine hata halimsumbui kabisaaa.
Inategemea unalichukuliaje na una weza kukabiliana nalo kwa mikakati ipi. Wengi tunachachawa kama sio kupagawa sana tunapofikwa na mambo.

Kuongea kunasaidia sana, unawezasema jambo au tatizo linalokusibu ukashangaa unapata ushauri au msaada ambao hsukuufikiria na umeshaumia sana na tatizo.
 
Hivi kuna tofauti sana kati ya upweke na msongo wa mawazo au lipi lina afadhali kiasi?
Tofauti ipo mkuu, ila ukicombine vyote ni hali tete zaidi bora uwe na msongo wa mawazo na upo na mtu pembeni unaweza kumwelezea kinachokusibu akukupa ushahuri tofauti ukiwa peke yako hapo utajaribu kutafuta majawabu ya mawazo yako ukaishia kuongeza mawazo

sent from kuzimu
 
Ni kweli kabisa ila mkuu ukikosa usingizi plus upweke ni hatari kabisa kama hapa naona chumba kimeongezeka ukubwa

sent from kuzimu

Pole sana. Upweke kwa wengine ndio maisha wanayoyapenda na kuyatamani.
 
Back
Top Bottom