Binti wa zamani
Platinum Member
- Nov 19, 2011
- 15,052
- 36,866
Mwaka ndiyo kwanza umeanza ila humu jukwaani zimejaa nyuzi za makasiriko, malalamiko, vijembe; “wanawake hawana mchango wowote?", “kwanini mnazeeka na hamuolewi?” mara "mna nini cha ku-offer? au "nyie ni kunguni tu mnanyonya wanaume hamuwanufaishi" na nyingine nyingi.
Njooni tuzungumze:
Njooni tuzungumze:
- Unafikiri ni aina gani ya wanaume wako nyuma ya hizi ID za nyuzi za makasiriko na kuwasema wanawake?
- Vitu gani inabidi hawa wenzetu wajifunze kuhusu wanawake ili waendane nasi kwenye ulimwengu wa leo?
- Je, ni kweli kwamba sisi ndiyo tatizo na hatueleweki ni nini tunataka? au tukiwaambia tunachotaka hawasikilizi?
- Ushawahi shuhudia mtu anapigwa tukio ukajisemea, kwa hili hata shetani anachukua notes 😂 .
- Seran na wenzako, mmewafanya jambo gani hawa ndugu zetu wa JF, mbona kama wamevurugwa mapema sana?