Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Kikalio ni kitu cha kuheshimiwa sana kwenye tamaduni nyingi.. Unapofika kwa mtu cha kwanza unachopewa ni kikalio... Kikalio chaweza kuwa kiti, jamvi au mkeka! Kiti ni mjumuisho wa kochi, stuli ama kigoda!
Kwa tamaduni za pwani ni nadra kukuta viti ndani ya nyumba .. Na hii inatokana na ama athari au mazoea ya kutawaliwa na waarabu...Kwahiyo kwa tamaduni za Pwani kikalio ni jamvi, jamvi ndio kama kiti na kila familia haikosi jamvi maalum la wageni na hili huwekwa nyuma ya mlango varandani.. Halikatizi zaidi ya hapo.
Mgeni akija litakunjuliwa akaribishwe akae na akiondoka litakunjwa na kurudishwa mahali pale. Huwezi kukaa bila kulikanyaga jamvi na huwezi kuinuka uondoke bila kulikanyaga jamvi. Hapo kabla iliaminika kwamba mwanamke hapaswi kuwa na wanaume wengi.. Hivyo alipotokea mwanamke wa namna hiyo basi alipewa jina la jamvi la wageni
Kutoka hapo ndio ikatungwa nahau ya kiswahili ya jamvi la wageni...!
Kwa tamaduni za pwani jamvi la wageni halina heshima, kwakuwa linakanyagwa na wengi na kukaliwa na wengi pia..halina maalum, wote wake!
Kwanini sasa jamvi la wageni awe mwanamke na si mwanaume?
Ni kwa vile kwenye kufanya matusi yanayoitwa ngono mwanamke ndio hulala ama hutangulia chini .!! Kumbuka wageni wa kupita ndio hupewa jamvi la wageni!
Kuna baadhi ya tamaduni hapa Afrika ukifika ugenini nyumba utayofikia wewe kama ni mwanaume lazima upewe binti mmojawapo wa kukuliwaza usiku.. Sasa sijui kama huyu naye anaweza kuwa jamvi la wageni!!!PENGINE.

- Wenye vijicho linapokea.
- Wenye kimavi linapokea.
- Washirikina pia.
- Wambeya.
- Wezi na kila aina ya watu halina jinsi ya kuwakataa.