TUSHIRIKISHANE JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane"

hongera sana mmepiga hatua kubwa sana yaani mmenifanya nifurahie sio kukaa na kulumbana bali kufanya kazi pamoja kwa kushirikiana mmepiga hatua ndefu sana mje sasa na mikoa mingine basi tuone haya maendeleo
 
Hongera Max na JF.
Kumbe inawezekana... nadhani mmetimiza jambo moja katika ushauri wa Rais.. wabunge na waliochaguliwa wajadiliane nawapiga kura wao jinsi ya kuleta maendeleo katika eneo lao. Hongereni JF
 
Wadau wa JamiiForums,


Leo wananzega tumefaidika na semina inayoendeshwa na Jamii Media ambayo ni zao la JamiiForums. CEO wa JamiiForums ndugu Maxence Melo ametuelewesha mengi kuhusu JamiiForums lakini kubwa zaidi ilikuwa ni kutoa elimu juu ya uwajibikaji wa viongozi juu ya miradi ya maendeleo katika eneo husika. Tumeshirikishana mengi kama kauli mbiu inavyosema “Tushirikishane".
 
Mimi nafanya Katika moja ya mamlaka ya serikali za mitaa nchini. Siamini kama kwa sasa kipaumbele kwa wananchi ni hicho kinachofanywa na Jamii Media.
Wananchi kwa sasa wanahitaji huduma bora za kijamii, miundo mbinu,mlo bora nk. Siyo hayo ya kuwasiliana kwa namna mradi huo unavyotaka. Na ushahidi wa kwamba mradi huo hautapata mwitikio siku za usoni ni pale hiyo ofisi ya afisa mahusiano kutokutumiwa na wadau.

Waendesha mradi wasihadaike na idadi ya watu waliojitokeza kwenye ufunguzi wa mradi. Ni sawa na siku ya kikao cha kwanza cha kamati ya harusi. Watu hujitokeza siku hiyo ili wafaidi na vilivyopo. Na baada ya hapo mahudhurio husua husua.
 

Mkuu Tuko, nilivyoelewa mradi utatoa platform kati ya mbunge/ diwani/ halmashauri na wananchi waliopo kwenye sehemu anayoingoza. Kwa mfano mbunge anasema katika ahadi X niliyoitoa nimefuatilia, nimefikia sehemu kadhaa, vinavyokwamisha ni kadhaa na majadiliano yao yanaweza kuwa sehemu ya suluhisho.

Pili ambalo kwangu naona ni muhimu sana, mtu akijua kuna watu wanaangalia na wako macho ni rahisi nae kukimbizana huko anapaosaka hayo maendeleo na kuja kushirikisha wananchi wake. Mbunge/ madiwani na wananchi wanaweza kuchagua vipaumbele vyao kwa pamoja kuliko baadhi kujifungia ndani na kuwachagulia wengine.

Kwa uelewa wangu mkuu..
 
Nadhani mrad wao una mantik endapo utapata fursa ya kuwasikiliza maana lendo la mrad ni kuleta awareness kwa wananchi juu ya mirad mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na serekali. Mi nimehudhuria jamaa wana nondo za maana sana.
 
Hatua nzuri Jamii, itaboresha dhana ya uwajibikaji kwa kutengeneza uwazi kwenye kutimiza malengo na ahadi za wananchi.

Ombi langu kwa wanajukwaa wenzangu, kama wahusika wakiletwa humu basi tuwashambulie kwa hoja na sio personality na mihemko, naamini italeta manufaa sana hasa kwa wale ambao wamekimbia walikotoka kutafuta maisha sehemu nyingine kwani hawataweza kushirikishana mawazo yao ana kwa ana majimboni.
 
Mfumo uliopo wa mawasiliano nchini unawawezesha wananchi kupata taarifa zozote zinazowahusu. Sidhani kama kuna kipya kitatolewa na huo mradi.
 
This is a routine maintenance ya JF.
Siku zijazo pawepo na exclusive interview au Awards kwa members.
Hongereni sana Wakuu.
 
Mfumo uliopo wa mawasiliano nchini unawawezesha wananchi kupata taarifa zozote zinazowahusu. Sidhani kama kuna kipya kitatolewa na huo mradi.
The issue is ni mwananchi wa aina gani anaeipata hyo taarifa, na kikubwa ni uwaz wa taarifa husika. Kuna mpango jamaa watakuja nao nadhan utawork out.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…