JamiiForums ya Maxence Melo imenipatia mume. Clepatina naolewa

JamiiForums ya Maxence Melo imenipatia mume. Clepatina naolewa

"Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa Bwana."
MITHALI 18:22.

Wapendwa nilitaka nipotee kimya kimya, ila kwa namna hii ID yangu ilikaribishwa kwa upendo na kwa upendo nilionao kwa marafiki na ndugu zangu zangu niliojipatia hapa JF nimeona sio ubinadamu nikaitelekeza hii ID bila kuwaaga halafu niwaache wapendwa wangu wakijiukiza Clepatina kapatwa na nini mbona kapotea jukwaani.

Wapendwa, Mungu akitoa kibali November ninaolewa na mchumba niliyempatia hapa JF.🤣❤️.

Huyu jamaa hajanikuta single. Alinikuta nikiwa kwenye uhusiano na jamaa ambae hata hapa jukwaani nishawahi kumtaja kama Mgweno.

Kwa huyu mgweno ndiko moyo wangu uliko. Nilimpenda sio kwa moyo wangu wote bali kwa vyote vilivyotumika kuniumba. Nilimpenda sana huyu mwanaume kiasi cha kuwaona wanaume wengine wote walionitongoza kama wachumba tu🤣.

Baadae nikagundua ninampenda Mgweno zaidi ya anavyonipenda na nikawa mtu wa kulalamika kila siku.

Hata hivyo Mgweno ndio aliyesababisha huyu shemeji yenu mpya atangaze ndoa fasta fasta.

Ni hivi,wakati nakutana na Mgweno nilikua na stress sanaa kiasi kwamba nilikua naonekana kama nina mara mbili ya umri wangu. Nilikua nimechoka sana. Nilikua kibibi🤣 lakini mahaba na faraja alizonipa Mgweno zikarudisha peace of mind na stress zikaisha na Clepatina nikawa pisi kali tena🤣.

Amini usiamini, mwanamke akipendwa na mwanaume anayempenda uzuri wake unarudi🤣. Ndio maana mtu ukiwa single hufatwi ila ukipata tu wa kukupenda utashangaa kila mwanaume anakutaka🤣.

Sasa baada ya kuona Mgweno haeleweki/kabadilika nikapambania penzi haijasaidia, ndio kajitokeza huyu shemeji yenu mpya na japo hatuna muda mrefu na siwezi kusema namjua vizuri ila nafsini mwangu nahisi amani juu yake.

Kwa hatua alizochukua na gharama alizoingia juu yangu nina imani yuko serious katika kutaka kunioa.

Yeye na familia yake yote ni walokole kama mimi na ninajihisi salama kuwa mikononi mwa mwanaume amchae Mungu.


Ndugu zangu, mwanaume Mcha Mungu, msomi, mwenye ofisi zake kubwa kubwa, handsome, mpole ila mkali kwenye upuuzi, asiyependa wanawake wengi na mwenye mapenzi kama kapewa limbwata, hatoki kokote zaidi ya Mbinguni kwa baba Mungu, Mungu wa ishara na miujiza. Mgweno anisamehe ila naamini huyu ndie niliumbwa toka ubavuni mwake❤️.

Hii itakua ni post yangu ya mwisho hapa. Kwa sasa najikita zaidi kusoma biblia kama alivyoniomba mume wangu mtarajiwa na pia kutumia free time yangu kujifunza kupika. Sijui kupika ndugu zangu😭 na shemu wenu kasema kutojua kwangu kupika ni tatizo na mpaka siku ananioa niwe nimeshajua kupika.

Najua ndoa zina changamoto, najua mume wangu mtarajiwa atakuwa na madhaifu yake, najua kuna siku za kulia na siku za kucheka najua kuna siku tutapata na kuna siku tutakosa najua kuna mengi mazuri na mabaya yatajitokeza ila hata itokee nini kamwe sitafanya yafuatayo;

1) Sitamcheat hata akipoteza dushe yake.

2) Sitamdharau hata akikosa uwezo wa kunipa jero.

3) Kamwe sitajiona nina akili kumshinda.

4) Kamwe sitapaza sauti yangu ninapoongea nae.

5) Kamwe sitonyanyasa watoto wake ambao mama yao amefariki, kwani tayari nawapenda na wao wananipenda kama nimewazaa mimi.

Kwa mnaonipenda naombeni mniage kwa neno zuri la ushauri.

Joannah Half american Gily
I CAME, I SAW, I CONQUERED
Sitamcheat hata akipoteza dushe yake.

2) Sitamdharau hata akikosa uwezo wa kunipa jero.

3) Kamwe sitajiona nina akili kumshinda.

4) Kamwe sitapaza sauti yangu ninapoongea nae.

5) Kamwe sitonyanyasa watoto wake ambao mama yao amefariki, kwani tayari nawapenda na wao wananipenda kama nimewazaa mimi........

( ushauri wangu kayafanyie kazi haya maneno na MUNGU akakufanyie njia )

haya maneno yakawe
nguzo zaidi sana mwombe MUNGU akuwezeshe ikawe maisha ya kheri kila baya likapate mlango wa kutokea .... kama una muda sema AMINA 🙏
 
Ninavyopenda kula Ubwabwa wa sherehe nahisi Novemba pamekuwa mbali 😋😁

Hakikisha kwa namna yeyote X wako anapata Kadi ya Mwaliko ili ajifunze aliposema Wanini kuna Watu walijiuliza Watakupata Lini 🏃🏃🏃
 
Hongeraaa sanaa uduguuu kwa kupata ubavu wako.
MC nipo hapaaaa bureee kabisaa kuchachua na kunogeshaa harusiii. [emoji8][emoji8][emoji8][emoji182][emoji182]

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hahahaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787] yani ujanja wote kama sungura ila kupika ni zero...[emoji1787][emoji1787][emoji1787] kumbe bado huja qualifie kuitwa wife material... Nahisi kuna mengi huyajui pia[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Kuachwa, kuachwa aaaaaa

Kuachwa ni shughuli pevuuu

Mbaya zaidi, yule uliyempenda

Wewe unakonda, mwenzako ananenepa

[emoji1787][emoji1787][emoji1787] bro vipi [emoji870] nakusalimia
 
Habari Clepatina...

Natumai ni mzima sana na mwenye utimamu sana, Naomba niseme hongera sana kwa uamuzi uliochukua...Sidhani kama ulishawahi kuwa ndani ya ndoa hapo awali, Lkn kwa maelezo yako ulikua na mahusiano na somebody mgweno....Sijui ulimpenda na mkapendana ila ikafika sehemu akaondoa upendo kwako! Naomba nikuulize ulishajiuliza ni kwa nini alifanya maamuzi hayo ya kupoteza upendo wake kwako!?

Sasa unaelekea kuingia kwenye ndoa au niseme unaenda kuijenga familia mpya na mwenza wako...Nikusii tu ili kuinusuru hii ndoa yako na iweze kudumu usirudie makosa uliyofanya hapo awali na ukawe mama bora mwenye maadili mazuri kwa watoto wako, Jifunze kuheshimu hisia za huyo mlokole.

Sina mengi nikutakie amani ya moyo na baraka kwenye hatua yako pia...

Hongera na Ahsante sana..
 
Back
Top Bottom