JamiiForums ya Maxence Melo imenipatia mume. Clepatina naolewa

Man you are right. We wish them best πŸ‘Œ
 
Mbona fasta Sana,
Yule yule jamaa alikuandikiaga Uzi au mwngn?
Wananzengo tayari wanasema eti ni ID moja inajinywesha chai na kujipulizia. JF bana 😁😁😁

Hekaheka mpya za mama J. lini tena mkuu au mpaka ajilipie rent kwanza ndo tunapata episode mpya? 😁😁😁
 
Kanuni kuu ya kuoana ni moja tu upendo

Oa au olewa na mtu kwa kuwa unampenda sio ohh naoa au au namhurumia au sababu nina stress au nataka kumpunlguzia stress wewe sio ofisa wa ustawi wa jamii au mshauri nasaha wa wenye stress

Upendo pekee ndio unatakiwa kuwa mwamuzu na upendo na mtu unayemjua vizuri

Hizi ndoa za matchmaking za mitandaoni nyingi future huwa hazina future nzuri

Anyway ulichofanya mleta mada ni trial and error lakini sio best way ya kupata mke au mume unless una malengo ya mafupi ya kuchumchuna au kupata fursa fulani toka kwake yakikamilika kuwa hata mkibwagana it doesn't matter to you mission accomplished
 
Kila kitu kikitumika vizuri kinaleta matokeo chanya na kikitumika vibaya kinaleta matokeo hasi. Kuna msemo unaotumika katika computer inasema "Garbage in Garbage out"

Nasema hivi kutokana na baadhi ya wanawake humu wanajiheshumu,wanapenda kuolewa na kutulia, wanamaanisha na pia kutokana na changamoto ya maisha ya kimapenz,wamedharauliwa,kunyanyaswa,na hata kuvunjika moyo kutokana na mateso ya mapenzi na manyanyaso na hivyo wanapenda kuwa na wapenzi wa chaguo lao na kufaidi mapenzi matamu.

Shangaa Sasa wapo wanawake na wanaume walioko serious, wengine na malaya tu humu ndani, utashangaa mwanamke anataka kuolewa ila ukimtafuta basi dk chache hana hela ya kula,kafiwa,hana hela ya saluni,nyumba anayokaa anadaiwa Kodi,hana vocha, ana shida binafsi anataka hela,mara akutumie picha za nusu utupu,mara anataka nguo aende kwenye harusi,mara anaumwa. Hivyo vyote hata siku haijaisha. Ukimtumia hela tu anakublock. Hao ndo wanaharibu taswira ya wengine wanawake walioko serious.

Kwa upande wa wanaume utasikia maneno mengi Sana,mara ooooh, huna mwanaume, hujawahi kuwa na mwanaume, kwenu huko hakuna wanaume,una chura,piga picha sura yako tuione, wewe unataka mwanaume basi ni malaya tu nk.

Anyway humu kuna walioko serious na walioko na utani na ujinga mwingi, nk. Yaani kwenye msafara wa mamba na kenge wamo.

Cha msingi ni kutambua walioko serious na walio choko ndo ugumu uliopo. Otherwise humu pangekuwa na sehemu salama kwa wale wasio na wanaume au wanawake kutafuta wenza wao hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…