Jamvi la wageni

Jamvi la wageni

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Kikalio ni kitu cha kuheshimiwa sana kwenye tamaduni nyingi.. Unapofika kwa mtu cha kwanza unachopewa ni kikalio... Kikalio chaweza kuwa kiti, jamvi au mkeka! Kiti ni mjumuisho wa kochi, stuli ama kigoda!

Kwa tamaduni za pwani ni nadra kukuta viti ndani ya nyumba .. Na hii inatokana na ama athari au mazoea ya kutawaliwa na waarabu...Kwahiyo kwa tamaduni za Pwani kikalio ni jamvi, jamvi ndio kama kiti na kila familia haikosi jamvi maalum la wageni na hili huwekwa nyuma ya mlango varandani.. Halikatizi zaidi ya hapo.

Mgeni akija litakunjuliwa akaribishwe akae na akiondoka litakunjwa na kurudishwa mahali pale. Huwezi kukaa bila kulikanyaga jamvi na huwezi kuinuka uondoke bila kulikanyaga jamvi. Hapo kabla iliaminika kwamba mwanamke hapaswi kuwa na wanaume wengi.. Hivyo alipotokea mwanamke wa namna hiyo basi alipewa jina la jamvi la wageni
Kutoka hapo ndio ikatungwa nahau ya kiswahili ya jamvi la wageni...!

Kwa tamaduni za pwani jamvi la wageni halina heshima, kwakuwa linakanyagwa na wengi na kukaliwa na wengi pia..halina maalum, wote wake!
  • Wenye vijicho linapokea.
  • Wenye kimavi linapokea.
  • Washirikina pia.
  • Wambeya.
  • Wezi na kila aina ya watu halina jinsi ya kuwakataa.
Na ndio maana linakunjwa na kuwekwa nyuma ya mlango barazani.. Ili kama kuna aliyekuja na nuksi zake au jhanaba zake akiondoka zisiende kwa wanafamilia bali zikunjwe aje kuondoka nazo mgeni mwingine!

Kwanini sasa jamvi la wageni awe mwanamke na si mwanaume?
Ni kwa vile kwenye kufanya matusi yanayoitwa ngono mwanamke ndio hulala ama hutangulia chini .!! Kumbuka wageni wa kupita ndio hupewa jamvi la wageni!

Kuna baadhi ya tamaduni hapa Afrika ukifika ugenini nyumba utayofikia wewe kama ni mwanaume lazima upewe binti mmojawapo wa kukuliwaza usiku.. Sasa sijui kama huyu naye anaweza kuwa jamvi la wageni!!!PENGINE.

1625116747558.png

 
Kama msemo huo ungekuwa urembo basi leo hii tungeuita pete inayovaliwa na wanaume na wanawake, maana wapo wanaume wakiona mwanamke mgeni mitaa yao macho ti ti ti kama saa ya disco...
 
Kikalio ni kitu cha kuheshimiwa sana kwenye tamaduni nyingi.. Unapofika kwa mtu cha kwanza unachopewa ni kikalio... Kikalio chaweza kuwa kiti, jamvi au mkeka! Kiti ni mjumuisho wa kochi, stuli ama kigoda!

Kwa tamaduni za pwani ni nadra kukuta viti ndani ya nyumba .. Na hii inatokana na ama athari au mazoea ya kutawaliwa na waarabu...Kwahiyo kwa
Sisi tushazoea kukalia kile kichanja cha watoto kina chotengenezwa ili mtoto anaeanza kujifunza kusimama ili miguu ikomae unaenda kumsimamisha hapo anajishika ili asianguke[emoji3][emoji3]
 
Umenena vyema, msemo wa jamvi la wageni unatumika kama lugha kificho kumuelezea mwanamke mwenye tabia za kimalaya, yaani yule asiyebagua wala kuchagua. Jamvi la wageni kama ulivyosema utumiwa na kila mtu,yaani huwezi kukataa kulitoa hata kama haujui dhamira ya ujio wa mgeni mwenyewe, vivyo hivyo mwanamke ( Jamvi la wageni) hamkatai mwanaume kwake kila mwanaume akiomba bila kipingamizi upatiwa mwanamke anaweza kuwa jamvi la wageni kwa sababu mbalimbali, ila wanawake wengi wao urithi kutoka kwa mabibi( laana), hawa hawawezi kubadilika katu.

Mwanamke mwenye sifa za jamvi la wageni kidogo naweza kusema ana utofauti na Mwanamke Malaya wenye dhumuni la kujipatia kipato, jamvi la wageni, wageni hawalipi kitu kulitumia, yaani kufika kwao kwenye nyumba waliyotembelea ni sababu tosha ya kulitumia jamvi hilo, vivyo hivyo na kwa mwanamke mwenye sifa za jamvi la wageni, yeye hayupo kibiashara yoyote atayeomba anampatia pasipo kujali kama atapewa fedha au laah.

Mtumiaji akimaliza haja na kwenda zake bila kutoa kitu yeye wala hajali tofauti na Malaya ambaye anafanya biashara mteja hasipolipa kivumbi kitatimka. Mwanamke malaya anayefanya biashara mimi naweza kumfananisha na choo cha kulipia yaani hauingii bila kulipa na kila mwenye hela uweza kumwaga uchafu wake na kwenda zake.​
 
Sisi tushazoea kukalia kile kichanja cha watoto kina chotengenezwa ili mtoto anaeanza kujifunza kusimama ili miguu ikomae unaenda kumsimamisha hapo anajishika ili asianguke[emoji3][emoji3]
Kikoje icho? Au unamaanisha kigoda?
 
Umenena vyema, msemo wa jamvi la wageni unatumika kama lugha kificho kumuelezea mwanamke mwenye tabia za kimalaya, yaani yule asiyebagua wala kuchagua. Jamvi la wageni kama ulivyosema utumiwa na kila mtu,yaani huwezi kukataa kulitoa hata kama haujui dhamira ya ujio wa mgeni​
Duh. Asante umefafanua vizuri sana .. Tunaweza kusema basi jamvi la wageni ni sawa na ule usemi mwingine wa maharagwe ya Mbeya! Chupi mkononi.. Yaani unacho huna yeye poa tu.. Hata kama umemtania yeye anajua unamaanisha! Ni kweli kabisa baadhi ya majamvi ni laana za wazazi, ndugu wa karibu au ukoo.. Na cha kushangaza wala hawapati magonjwa
 
Halafu inakuwaje unakuta mtu kaiba Jamvi la Wageni. Au kaoa Jamvi la Wageni!
 
Back
Top Bottom